NA BASHIR YAKUB -
Mara nyingi wazazi
wanapotengana huwa tunashuhudia
mabishano ya nani
anatakiwa kukaa na
mtoto. Ni mama au baba. Kwa suala
hilihili wapo watu wako
mahakamani na wengine
hawako mahakamani lakini
wako katika ugomvi
mkubwa wa nani
haswa akae na mtoto.
Wapo ambao walikuwa
katika ndoa na
sasa ndoa imevunjika,
wapo ambao walikuwa wakiishi kama
mke na mme
lakini bila ndoa
na sasa mahusiano yao
yamekwisha na wapo
ambao hawakuwahi kufunga
ndoa wala kuishi
kama mke na mme
ila walizaa tu
ila kwasasa wapo katika mgogoro
wa nani akae
na mtoto.
Makala yataeleza namna sheria
inavyozungumza kuhusu umri
wa mama kukaa
na mtoto lakini
kabla ya hilo ni vema
pia kutizama ni
wapi waweza kupeleka malalamiko ya
jambo hili. Sheria ya
Mtoto , namba 21 ya mwaka
2009 ndiyo inayohusika katika
jambo hili.
1.WAPI UKALALAMIKE UKITAKA
KUKAA NA MTOTO.
Zipo sehemu mbili
ambazo waweza kupeleka malakamiko yako
ili uweze kupatiwa
haki ya kukaa
na mtoto. Kwanza
ni ustawi wa jamiii
na pili ni
mahakamani.
Mahakama yoyote ya
mwanzo, wilaya, hakimu
mkazi hata mahakama kuu
unaweza kupeleka mombi haya.
Ila ni vema ukaanza
mahakama ya mwanzo
au wilaya.
Tofauti ya ustawi
wa jamii na mahakamani ni kuwa
mahakama wana amri
wakati ustawi wa jamii
hawana amri( order) .
2. NI
UMRI GANI MTOTO
AKAE NA MAMA.
Kifungu cha 26( 2 )
cha Sheria ya mtoto, namba 21 ya
2009 kinasema kuwa
ni vizuri mtoto
aliye chini ya
umri wa miaka
saba akae na
mama. Hata hivyo
ni vema kufahamu
kuwa kifungu hiki
hakikusema ni lazima( shall) mtoto
wa umri huo akae
na mama.
Kifungu kinasema suala
la mtoto chini
ya umri wa miaka
saba kukaa na
mama ni dhana
inayoweza kutozingatiwa( rebuttable
presumption). Ni dhana inayoweza
kutozingatiwa kwa maana
kuwa zipo sababu
ambazo mtoto chini
ya umri huo inaweza kuamuliwa kukaa
na baba au
mtu mwingine yeyote ambaye
ataonekana kufaa zaidi kuliko
mama.
Kwahiyo lazima tuzingatie kuwa
sio lazima mtoto
chini ya umri wa miaka 7
kukaa na mama.
3. SABABU ZIPI
MTOTO CHINI YA
UMRI WA MIAKA
7 ATAAMULIWA KUKAA
NA BABA.
Kifungu cha 37( 4 ) kinasema
kuwa katika kutoa
amri ya mtoto
akae na nani
mahakama itatakiwa kuzingatia
maslahi mapana ya
mtoto husika( best interest
of the child). Kwahiyo
habari sio kwamba
lazima mtoto akae
na mama au
baba laa hasha,
isipokuwa habari ni maslahi
mapana ya mtoto, wapi
mtoto atapata malezi
bora.
Hii ndiyo
sababu au kigezo
kikuu kinachozingatiwa na mahakama
inapokuwa inaamua. Kwa ufupi
maslahi mapana ya
mtoto ni kama, wapi
kuna mazingira mazuri
kwa mtoto, ni mzazi
yupi anajali kuliko
mwingine, wapi atapata matunzo
bora, wapi hatanyanyaswa, mzazi yupi
ni mlevi, kahaba na
ana tabia mbaya, ikiwa
kuna mzazi ana
matatizo ya akili,
magonjwa ya kuambukiza n.k.
Kwa hiyo kwa
ujumla niseme kuwa mtoto
chini ya umri
wa miaka 7 ni
vizuri kukaa na
mama lakini ikiwa baba
atathibitisha mambo ambayo
hayafai kwa mama
basi anaweza kupewa
mtoto na akaachwa
mama .
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
mke wangu aliiacha ndoa na alitoroka (alikimbia na watoto) anadai haki za watoto ambazo sina shida nazo kwani nilimshauri awaache watoto Kama anataka kuondoka, nilimpa uhuru huo. akakaidi akaondoka nao lakini haitoshi alichukua kila alichoona kinamfaa akaondoka na watoto. Naomba ushauri kwanza nawataka watoto kwa kuwa nafahamu hana uwezo wa kuwapa mahitaji yote muhimu. kwa upande wake anataka matunzo ya watoto na mie Sina shida na hilo kipato changu ni Kama dola 128 yaani Kama laki tatu za kitanzania sheria ikitaka watoto waendelee kukaa na Mama yao nitakuwa na jukumu la kutoa pesa kiasi gani kulea watoto wangu ambao Sina shida nao kwa kweli.
mimi ni mhanga wa tatizo la mzazi mwenzangu( baba ) kutokutoa matumizi ya mtoto nishajaribu kumuita dawati la jinsia pia ustawi wa jamii lakini hakuna mafanikio mwisho nikaambiwa niende mahakamani sasa nikapata na kingugumizi pale ambapo niliambiwa nikifika mahakamani nitapewa wito wa kumpelekea mtuhumiwa kipindi hiko cjui anapoishi wala nduguze ama anapofanyia kazi pia kwenye mawasiliano ya simu kani block ila nikitumia namba ya mwingine kupiga inaita ila haipokelewi naomba ushauli nifanye nini? maana mtoto kwa sasa ana umri wa miaka 7 na hajawah kutoa hata centi tano tokea azaliwe
Asante sana mwanasheria, nmeielewa hii kitu
Habari, mimi niliwahi kuishi na mwanamke miaka 7 na kubahatika kupata watoto 3. Miaka mitatu iliyopita, Mke alinikimbia na kuniachia watoto wote 3 mmoja akiwa na umri wa mwaka 1. Kwa kuwa sikuwa nimefunga naye ndoa yoyote na kwa juhudi nyingi za kumrudisha kutokuzaa matunda nimeamua kudai talaka. Nilipodai talaka, amekana anasema yeye hajaniacha ila mimi ndiye ninataka kumwacha. Je kisheria kwanza niko sawa kumwomba talaka au hana uhalali wa kudai kuwa mke wangu? Pili je, ikiwa nimelea watoto peke yangu miaka mitatu na sasa wako shule wrote, je ana haki ya kuwadai watoto ikiwa tumepeana talaka kwa kigezo cha umri wa watoto?
vipi inapofika miaka saba? sheria inasemaje
Habari za leo. Nashauri , uende ustawi wa jamii katika eneo analokaa na kupeleka suala Hilo huko watakusaidia.
Habari. Suala lako ni zito kwa sababu hukutakiwa kuwa na maamuzi ya haraka kuingia kwenye mahusiano na mtu hujamfahau vizuri, ndugu zake, wazazi, anapoishi, anapotoka n.k hivyo fanya jitihada za kumpata Kwanza ndipo uendelee na shauri.
Suala lako linatakiwa kupelekwa ustawi wa jamii ili wawasikilize kwa upana zaidi kabla ya kutoa suluhisho.
Mm kuna mdada nimekaanae miaka 10 na tumepata watoto 2 wakwanza wa kiume ana miaka 10 kwa sasa, na wakike ana miaka 5. Lakini mzazi mwenzangu tumetengana, na tumesumbuana sana swala la watoto, hadi tumeenda ustawi wajamii, nikawambia mm naomba kukaa hata na mtoto 1 lakini ustawi wa jamii, wamekataa,sijajuwa kwa nn wamekataa,
Lakini mama yao anaishi na watoto,na wakati mwingine awatesa sanasana, kwama huyo mkubwa amewahi,kumchoma na pasi ya umeme, akaja akamjeruhi paji la uso kwa kumpiga na kikombe cha udobgo na kuperekea kuchanika, akaja tena akampiga na uma sehemu ya jicho na kumuumiza, na bado akiamka asubuhi watoto ana wapangia kazi za kufanya hapo nyumbani, Naomba ushauri nifanyaje,
Naomba msaada niliishi na mwanamke Kama mke na mume,baada ya muda aliamua kuondoka na mtoto. Kwa vile mtoto alikuwa umri chini ya miaka Saba bas niliendelea kutuma mahitaji,na Sasa Ana umri zaidi ya miaka Saba ambayo kisheria naruhusiwa kuishi nae,lakin kutokana na tabia za mama yake amekuwa akimtumia mtoto ili aweze kupata chochote kutokana kwangu,
Ninaomba ushauri nifanyaje?
Asante
Nilifunga ndoa kanisani 2013 tukaishi kwa miaka mitatu tukatofautiana ila tulibahatika kuwa na mtoto mmoja Wa kike, tatzo alkuwa hamtunzi nikiwa kwake zaidi ya chakula tu, niliporudi nyumbani kwetu hakuendelea kumtunza mtoto Bali alikuwa akija kwa lengo LA kumchukua mtoto, ila sikukubali kwani mtoto alkuwa mdogo. Tulivutana sana kuhusu elimu kwa mtoto akitaka amchukue akasome mkoani kwao ila hakuweza nilimuomba asomee huku nilipo alikubali ila kishingo upande, sasa amefikisha umri Wa miaka 7 baba anakuja kumchukua kwasababu umri uliowekwa na sheria umefika na huku matumizi alikuwa hatoi zaidi ya shule aliyoanza kumpeleka mwaka Jana.
Alienda mahakamani nikaitwa nikiwa mkoa mwingine sikuweza kufika kwani nafanya kazi shulen kama secretary na kilikuwa kipindi cha mitihani,
Nimeshangaa kuskia karuhusiwa kuoa na kumchukua mtoto na sina barua yeyote niliyoisaini kwamba aoe na tatizo sio kuoa tatzo ni mtoto karuhusiwa kumchukua wakat hajamlea siku zote alkuwa akisubiri umri ufike atumie kama kigezo, naomba unisaidie nifanyeje??? Naumia mwanangu kulelewa na mama Wa kambo wakat miaka yote nilkuwa namuangalia Mimi. Asant
Naomba ufafanuzi, nilikua na mchumba akanitolea kishikauchumba baada ya muda nikaenda kumtembelea maana alikua mbali kidogo....lakini kutokana na tabia yake ya mabavu (kulazimisha tendo) na kipigo niliamua kuvunja uchumba....kwa bahati mbaya nikawa nina ujauzito ambao baada ya kumpa taarifa alisema mpaka turudiane ndo ahudumie, nilikataa na nikavunja mawasiliano nae kutokana na tabia zake chafu...... lakini pia nilipata mwanaume mwingine yey alinijali na alinihudumia hadi siku nikajifungua mtoto wa kike na akampa jina.....ametutunza vizur na sasa hivi nategemea kupata mtoto wa pili hivi karibuni
Shida inakuja yule mwanaume wa kwanza kaenda nyumban anadai anataka amchukue mtoto wake ambapo hajawahi kutoa hata Sumni kwa ajili ya mtoto, na najua anataka kunikomoa tuu
Hapo kisheria imekaaje na mtoto ana miaka mi3 na tunamtunza vizur
Asante.
Nimeachana na mwanaume alafu akamchukua mtoto kwa nguvu nifanyeje ili nmpate mtoto maana anamiaka 5 na hakai na babayke Bali Yuko kwa Bibi yake msaada plz
Mmmh �� kumbe shida hzo tupo wengi me nimenyimwa mtoto ana miaka 7 kwenye dawati eti mtoto kukaa na baba mpaka miaka 10 wataki mama katoroka nao tena akiwa shule na mitihani hajafanya��
Ulipata msaada?shida yangu ni kama yako Ila yangu zaid
Mimi nimezaa mtoto Ila baba yake hamuhudumii kwa lolote tangu amezaliwa ameshatoa Kama laki 3 tu na mtoto ana umri wamiaka nane Sasa na kasema anataka kukaa nae je Ni haki na sijampeleka kushtak popote na yeye anakipato kikubwa kuliko Mimi Mimi Sina uwezo mkubwa na yeye anaishi mkoa wa mbali Sana na mimi
Mm shinda na mwenzangu mtoto ataki kukaa naye yeye anampelekwa kwa mama yake nilaachana nae nikamwachia kila kitu lkn anaona Bora ampeleke kwa mama yake yeye mtoto ana mwaka 1 na mienz 3 mtoto aliachishwa ziwa akiwa na mienz 9
This comment has been removed by the author.
Hii changamoto ninayo hata Mimi mke wangu hawajibiki kabisa kwa upande wawatoto hajishughulishi kabisa na mpaka sasa sioni haja ya kuishi nae. Ushauri nifanyaje
Mimi baba wa mtt anamhitaji mtt wake kwa sasa anamika mi 4 lakin mtt tangu anamiez 5 had sasa hajawahi kumtembelea mtt na hata akiumwa na nikimjulisha haulizi chochote anaweza kaa hata miez 6 bila kuliza mtt wake anaendeleaje je naanzaje kumpa mtt baba wa stahili hii
Habari mimi naitwa charles Arobogast massawe nilikua naishi na mwanamke tulikua bado atujafunga ndoa ila mungu alitujalia mtoto mmoja wa kike ana miaka mitatu sasa ila tumetengana na mzazi mwenzangu yapata miezi sita sasa ila chaajabu nikimtafutaga huyo mwanamke ili tupange jinsi gani tutamlea mtoto yeye ananzaga kuja juu xana mbka inapelekea kutoa mbaka matusi bc mm naishiaga hapo tyu na kinachoniuma saidi ni kuwa ana kipato chakumtunza mtoto na anaishi na wanawake 2 chumba kimoja yeye wa 3 mtoto wa 4 embu niambie nn mtoto anajifunza hapo na ni wakike msaadha tafafhali
Asante sana kwa msaada wako wakisheria
NAOMBENI MNISAIDIE MKe wangu tuliacha akaondoka na mtoto akiwa na miaka 4 mazingira aliyo kwenda kuishi nae yalikua mabaya mno alikua anaingiza wanaume katka chumba alicho kuwa anaisha tena mpka mtoto nikienda kumsalimia ananiadisia bado akawa anauza bar anakaa bar na mtoto mpaka usiku baadae niliamua kuoa nakumchukua mwanangu akiwa na miaka 5 nimekaa nae mpaka muda wote mpaka sasa bado miezi6 tuu afikishe miaka saba mama wa mtoto amerudi tena anamtaka nimpe mtoto nimekataa na amekwenda ustawi wa jamii niliitwa kwa mara ya kwanza nikaenda nakutoa maelezo lkn hawakutaka kunielewa tuliambiwa tuondoke nitaitwa tena na mwanamke akapewa barua yakupeleka ustawi wa jamii iringa ambapo ndipo anapotaka kwenda kuishi na mtoto na mim naishi moshi Leo majira ya saa tano asubui nimepewa barua inayonitaka kufika ofis ya ustawi wa jamii na sikuweza kufika kwakua ilikuwa ghafla na tayar nilikua nahitajika katka shuhuli zangu jion Leo Leo jioni nimeletewa barua naitwa polisi dawati kitengo cha haki ya za wanawake na watoto na takiwa kufika tarehe 19 kesho kutwa sasa ndugu zangu mwenye kuweza kunipa ushauri namuongozo mzur juu ya hili naomba anisaidie na mungu awabariki wote mliosoma hii naomba msaada hata wakisheria
Kuna mwanamke nimezaa nae kantupia mtoto mara tatu mara ya kwanzaa mtoto akiwa na umri wa miezi Mitano mara ya pili miaka minne na mara ya tatu kamleta mtoto na miaka sita nidhi mancha ajabu miezi miwli tu kaja kumdai mtoto tena je hii imekaaje na vipi nifanye na sheria inasemaje?