NA BASHIR YAKUB -
Badala ya kuendesha shule za kulea watoto kinyemela huko mitaani,
makala haya yatakueleza namna ambavyo unaweza kufanya kusajili na hivyo ukaendesha shughuli hii kihalali.
Ifahamike kuwa ni kosa
la jinai kuendesha kituo au shule ya kulea
watoto bila usajili. Kanuni ya 4( 1 ) ya
Kanuni za Vituo vya Kulea Watoto Wadogo Mchana na Watoto Wachanga za mwaka 2012, zinasema kuwa mtu hataendesha kituo cha kulea
watoto wadogo isipokuwa kama anamiliki cheti halali cha usajili. Kwahiyo epuka
kuingia katika kosa hili kwa kusajili kituo chako.Makala yatakuwa yakitafsiri
Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009, pamoja na Kanuni za Vituo vya Kulea Watoto
Wadogo Mchana na Watoto Wachanga za mwaka 2012.
SIFA ZINAZOHITAJIKA
KABLA YA KUOMBA USAJILI.
1.Eneo ambapo kituo kitajengwa litatakiwa kukaguliwa na
afisa afya wa eneo husika na kutoa ripoti ya kuridhisha kuwa panafaa kwa ajili
ya kulelea watoto. Hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 4(3).
2. Kama eneo/jengo ambapo utaendeshea kituo ni la
kupanga basi hakikisha una mkataba wa pango ambao hauko chini ya miaka
mitatu. Kanuni ya 4(4).
3. Utatakiwa kuthibitisha uwezo wa
kifedha kuwa unaweza kuendesha kituo.
4. Hakikisha eneo lina vifaa vya
kutosha kwa ajili ya michezo ya watoto. Hii ni kutoka kifungu cha 47(1)( c ).
5. Muombaji/waombaji wawe na akili
timamu.
6. Uthibitisho kuwa baada ya kupewa
cheti cha kuendesha kituo hautatoa, kuuza, kukodisha kituo au cheti chako kwa mtu mwingine yeyote.
BAADA YA HAYO SASA WAWEZA KUOMBA USAJILI KWA UTARATIBU HUU.
1. Jaza fomu ya maombi iitwayo D.C.C No. 1 kwa mujibu wa kanuni za Vituo vya Kulea Watoto Wadogo Mchana na Watoto
Wachanga za Mwaka 2012.
Fomu hii unaweza kuikopi au kuipakua kutoka kwenye hizi
kanuni au ukaenda kuiomba ustawi wa
jamii. Ukishaipata utaijaza kama inavyojielekeza.
2. Baada ya kujaza hiyo fomu ya maombi
sasa utaiwasilisha kwa Kamishna wa ustawi wa jamii kwa mujibu wa kifungu cha
47(1) cha Sheria ya Mtoto.
3. Baada ya kupokea maombi yako
Kamishna ataweka utaratibu wa kukagua eneo husika.
4. Baada ya kuridhika na ukaguzi basi
Kamishna atatoa cheti cha usajili kwa mujibu wa kifungu cha 147(6) Sheria ya
Mtoto.
Namna hiyo utakuwa umesajili kituo.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment