USINYANYASWE NDUGU


USINYANYASWE WE NDUGU FANYA HAYA UWAPO MIKONONI MWA POLISIIMEANDALIWA  NA  MAWAKILI WETU

( 1 )Askari  akikuweka   chini ya ulinzi  muulize  kitambulisho  ni  haki yako.

( 2 )Askari akikukamata akuoneshe  kitambulisho chenye muhuri wa mahakama  kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.

( 3 )Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata  na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.

( 4 )Unaruhusiwa  na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa  sababu  ya  kukamatwa.

( 5 ) Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa  mhalifu  ni haki  yako kujikinga naye.

( 6 )Askari haruhusiwi  kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri  halali.

( 7 )Askari haruhusiwi kuondoka  na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa  halisi.

( 8 ) Askari  haruhusiwi  kupekua nyumba ya mtu bila kibali  cha kupekua.
( 9 )Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.

( 10 )Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.

( 11 )Hairuhusiwi  kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.

( 12 )Ni  haki yako kumpekua askari kabla  hajakupekua ili asipandikize kitu.

( 13 )Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi  wa mtaa.

( 14 )Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.

( 15 ) Mali iliyochukuliwa  katika upekuzi lazima ibaki salama.

( 16 )Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.

( 17 )Unaruhusiwa  kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.
( 18 )Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.

( 19 ) Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.

( 20 )Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.

( 21 )Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.

( 22 )Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu  uwapo chini ya ulinzi.


HIZI  ZOTE  NI  HAKI  ZAKO, ZILAZIMISHE    USIBEMBELEZE  WALA    USIZIOMBE.

9 comments:

 • Nsolo S. Stephen says:
  17 February 2015 at 19:59

  Mengi kati ya haya mengi hukiukwa na Polisi na Anayekamatwa hunyanyasika.

 • Polo Alawi says:
  25 August 2015 at 12:05

  Kuwe na kipindi cha sheria ktk redio au tv kufundisha raia Kujua haki zao .Most Tanzania Hawajui haki zao 99% hata hawo police Hawajui haki zao wenyewe.
  Police wanapochukuwa training wanatakiwa Kujua sheria hata basic .Hii hitasaidia sana.

 • Polo Alawi says:
  25 August 2015 at 12:29

  Kuwe na kipindi cha sheria ktk redio au tv kufundisha raia Kujua haki zao .Most Tanzania Hawajui haki zao 99% hata hawo police Hawajui haki zao wenyewe.
  Police wanapochukuwa training wanatakiwa Kujua sheria hata basic .Hii hitasaidia sana.

 • C Sato says:
  10 March 2016 at 11:52

  Katika hizi haki zilizoainishwa hapa ile ya kumi na moja inasema kuwa:Hairuhusiwi kupekuliwa kuanzia saa moja jioni mpaka saa kumi na mbili asubuhi.Je sheria iko je ktk kukamatwa?

 • C Sato says:
  10 March 2016 at 12:03

  Katika hizi haki zilizoainishwa hapa ile ya kumi na moja inasema:Hairuhusiwi kupekuliwa kuanzia saa moja jioni mpaka saa kumi na mbili asubuhi.Je katika kukamatwa haki inasema je?

 • gulyasilyasi says:
  12 April 2016 at 21:18

  sheria hizi hukiukiwa ukishafika kaunta ya polisi....nashauri cctv kamera zifungwe kila kituo

 • beckaramso.blogspot.com says:
  2 July 2017 at 02:22

  Tunashukuru kwa kutufungua juu ya hizi haki zetu!!!!

 • Amani Jolam says:
  8 March 2018 at 12:11

  wendi tunaburuzwa kwa kukosa kujua sheria

 • Amani Jolam says:
  8 March 2018 at 12:11

  wendi tunaburuzwa kwa kukosa kujua sheria

Post a Comment