NA BASHIR YAKUB -
Kuna matatizo sana
kati ya wapangaji
na wenye nyumba
kuhusu notisi ya
kuondoka au kuondolewa. Wako
wanaosema notisi ni
mwezi mmoja, wako wanaosema
ni miezi mitatu
n.k. Kama ni kweli
ama hapana tutaona hapa
sheria inasemaje.
Masuala ya pango
yanaongozwa na sheria
kuu mbili. Moja
sheria ya ardhi
namba 4 ya mwaka 1999
na pili sheria
ya mikataba sura
ya 345. Kwa
pamoja sheria hizi
mbili husimamia jambo
hili.
1.MIKATABA YA PANGO.
Mikataba ya pango inahusisha makubaliano
ya upangaji kati
ya mwenye nyumba
na mpangaji au
mpangaji na mpangaji
mwingine wa pili.
Pango laweza kuwa la nyumba ya
kuishi, kwa ajili ya
biashara, nyumba ya
ibada au shughuli
nyinginezo. Yote
haya yataingia katika
maana ya pango.
2. AINA ZA MIKATABA YA PANGO.
Sheria ya ardhi vifungu
vya 78 na
79 inatambua mikataba ya
upangaji ya muda
mrefu na vipindi
vifupi. Inatambua pango la
wiki, mwezi, miezi,
mwaka na miaka.
Imetoa uhuru kwa
wahusika wenyewe kuamua
ni muda gani
wangependa kuingia mkataba.
3. NOTISI
YA KUONDOKA.
Katika vitu muhimu
sana katika suala
la pango ni
notisi ya kuondoka au kuondolewa
katika pango. Jambo
la kuzingatia awali kabisa ni
kuwa notisi hii
ni muhimu pande
zote mbili. Upande
wa mwenye nyumba
na upande wa
mpangaji. Kila mmoja
kwa nafasi yake
anawajibika kutoa notisi
kwa mwenzake panapo
mahitaji ya kuondoka
au kuondolewa.
Ikumbukwe notisi si kwa ajili
tu ya kuondoka na kuondolewa bali
pia hutakiwa yanapotokea mabadiliko yoyote
katika masharti ya
mkataba. Hii ina maana
hata kuongeza kodi, kupanga
kukagua nyumba, kufanya marekebisho
n.k. notisi yafaa
itolewe.
4. NOTISI
NI YA MUDA GANI.
Sheria haikutamka moja
kwa moja notisi
ya kuondoka au kuondolewa iwe
ya muda gani. Kinachohitajika na cha
lazima ni kuhakikisha notisi inatolewa
lakini
pia inatolewa katika muda
unaokadirika na kuingia akilini( reasonable ).
Kwahiyo
notisi inaweza kuwa
muda wowote isipokuwa muda huo
uwe unaokadirika na
kuingia akilini.
Ili tujue
muda unaokadirika yafaa tuangalie muda
wa pango ulio
katika mkataba. Kwa mfano mtu
mwenye mkataba wa miaka
mitano huwezi kumpa
notisi ya kuondoka ya mwezi
mmoja au hata miwili. Lakini mwenye
mkataba wa miezi minne
au
mitatu unaweza kumpa
notisi hata ya mwezi
mmoja. Mwenye miezi
sita hata miezi
miwili inaweza kuwa
sawa na wa
mwaka miezi mitatu
inaweza kuwa sawa.
Jambo moja nisisitize sana
hapa. Kwakuwa sheria haijataja
wazi muda wa notisi
ya kuondoka ni vema
sana tena sana kuhakikisha
mkataba wenu wa
pango unaeleza muda wa notisi. Ni
muhimu sana. Mkataba
ueleze wazi kabisa
notisi itakuwa
ni ya muda
gani ikiwa mwenye
nyumba anataka nyumba
yake na ikiwa
mpangaji anahitaji kuondoka. Na katika kukubaliana, muda
wowote mtakaokubaliana unatosha
na unakubalika kisheria
kwasababu umetokana na hiari
ya mkataba.
Usikubali kusainishwa
mkataba ambao hauelezi
muda wa notisi . Hili litakuondolea masahibu
baadae.
Hapo juu tumesema
huwezi kumuondoa mpangaji
kwenye nyumba bila kumpa
notisi. Hili ni
muhimu kulirudia. Notisi
ni lazima isipokuwa
muda wa notisi
ndio utatofautiana.
5. KUMUONDOA
MPANGAJI KABLA YA
MUDA WA MKATABA KUISHA.
Hili nalo ni
kosa na ikitokea
basi mwenye nyumba
lazima alipe fidia.
Hili ni kosa
la kuvunja mkataba
kama ilivyo kuvunja
mikataba katika mikataba
mingine yoyote.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
kipengele cha tano, kipitie vzur kwenye sheria na regulations zake zote, pia hata suala la notisi pitia regulation zake pia,
Na mpangaj anapovunja mkataba inapaswa adai pesa yake ya miez/ miaka iliobaki?
Naomba kujua veep kama mpangaji kamaliza mkataba na hakutoa taarifa za kuendelea mkataba.na mwenye nyumba anataka nyumba ake na hakumpa taarifa zakumpokonyaa nyumbaa. Sheria inasemaje
Vipi kw mpangaji mwenye deni na hana mkataba
Naomba kuuliza, Mimi ni mpangaji ila kuna mvutano kwa wasimamizi wa mirathi, shauri lao linaendelea mahakamani, msimamizi A, ambaye tumelipa kodi ya mwaka, inasadikiwa ameshindwa mahakamani, inabidi msumamizi B, anasimamia mirathi, swali: je mkataba wangu mpaka uishe ndipo mkataba mpya niingie na msimamizi B au msimamizi B anahaki ya kunitowa kwenye nyumba bila kurudishiwa kodi iliyobaki ?
Ukarabati wa nyumba, utengenezaji wa miundombinu mibovu ya maji na ile ya umeme iliyochakaa ni kazi ya nani kati ya mpangaji na mwenye nyumba? Asante
Vipi kuhusu kuvunja mkataba lakini siyo kwa ghafla unakua umempa muda mpangaji je anatakiwa kulipwa fidia!
Mbali na ile pesa atakayorudishiwa yamieziiliyobakia!
Kama mpangaji hana mkataba na makubiano mda wake umeisha sheria inasemaje.
Inakuaje kama, mkataba umeisha, makubaliano ya mwenye nyumba na mpangaji ikawa ni kulipia kwa mwezi mmoja mmoja, japo mwenye nyumba hajakukabidhi mkataba katika katika nakala ya karatasi(hard copy), na baada ya kipindi kifupi(miezi miwili), akataka kukufukuza katika nyumba yake??
Je mm ni mpangaji na nimemcheleweshea mwenye nyumba kumpa kodi mwez moja na amekuja kazn kushitaki na kazn wanataka kunichukulia hatua je ni haki kisheria kuwa ofcn kwangu Wana mamlaka ya kunichukulia hatua dhid ya mm na mwenye nyumba wangu
Napenda kujua sheria inasemaje kuhusu mpangaji alikaa eneo kwamda wa miaka 8.bira kuvunja masharti ya mkataba kodi analipa kwa mwaka mmoja analipa kwawakati.mwanzo wa mwaka. namkataba unasema siku mpangaji akitaka kuhama atoe talifa kabla ya miezi 3) na alipie kama tulivyo kubalia pande zote mbili.nampangaji akitaka kuendelea andike barua yakujurisha.kama anaendelea hapo akusema najulisha kwa wakatigani. hilipo fika 28/12/2017 nikamjulisha kua naendelea kutumia eneo. th.30/12/2017 nikapewa notice ya masaa24. niondoke katika eneo hilo. maelezo yaliyoko kwenye notice inasema tumeamua kutopangisha tena.naomba ushauli nifanyeje hili niweze kupata haki zangu?
Naomba kujua iwapo mi nimepanga khalafu baada ya mwezi 1 mwenye nyumba anakuja kuniambia kwamba chumba ishachukuliwa kwaiyo natakiwa nitoke hapo natakiwa nifanyeje
Mm kaniambia baada ya Kodi kuisha nirudishe chumba inakuaje hapo Kama nitakua cjapata chumba
Namkataba hajanipatia hii miezi sita amefanya kuandika kwenye kikaratasi nakumpa mtoto
Sheria iko vipi kwenye mapangishano ya nyumba ya kuishi ambayo hayana mkata wa kwamba mpangaji atakaa mda gani Bali makubaliano yaliyopo n kwenye Kodi tu. Na badae mpangaji akakaa kwenye nyumba takriban mda wa mwaka mzima bila kulipa kwasababu tu mwenye nyumba Yuko mbali nae, ili kusudi ssa mweny nyumba apate haki ya kodi yake anatakiwa afuate vitu gan pp
non sense hawana mamlaka hata kidogo