NA BASHIR YAKUB -
Mara nyingi nimeandika
kuhusu ardhi hususan viwanja
na nyumba. Katika
kufanya hivyo mara
kadhaa nimejaribu kuwatahadharisha watu namna
mbalimbali ya kisheria ya kuepuka kuingia
katika migogoro ya
viwanja na nyumba
hasa wakati wa kununua(
wanunuzi). Nimewahi kueleza
namna au vitu
vya msingi ambavyo hutakiwa
kuwa katika mkataba
wa ununuzi
wa nyumba au
kiwanja. Nikaeleza umuhimu wa
kila kimoja na nikasisitiza kuwa atayekuwa
amenunua ardhi na mkataba
wake ukajaaliwa kuwa
na vitu hivyo
basi si tu
atakuwa amefanya manunuzi
bora lakini pia atakuwa amefanya manunuzi yanayokubalika kisheria.
Ifike hatua watu waelewe kuwa migogoro
mingi ya ardhi
huanzia na kutokuwa makini kwenye manunuzi. Kutokupata ushauri
wa kisheria ikiwa
ni pamoja na kutopitia hatua za msingi
za kisheria kabla ya
manunuzi, kuandikiwa mikataba ya
manunuzi isiyokidhi vigezo
vya kisheria ikiwemo
ile ya serikali
za mitaa ambayo
hairuhusiwi kabisa kisheria ni
kati ya sababu chache kati
ya nyingi zitakazokupelekea uingie
katika mgogoro. Leo
nitaeleza hatua moja ya msingi
sana ambayo hutakiwi ufanye manunuzi
ya ardhi bila
kuipitia.
1.HATUA
TANO ZA KUFUATA
UNUNUAPO NYUMBA/KIWANJA.
Ziko hatua tano
muhimu za kupitia pale
unapo kuwa katika mchakato
wa kununua ardhi. Umuhimu wa
hatua hizi ni
kuwa kwanza kabisa
si rahisi kujikuta
katika mgogoro unapokuwa
umezipitia. Lakini pili
hata bahati mbaya
utokee mgogoro basi
wewe uliyepitia hatua
hizo utakuwa salama
na kama ni
kesi basi wewe
upo katika mazingira
mazuri ya kushinda. Hatua
ya kwanza huitwa
hatua kabla ya
mkataba( pre contractual
stage).
Hatua hii inayo mambo
yake ya msingi
na ya kisheria
ambayo kuyafuata kwako
kwaweza kukuweka mbali
na hatari ya kununua
ardhi yenye mgogoro
au itayokuingiza katika
mgogoro . Hatua hii
ndiyo nitakayoeleza kama msingi
wa makala ya
leo kama tutakavyoona.
Kabla ya kueleza
hatua hiyo ni
vema pia nikazitaja
hatua nyingine japo
kwa ufupi. Hatua ya pili
huitwa hatua ya mkataba( contractual stage). Hii
ni hatua ya
kupitia na kujiridhisha
na mkataba wa
manunuzi ikiwa ni
pamoja na kuusaini. Hatua ya
tatu huitwa “pre completion stage”,
hatua ya nne huitwa
hatua ya kumalizia ( completion stage) na hatua ya tano na ya mwisho
huitwa hatua baada
ya kumalizia ( post completion
stage).
2. USINUNUE
NYUMBA/KIWANJA BILA KUPITIA
HATUA HII.
Kama nilivyoeleza hapo
juu hatua nitakayojadili hapa
huitwa hatua kabla
ya mkataba au “pre
contractual stage”. Jambo
kubwa ambalo huhusishwa
katika hatua hii
ni kufanya utafiti
wa kitaalam uitwao “official search” . Katika hatua
hii mlengwa anayetaka
kununua ardhi kupitia ofisi
ya mwanasheria ataandika
barua kwenda kwa msajili wa
ardhi kumuuliza taarifa
kamili za nyumba
au kiwanja anachotaka
kununua. Msajili wa ardhi atapekua katika
kumbukumbu zake rasmi
na kutoa majibu
sawa na kile
kilicho katika kumbukumbu
zake.
3. MAMBO
MUHIMU UTAKAYOULIZA KWENYE BARUA
YA MSAJILI.
Kwanza katika barua
yako utahitaji kujua
jina la mmiliki linalosomeka katika
nyaraka za serikali. Hii
itakusaidia kulinganisha jina
la anayekuuzia na
lile linasomeka katika
kumbukumbu za serikali. Kwa
kujua jina tu utaepuka kununua ardhi kutoka kwa mtu ambaye
si mmiliki halisi. Pili
utahitaji kujua iwapo
ardhi hiyo imewekwa
kama dhamana popote
katika taasisi za
fedha. Kama imewekwa dhamana
basi taarifa zitaonesha. Hii ni
kwasababu taasisi za
fedha hutuma taarifa
kwa msajili wa ardhi katika
kila ardhi inayowekwa
kwao kama dhamana.
Tatizo la kununua
ardhi iliyowekwa dhamana
bila kujua ni
aidha ukubali kuingia
hasara kulipa deni
ili nyumba ubaki
nayo au uwe
mpole nyumba uliyonunua
iuzwe upate hasara. Tatu
utaweza kujua iwapo
ardhi hiyo ni
ya wanandoa hasa
iwapo wanandoa hao wana mgogoro.
Hii ni
kwasababu sheria humpa
haki mwanandoa kuweka zuio
katika ardhi ya familia iwapo
mmoja wao ana wasiwasi mwenzake anaweza
kuuza ardhi hiyo. Kwahiyo
ikiwa taarifa kama
hizo tayari zimepelekwa
ardhi basi utakapopitia
hatua hii kabla
ya kununua utaoneshwa
taarifa hizo na hivyo
kuepuka kununua mali ya
familia kitu ambacho
ni kama kupoteza. Nisisitize kuwa hatua hii ni
muhimu sana kwakuwa ni
hatua pekee ya
kujiridhisha na uhalali wa
ardhi unayotaka kununua. Nathubutu kusema
kuwa usinunue kiwanja/nyumba bila
kupitia hatua hii.
MWANDISHI
WA MAKALA HAYA
NI MWANASHERIA NA
MWANDISHI WA MAKALA YA SHERIA
KUPITIA GAZETI LA JAMHURI KILA JUMANNE. 0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
Nakufuatilia sana wakili msomi
Naomba msaada nipate pdf ya mkataba wa kiwanja au nyumba