USIHOFU NDUGU


USIHOFU NDUGU JITETEE HIVI UWAPO MAHAKAMANI
IMEANDALIWA  NA  MAWAKILI WETU


( 1 ) Kama  unahojiwa na  Wakili mahakamani  usijibu  bila kutafakari alichokuuliza.

( 2 ) Wakili  asikuogopeshe kwa ukali  anapokuuliza  kwani  ukali hulenga kuleta paniki na kukusahaulisha  ulichopanga kusema.

( 3 ) Usilazimishe  kujibu kitu ambacho hukijui ni bora kusema  sijui kuliko kulazimisha kujibu.

( 4 ) Penda sana kujiamini  kwakuwa kujiamini  hupunguza  uwezo wa  Yule anayekuuliza, hata awe Jaji/Hakimu.

( 5 ) Jitahidi  kupata ushauri  wa wanaojua  sheria  kwa  kila hatua unayopiga  katika  kesi.

( 6 )Kama we  ni  shahidi hakikisha unajadiliana  vya kutosha  na Yule unayemtolea ushahidi  kabla  hamjaingia mahakamani.

( 7 )Usipaniki kiasi cha kutoa neno  lolote la kashfa ,kejeli, au  tusi mahakamani unaweza kuongeza kosa  la  kuidharau mahakama.

( 8 )Katika kesi ya jinai usikubali kosa haraka kabla hujajua kitaalam kosa  hilo linaundwa na nini(vipengele vya kosa).

( 9 )Kama  hukuelewa  vizuri  kosa  ulilosomewa  ni bora kukaa kimya, kwakuwa ukikaa  kimya unaandikiwa umekataa kosa.

( 10 )Kanuni  ya  sheria ni kuwa, Ni kazi ya  aliyekushitaki kuthibitisha kwa ushahidi kuwa umetenda kosa  na si kazi yako kuthibitisha kuwa  haujatenda  kosa.

( 11 )Katika kesi ya jinai msikilize kwa makini anayekushitaki na hakikisha unapata  lolote lenye kutia shaka katika maelezo yake na iambie mahakama shaka hilo hii ni kwasababu  huwezi kuwa na hatia kama kuna shaka katika maelezo.

(12)Kama ulitenda kosa katika harakati za kujitetea usidhuriwe iambie mahakama kuwa ulitenda kosa ukijilinda(self defence) inaruhusiwa, hata kama uliua waweza kuachiwa.

( 13 )Kama ndugu yako hana akili tinmamu na ametenda kosa iambie mahakama.Hii ni kwasababu  kutokuwa na utimamu wa akili ni kinga inabidi aachiwe lakini hatarudi nyumbani atapelekwa vituo vya wasio na akili.

( 14 )Inakubalika  na ukaachiwa huru  ukisema kuwa ulilazimishwa kutenda kosa kama kweli ulilazimishwa.

( 15 ) )Inakubalika  na ukaachiwa huru  kusema kuwa sikuwa eneo la tukio wakati likitokea kama kweli haukuwapo.

( 16 )Kama kosa ni kupita taa nyekundu ikiwaka barabarani,swali lako kwa  shahidi  traffic lilenge  kumbana kama sehemu aliyokuwa amesimama alikuwa na uwezo wa kuangalia vizuri na kutambua rangi  za taa. Mfn. jua kali linawaka yeye ameuonaje mwanga wa taa kutoka mbali.

 ( 17 )Ukipewa nafasi ya kumhoji shahidi muhoji maswali mafupi. Mfn. ulikaa upande wa pili barabara, si ndio, jua kali lilikuwa linawaka , si ndio, ulifanya kazi ya kuangalia magari mengine pia si ndio, na mbele kulikuwa na miti si ndio, sasa kama hali ilikuwa hivyo uliwezaje kuona taa nyekundu ikiwaka wakati nakatiza.

18 )Ukipewa nafasi ya kumhoji shahidi wako uliyemleta katu usimuulize swali ambalo mlikuwa hamjalijadili na hivyo hujui atatoa jibu gani.

( 19 ) Kama wanaokushtaki wanashahidi na unamjua  kuwa kuna kipindi aliwahi kuchangnyikiwa au kufanya tukio lolote la uhalifu kabla,  ni nafasi nzuri kuhoji uwezo na uadilifu wake mpaka aaminike  kwa anayoyatolea ushahidi leo.

.........ITAENDELEA

5 comments:

Post a Comment