NA BASHIR YAKUB-
Makuzi
ya biashara hasa biashara za kimataifa yameleteza utitiri wa makampuni. Karibia
kila biashara kubwa au ya kati kwa
sasa hufanywa na makampuni. Baadhi ya
ndani na mengine ya nje. Hatua hii njema kwa kiasi fulani imeongeza ajira
japo ajira zenyewe hazina vigezo vya kuitwa ajira. Yatosha ziitwe kazi
tu. Ajira hizi ambazo nyingi ni za
umanamba zimekuwa zikifanywa na wazawa. Upande mmoja zimekuwa neema na upande
mwingine zimekuwa laana. Ni neema kwakuwa baadhi wanaweza kuishi japo kwa pato la mlo tu na kusiwe na akiba
yoyote lakini pia zimekuwa laana kwakuwa ukihadithiwa baadhi ya mambo yanayoendelea
huko waweza toa chozi.Sio pote ila yapo maeneo yaliyoshindikana kama viwandani,
migodini, miradi ya barabara na kwingineko waliko wawekezaji hasa wa kigeni.
Hili ndilo limenituma kuandaa makala haya ili basi wenye fursa wasome na waelewe na wenye kutaka
msaada waweza kuwasiliana nami na kuona la kufanya.
Nianze
hivi, kampuni kwa mujibu wa sheria ni mtu( legal person). Kuna tofauti kubwa kati
ya kampuni na mmiliki wake. Kisheria kampuni
ikifanya kosa yatakiwa ishitakiwe
kampuni na sio wamiliki au mfanyakazi
kama mameneja, mkurugenzi n.k. Nimewaona wengi
hasa vijana ambao huyadai makampuni
haki zao hufungua kesi wakiwashitaki
wamiliki au mabosi wao. Hili ni kosa kubwa na wengi wao huwa wanashindwa
zile kesi na badala yake kuanza kulalamikia mfumo wa nchi , mahakama
au viongozi na hata chama tawala.
Ndugu hili halikusaidii. Hili sio la serikali wala rais wala nani ni suala ka
kisheria. Kampuni yako imekukosea unataka kudai fidia umemshtaki mmilki au
viongozi badala ya kampuni, ni lazima utashindwa kesi usimtafute mchawi wala kulalama kwa tuhuma za rushwa.
Unapokosea taratibu sheria haina huruma
inakata. Upo msemo usemao ( A law is a
merciless sword) yaani sheria ni upanga usio na huruma unamkata yeyote
anayeuchezea. Kampuni kama kampuni inao
uwezo wa kushtaki kwa jina lake na kushtakiwa kwa jina lake,namna gani tutaona hapo chini.
1.MAKOSA AMBAYO MAKAMPUNI HUWATENDEA WAFANYAKAZI
Makosa
ni mengi ila haya ni baadhi na ya mara
kwa mara. Kufukuzwa kazi bila kupewa stahili,
au kupewa kidogo, kuumia kazini bila kupewa matibabu, au kuumia kwasababu ya
kutopewa zana za kufanyia kazi kama kofia ngumu, viatu vizito( boots), mkanda
wa kiunoni kwa wajenzi majengo marefu, miwani wanaochomelea, kufukuzwa kazi
bila kupewa nafasi ya kujitetea au
kuhojiwa, kufukuzwa kazi bila notisi,
kutopeleka hela za mafao ( NSSSF, PPF n.k) ya wafanyakazi kwenye mifuko yao
huku mfanyakazi akikatwa kila mwezi, kuvunja
mkataba bila sababu za msingi au kwa hila,kumtukana, kumpiga au kumdhalilisha
mfanyakazi kwa namna yoyote ile( hasa makampuni ya Wahimdi), kutolipwa mshahara
kwa wakati au kutolipwa kabisa au
limbilkizo la muda mrefu, na makosa mengine mengi.
Makosa
kama haya huwezi kumfungulia mmiliki wa kampuni
au bosi wako kesi ukashinda. Ni lazima
tu itatupiliwa mbali kwa kumshitaki asiyehusika.
2. NAMNA GANI KAMPUNI
HUSHITAKIWA.
Kampuni
yoyote ina jina na unapotaka kufungua kesi unafungua kwa jina hilohilo la
kampuni. Kwa mfano jina la kampuni ni
KEISO LTD. Unapofungua kesi unasema namfungulia kesi KEISO LTD na si
vinginevyo. Kama wewe unaitwa Juma kesi itaitwa
JUMA dhidi ya KEISO LTD, hili ndo
litakuwa jina la kesi na nyaraka zote zitaandikwa
hivyo mpaka kesi inaisha.
\
Kimsingi malalamiko
na migogoro itokanayo na ajira au kazi kwa
ngazi ya Wilaya kisheria hufunguliwa kwenye Tume ya usuluhishi na uamuzi( Commission
for mediation, arbitration) na mahakama kuu ya kazi kulingana na uzito wa mgogoro.
Ukifika makao makuu yoyote ya Wilaya au mkoa uliza ofisi hizi zilipo hazikosi utapewa fomu maalum na utaelekezwa
vizuri tu namna ya kuijaza na lipi la kufanya.
Fomu hizi ni bure na kwa kuijaza utakuwa tayari umefungua kesi. Usiogope kuchukua
hatua ofisi hizi zimerahisishwa sana
utapata maelekezo mazuri sana palepale na utasaidiwa sana.
3. KWANINI
ISHITAKIWE KAMPUNI NA SI MMILIKI.
Kanuni
hii ya kushtakiwa kampuni na kuwaacha wamiliki ilianza kutumika duniani mwaka
1897 na ilianzishwa na mahakama ya
Uingereza katika kesi ya Salomon v Salomon (1897) ,AC 22. Katika kesi hii Mlalamikiwa Salomon alikuwa mmiliki wa
kampuni ambayo wanahisa wake
walikuwa ni yeye, mke wake,mtoto wake wa
kike mmoja na wa kiume wanne.
Salomon
ndiye aliyekuwa Mkurugenzi wa kampuni na hivyo alikuwa akikopa sehemu
mbalimbali ili kuiendesha kampuni hiyo. Muda
fulani kampuni ilishindwa kuendelea
na ikawa inafilisika ambapo walitakiwa
kulipa madeni. Waliweza kulipa baadhi na baadhi wakashindwa hali iliyopelekea
wadeni kumpeleka Salomon mahakamani.
Katika hukumu yake Jaji Macnaghten alisema kuwa waliokuwa wakimkopesha
Salomon hawakuwa wakimkopesha mwenyewe
kwakuwa alikuwa akitumia jina la kampuni.
Kwa hivyo hawana haki ya
kumdai Salomon chochote kwakuwa hakuwa
wakala wa kampuni isipokuwa mtumishi tu
na mtumishi si wakala. Ikasenmwa kuwa kampuni ni kitu kingine na wamiliki ni
kitu kingine deni la mmiliki haliwezi kulipwa na kampuni na deni la kampuni
haliwezi kulipwa na mmiliki kwakuwa kila kimoja kinajitegemea. Ikaonekana Salomon
hadaiwi chochote na akashinda kesi.
Kuanzia
hapo kanuni hii ikaenea dunia nzima na kuingizwa katika sheria za nchi mbalimbali
ikiwemo Tanzania mpaka leo. Pamoja na hayo
kanuni hii iliendelezwa na kuwekewa masharti kadhaa ambapo unaweza kuiweka kampuni pembeni
hata kama kampuni ndiyo iliyohusika na
kuwashtaki wamiliki.
4. KUSHTAKIWA WAMILIKI BADALA YA KAMPUNI
Yamewekwa
mazingira ya kuwashtaki wamiliki wa kampuni hata kama kosa limetendwa na kampuni kwa ajili ya usalama na
kuepuka utapeli wa baadhi ya watu kuunda
makampuni na kuyatumia kufanya uhalifu ili kukwepa kushtakiwa wao kama wao.Mazingira
hayo ni kama kampuni itaundwa kwa malengo ya kitaalam ya kukwepa kodi, kama
kampuni itajihusisha na udanganyifu, mikataba ya wizi kama wanavyofanyiwa
wazungu hapa Dar es salaam na watu
wanaoitwa mapedeshee, kama kampuni itakuwa ikifanya kazi za ujasusi kwa ajili
ya nchi nyingine basi wamiliki watakamatwa na watashtakiwa wao kama wao na si kampuni
tena.
Basi
tuondoe woga tuyashitaki makampuni
korofi ili kupunguza matendo ya unyanyasaji.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA
NA MSHAURI WA
SHERIA KUPITIA GAZETI
LA SERIKALI LA
HABARI LEO KILA
JUMANNE , GAZETI JAMHURI
KILA JUMANNE NA
GAZETI NIPASHE KILA
JUMATANO. 0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.comTANGAZO MUHIMU
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
KUONA BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
VIWANJA NA NYUMBA ZINAUZWA.
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0783851726.
Msaada mkuu
Pindi nilipoingia mkataba Na mwajiri wangu mkataba ulieleza kua nitalipwa night allowance lakini tangu nilipo anza kazi sikuwahi kupata night allowance.hivyo baada ya mwaka mmoja niliandika barua nikimuomba mwajiri arejee terms za mkataba lakini barua haikujibiwa miaka mingine mitatu mfululizo nilimwandia tena lakini hakujibu.sasa mwezi wa saba mwaka Jana ikiwa nimetimiza miaka mitano niliandika barua nyingine lakini hii alijibu akadai ya kwamba sharia imebadilika kutokana Na kazi unayofanya
(doctor) sheria hairuhusu wewe kupata night allowance. lakini kumbuka hakushauriana Na mimi Na wala hakunipa notice yoyote juu ya mabadiliko hayo Na isitoshe mkataba ni ulele nilio anza anao kazi kwa maana hiyo pasipo Ku update mkataba INA maana amekubali terms Na conditions ziendelee .je kwa hili naweza kumshtaki msaada tafadhali
Komaaa
Komaaa