Wednesday, 27 July 2022

NAMNA YA KUCHUKUA PESA ZILIZOACHWA NA MAREHEMU TIGOPESA, MPESA N.K. KAMA HUNA PASSWORD YAKE.

 





Na  Bashir  Yakub, WAKILI.  -     

Hii itakusaidia kuchukua pesa zilizoachwa na marehemu katika akaunti yake ya simu au hata kutaka kujua kama ameacha chochote kwenye simu ana hapana, hasa kama hujui namba yake ya siri ya akaunti(nywila).

Kuwa na nyaraka zifuatazo halafu nenda ofisi za mtandao husika.

1. Hati ya usimamizi mirathi. Kwa wakristo ni fomu Na. 68 kwa waislam ni Fomu Na. 4. Zinapatikana mahakamani baada ya kukamilisha utaratibu wa mirathi.

2. Cheti cha kifo cha marehem. Kinapatikana ofisi za RITA.

3. Kiapo cha msimamizi wa mirathi. Kinapatikana kwa Wakili yeyote.

4. Wosia kama upo, kama haupo sio lazima.

5. Barua ya utambulisho. Inapatikana serikali za mitaa.

6. Kitambulusho cha msimamizi wa mirathi. Inaweza kuwa NIDA, cha kura, leseni nk.

7. Mukhtasari wa kikao cha familia. Unapatikana baada ya familia kukaa  na kuuandaa.

8. Kitambulisho cha marehemu. Inaweza kuwa NIDA, cha kura ama Leseni.

Kimsingi kitu kikubwa kinachohutajika ni Namba 1. Hata hivyo makampuni ya simu huhitaji na hivyo vingine Namba 2 - 7. 

Hata hivyo isikupe tabu, ukishaweza kuwa na Namba 1 hivyo vingine Namba 2- 7 lazima uwe navyo tu,  kwasababu ili mahakama ikupatie Na.1 lazima uwe umewasilisha 2 - 7 pia.

Kwahiyo ukishapeleka mahitaji hayo mtandao husika utapewa namba ya siri ya marehemu na hivyo kuweza kufanya miamala ama kuangalia kama  kuna akiba n.k.


0 comments:

Post a Comment