NA BASHIR YAKUB -
Nilipoandika kuhusu namna
ya kuunda kampuni nilieleza
pia kuwa unapokuwa
umekamilisha usajili wa
kampuni na umepata
cheti cha usajili
yapo mambo mengine
ya kufanya kabla
ya kuanza rasmi
biashara. Moja ya mambo
hayo nilisema ukishapata cheti unatakiwa uende
manispaa husika ukapate
leseni ya biashara. Manispaa husika ni
manispaa ambako ofisi
ya kampuni yako
itakuwa. Kitu kingine
baada ya kupata cheti
cha usajili ni kupata
namba ya mlipa
kodi (TIN). Ili kampuni ifanye
biashara kisheria inatakiwa
kuwa imepata namba hii.
Yawezekana
wanahisa kila mmoja
anayo namba yake ya
mlipa kodi lakini
namba hizo haziwezi kutumika kwakuwa
ni za watu
binafsi na si
za kampuni. Kampuni
inatakiwa ipate namba yake
inayojitegemea.
Halikadhalika kwa
wanaoanzisha vikundi kwa mfano
saccos, na asasi za kiraia( NGOs) nao wanatakiwa kuwa
na namba ya mlipa
kodi ya
vikundi hivyo.
1.TIN NAMBA
HUPATIKANA WAPI.
Mamlaka ya mapato
Tanzania ( TRA) ndiyo
mamlaka inayoshughulika na
utoaji wa namba
za mlipa kodi. Awali
namba hizi zilikuwa
zikitolewa makao makuu
ya mamlaka ya
mapato ambapo kwasasa katika
kuboresha huduma wameweka
ofisi za kikanda
sehemu mbalimbali ambazo
huhudumia wahitaji wa
kanda husika kwa
mfano kwa Dar es
salaam
eneo la ilala , buguruni, tabata, kariakoo ofisi
zipo makutano ya Shaurimoyo
badala ya mnazi
mmoja au samora . Hata
hivyo yapo maeneo
mengine ambayo ofisi
za kanda hazijawekwa
kwa mfano mikoani
ambapo wahitaji hulazimika
kufuata huduma hii
makao makuu ya
mamlaka ya mapato.
2. KUPATA
TIN NAMBA YA KAMPUNI.
Ili kupata TIN namba
ya kampuni unahitaji
kwenda na viambatanisho
vifuatavyo.
( a ) Picha mbili
za passportsize kwa
kila mkurugenzi. Wakurugenzi wawe
wawili, watatu au mmoja kila
mmoja atatakiwa kuwasilisha
picha zake mbili.
( b ) Nakala moja
ya kitambulisho kwa kila
mkurugenzi. Hapa
kitambulisho kinaweza kuwa
cha taifa, cha mpiga kura, cheti
cha kuzaliwa, hati ya kusafiria au
leseni ya kuendeshea.
( c ) Nakala moja
ya katiba na
waraka kampuni( memorandum &
article of association). Hii ina
lengo la kuonesha aina ya biashara ambazo
kampuni itakuwa inazifanya.
( d ) Nakala moja
ya cheti cha
kuzaliwa kwa kampuni( certificate of
incorporation). Hii ni
kuthibitisha kuwa kampuni inayoomba
namba ya mlipa
kodi imesajiliwa kisheria.
( e ) Mkataba wa
pango wa eneo
ambalo biashara itakuwa
ikifanyika. Kama ni
nyumba yako basi
utawasilisha nyaraka ya
umiliki wa nyumba
iyo.
( f ) Barua iliyojazwa
na mwenyekiti wa serikali za
mitaa wa eneo ambalo
biashara itafanyika. Barua
hii hutolewa na
mamlaka ya mapato
TRA na hujazwa
na mwenyekiti wa serikali za
mitaa. Kwahiyo barua
hii utaifuata TRA
na kuipeleka seriklali za
mitaa ili ikajazwe
na kugongwa mhuri.
Mwisho unapokuwa
umekamilisha viambata hivi
utaenda TRA ambako
utakuta fomu maalum utazotakiwa kujaza. Katika fomu
hizo kuna sehemu
wakurugenzi wa kampuni watasaini
pamoja na mwenye
nyumba wako aliyekupangisha ofisi
kama umepanga. Baada
ya hapo utafanyiwa
usaili( interview) kwa ajili ya
kupata namba ya
mlipa kodi (TIN ).
3. KUPATA TIN NAMBA
YA NGOs, VIKUNDI/SACCOS.
Vifuatavyo ni viambatanisho
vinavyotakiwa.
( a ) Nakala moja
ya cheti cha usajili
wa kikundi kutoka
RITA. Mamlaka ya
RITA ndiyo hushughulika na usajili
wa vikundi na hivyo cheti
chao hutakiwa kuambatanishwa ili kuthibitisha
usajili.
( b ) Nakala moja
ya Katiba ya
kikundi na muhtasari
wa kikao cha
mwisho.
( c ) Picha mbili
za passportsize za katibu, mweka
hazina na mwenyekiti. Kila mmoja
mbili mbili.
( d ) Nakala moja
ya mkataba wa pango iwapo
ofisi za kikundi
zimepangwa au hati, leseni
ya makazi, ofa iwapo
ofisi sio za
kupanga.
( e ) Nakala moja
ya kitambulisho kwa kila
mbia(partner). Hapa
kitambulisho kinaweza kuwa
cha taifa, cha mpiga kura, cheti
cha kuzaliwa, hati ya kusafiria au
leseni ya kuendeshea.
( f ) Barua iliyojazwa
na mwenyekiti wa serikali za
mitaa wa eneo ambalo
biashara itafanyika. Barua
hii hutolewa na
mamlaka ya mapato TRA
na hujazwa na mwenyekiti. Kwahiyo
barua hii utaifuata
TRA na kuipeleka serikali za
mitaa ili ikajazwe
na kugongwa mhuri.
Hapa pia baada
ya kukamilisha viambata
vyote zitajazwa fomu
maalum zilizopo mamlaka
ya mapato na utafanyika
usaili mfupi kwa
wahusika na TIN namba itapatikana.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment