NA BASHIR YAKUB-
Wapo
watu ambao shida yao ni kuandaa wosia
lakini tatizo ni waanzeje.
Je waandike kama barua, je waandike
kama makala, je waandike kama maombi ya zabuni, je waandike kama notisi, waandikeje hasa. Wapo watu ambao
wameshaandika wosia lakini wameandika hovyohovyo tu bila mpangilio maalum.
Ikumbukwe kuwa wosia mbovu usio katika taratibu na mpangilio wa kisheria ni
wosia ambao baada ya kufa kwako unaweza kuleta ugomvi mkubwa na hatimaye
inaweza kuamuliwa kuwa wosia huo si halali hata kama ni kweli uliuandika na hivyo kusababisha yale yote uliyotaka
yafanyike baada ya kufa kwako yasifanyike. Aidha hili ni tatizo ambalo makala
haya yaweza kusaidia kulimaliza kwa atakayesoma. Mfano huu au sample hii hapa chini ni ya kitaalam na ya
kisheria hivyo mtu anaweza kuinakili hivihivi ilivyo na akaitumia
kuandalia wosia wake.
MFANO/SAMPO YA
WOSIA
- Huu
ni wosia wangu wa mwisho mimi ………………………………wa S.L.P…………………………………
- Namchagua
………………………………………………………………………….
wa S.L.P. ……………………………………………………………………………….
Simu………………………………………………………………………………………
ambaye anaishi
…………………………………….kuwa msimamizi wa mirathi yangu.
- Nitakapokufa
mwili wangu ukazikwe……………………………………………..
Wilaya
……………………………………Mkoa……………………………………...
- Mali zangu ni:
(a)………………………………………………………………………………………
( b ) ……………………………………………………………………………………
( c )……………………………………………………………………………………..
( d ) Nina akaunti zifuatazo:…………………………………………………………
………………………………………………………………………………………….
5. Natamka
kwamba mali zangu zote zinazohamishika
na zisizohamishika zitamilikiwa na mke/mume
wangu aitwaye..................……………iwapo
atakuwa hai baada ya
kufa kwangu.
6. Iwapo mke/ mume wangu aitwaye
……………………………………..atafariki mapema kuliko mimi
, mali zangu zitarithiwa na watoto wangu wafuatao:-
(a)………………………………………………………………………………………….
S.L.P………………………………………………………………………………………
Simu…………………………………………………………………………………………
(b)……………………………………………………………………………………………
S.L.P…………………………………………………………………………………………
Simu………………………………………………………………………………………..
(c)………………………………………………………………………………………….
S.L.P…………………………………………………………………………………………
Simu………………………………………………………………………………………..
(d)……………………………………………………………………………………………
S.L.P………………………………………………………………………………………….
Simu
………………………………………………………………………………………….
Katika mafungu yaliyo sawasawa ( kama
si katika mafungu sawa utaainisha mbele
ya kila jina la mtoto/mrithi kile ulichompa ) .
Imetiwa saini
hapa……………………………………………….….......………………….
Siku
ya………..………………………………………………………….........………………
Mwezi
wa………….…………………mwaka……………………….........………………
Saini
ya mwosia…………….…………………………………………..........……………
Shahidi
wa Kwanza:
Jina:……………………….......…………………………………………………………….....…….
Saini:……………………………………………...................………………………………………
Anuani:………………………………………………………………………………………………
Kazi…………………………………………………………………………………………………..
Shahidi
wa Pili :
Jina:………………………………………………………………………………………………….
Saini:…………………………………………………………………………………………………
Anuani:………………………………………………………………………………………………
Kazi…………………………………………………………………………………………………..
Mbele ya ……………………………………………………………………………......………….
…………………………………………………………………………………………….........…….
WAKILI
Mshuhudi viapo/Saini:…………………………………………………………………................
ANGALIZO: “ Kuandika wosia si uchuro bali ni
kujizatiti katika kuhakikisha
mambo yako yanakuwa kama unavyotaka hata usipokuwepo , ukiwa ni mmojawopo wa wanajamii chukua
hatua
ya kuandika wosia na uwashawishi wengine kufanya hivyo”.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI LA
HABARI LEO KILA
JUMANNE , GAZETI JAMHURI KILA JUMANNE , NA GAZETI
NIPASHE KILA JUMATANO. PIA NI KATI YA WANASHERIA WAANZILISHI WA BLOG HII 0784482959, 0714047241
bashiryakub@ymail.com
Makala nzuri..haswa uandishi wa wosia..km sipendi mke arithi je?
Mke ana haki ya kurithi kisheria has a kwa Mali ulizopata ukiwa pamoja naye,ila kama hukutafuta neye wataalamu was sheria watakujuza zaidi
My learned brother
good job stay blessed
Je,kama mume wangu alinikuta na mali ambazo nilichuma mwenyewe kabla ya kuolewa,mfano nyumba na viwanjaanahaki gani kwenye hilo?
Na kama sitaki mume wangu arithi mali zangu ,Je ni sawa au sio sawa?
Asante kwa mwongozo
Asante kwa elimu nzuri ya kutufahamisha mambo muhimu.
Wosia ni mzuri sana na nivema kuandika mapema ili kuepuka ugomvi
Asante Sana kwa makala haya Mimi naanza kuandika leo japo sijao
🙏
Mara nying wanawake wanajua wanaume ndo wanatangulia kufa sheria inasemaje mwanamke aktanglie kufa
Ni changamoto sana kuona kuwa wannaume watakufa mapema. Kikubwa kujiandaa kwa kuweka wosiaa vizuri.
Hawa mashaidi kwenye wosia ni kina nani na je msimamizi wa wosia anatakiwa kujuanwakati wa uandishi wa wosia? Jr baada ya uanfishi wosia unahifadhiwa na nani na wapi?