NA BASHIR YAKUB -
Mara nyingi tunapoongelea
suala la ndoa huwa
tunarejea ndoa za
aina tatu. Kwanza huwa
tunaongelea ndoa za kidini,
pili ndoa za
kimila na tatu
ndoa za kiserikali.
Kila moja katika
ndoa hizi inazo
taratibu zake ambazo hutofautiana
na nyingine. Ndoa za
kidini na za
kimila mara nyingi
taratibu zake hujulikana
kwa wengi. Hii
ni kutokana na
ukweli kuwa ndoa
hizo hufungwa kwa
wingi na hivyo
taratibu zake ziko
wazi kwakuwa hushuhudiwa
mara kwa mara. Ndoa za kiserikali ( civil marriage)
mara nyingi taratibu
zake huwa hazijulikani
sana. Hii ni
kutokana na uchache
wa ndoa hizi
katika jamii zetu. Yumkini
kuna umuhimu wa
kuzijua kwakuwa waweza
kuwa mhitaji wa
kufunga ndoa ya
aina hiyo.
1.MAHITAJI YA KUFUNGA NDOA
YA KISERIKALI.
Mara zote ndoa
ni hiari. Na
hiari ya ndoa
hutokana na mapemzi
ya wahusika wawili.
Wakati mwingine hutokea
mapenzi yapo na uhiari upo
lakini mazingira ya
namna fulani hasa ya
kimila au kidini
yanazuia kabisa ndoa
kufungwa japo wahusika
wanahitaji ndoa. Hapa ndipo
mahitaji ya kufunga ndoa kwa mkuu
wa wilaya yanapokuja.
Yumkini ndoa hii inapofungwa
hadhi yake huwa sawa
na ndoa nyingine
zote na wahusika hustahili haki
zote za msingi
zinazotokana na ndoa.
2. SABABU ZINAZOWEZA
KUKUFANYA UFUNGE NDOA KWA
MKUU WA WILAYA.
( a ) Utofauti wa
dini. Hii ni
sababu kubwa inayoweza
kupelekea wahusika kufunga ndoa kwa mkuu
wa wilaya. Kifungu cha 25
cha Sheria ya Ndoa
kinasema
kuwa ndoa hutambulika
kuwa ni ya kidini inapokuwa
imefungwa kwa taratibu
za dini husika. Hata
hivyo karibia taratibu za
kila dini huruhusu
ndoa kwa sharti
kuwa wahusika wote lazima wawe waumini
wa dini moja. Kutokana na hilo
huwa si
rahisi kwa watu
wa dini tofauti
kufunga ndoa kutokana
na sharti hilo. Lakini
ndoa ya kwa mkuu
wa wilaya jambo
hilo halipo kwani watu
wa dini tofauti
wanaweza kufunga ndoa.
( b) Ndoa
inayofungwa kwa mkuu
wa wilaya hutoa
uhuru kwa wahusika
kueleza aina ya
ndoa wanayoitaka ikiwa
iwe ndoa ya mke
mmoja
au wake wawili. Ikiwa
watasema wanataka ya
mke mmoja basi
mwanaume hatoruhusiwa kuongeza
mke mbeleni na
ikiwa watasema wanataka
ya mke zaidi
ya mmoja basi mwanaume
anaweza kuongeza mke
mwingine mbeleni akiamua
kufanya hivyo. Ndoa za
kidini na kimila hazina
uhuru huu kwani taratibu
zake tayari zimepangwa
na hazibadiliki.
3. TARATIBU
ZA NDOA KWA
MKUU WA WILAYA.
( a ) Kwanza wahusika
watatakiwa kutoa taarifa
ya maandishi ndani
ya siku 21
kabla ya siku ya ndoa ikieleza
majina yao, ya
wazazi wao, nia yao ya kutaka
kufunga ndoa, umri wao , hadhi
yao ya kindoa
kama kuna mtu ana ndoa nyingine au
mjane au mseja. Pia
katika notisi hiyo
lazima ielezwe iwapo
wahusika hawana uhusiano
wowote wa kiundugu
uliozuiwa kwa mfano
wasiwe kaka na
dada, mtu na
shangazi yake au
mjomba wake,mtu na baba
yake au mama
yake n.k.
( b ) Ni
jukumu la ofisi
inayotarajia kufungisha ndoa
hiyo kutangaza notisi
hiyo ili ikiwa kuna mtu mwenye pingamizi
juu ya ndoa
hiyo ajitokeze na
kuwasilisha pingamizi lake. Ikiwa
kuna pingamizi lolote basi
bodi ya usuluhishi
wa ndoa ( Marriage Reconciliation Board) au
mahakama ndiyo itakayoamua
pingamizi hilo.
( c ) Ikiwa hamna
pingamizi lolote baada ya
siku 21 ndoa
itafungwa na maneno
yafutayo yatasemwa. Mwanaume
atasema “Mimi Fulani
ninamchukua fulani kama
mke wangu”. Na mwanamke
naye atasema “Mimi fulani ninakuchukua
fulani kama mme
wangu”. Ndoa itakuwa imekamilika
na wahusika baada
ya kusaini nyaraka
za ndoa wataruhusiwa
kuendelea na taratibu zao nyingine.
( d ) Kama
ilivyo ndoa zote
mashahidi huwa ni
suala la msingi
sana. Sheria imelazimisha wawepo
mashahidi wasiopungua wawili
katika ndoa hii
ambao umri wao ni
kuanzia
miaka 18 na
kuendelea. Pia wakati ndoa inafungwa
haitakiwi kuwa siri. Sheria
imesema kuwa watu
waruhusiwe kuwapo na kushuhudia kadri
eneo inakofungiwa litakavyokuwa
linaruhusu.
Hii ndio ndoa ya serikali ( civil marriage)
ambayo hujulikana kama
ndoa ya kwa
mkuu wa wilaya.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA
NA MSHAURI WA
SHERIA KUPITIA GAZETI
LA SERIKALI LA
HABARI LEO KILA
JUMANNE , GAZETI JAMHURI
KILA JUMANNE NA
GAZETI NIPASHE KILA
JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment