NA BASHIR YAKUB -
Wapo watu wanaojua kuwa kuendesha gari kwa mwendo mdogo ndio
ustaarabu na ndio jambo zuri linalopendwa sana na sheria. Yeyote mwenye mawazo ya aina hii amekosea sana. Kifungu cha 56 cha
Sheria ya Usalama Barabarani, Sura ya
`168 kinakataa dhana hii. Kifungu hicho kinasema kuwa “dereva wa gari au teela ambaye bila sababu za msingi ataendesha kwa
mwendo mdogo(low speed) ambao utaelekea
kuwasababishia watumiaji wengine wa barabara usumbufu au utawasababishia
usumbufu, atakuwa ametenda kosa na panapo hatia yake atatakiwa kuadhibiwa kwa kulipa
faini”.
Maneno bila sababu za msingi hapo juu humaanisha kuwa kama itatokea mtu anaendesha kwa mwendo
mdogo basi kuwepo na sababu za msingi za kufanya hivyo na hapo ndipo anaweza
kukwepa kuingia katika kosa hili. Sababu za msingi zaweza kuwa foleni kubwa na
hivyo huwezi kuongeza mwendo, unaendesha ndani ya msafara rasmi unaotambulika
kisheria, maelekezo ya vibao na alama za
usalama za eneo hilo yanakuelekeza kuendesha kwa mwendo huo, ubovu wa barabara
ambao haukuruhusu kwenda mwendo mkubwa, barabara imezuiwa na waandamanaji au
halaiki(population) nyingine ambayo
haikuruhusu kwenda haraka.
Ubovu wa gari unaweza kuwa sababu ya kutembea taratibu lakini sio sababu ya msingi. Sheria hii
inaelekeza gari likiwa bovu kutokuendeshwa barabarani kwa maana ya kuwekwa
pembeni ili kulirekebisha au kutafuta namna nyingine.
Kwahiyo usiwasababishie watu usumbufu barabarani kwa kudhani
kuendesha mwendo mdogo ndio uendeshaji mzuri na bora. Askari wa usalama barabarani
anayo mamlaka ya kukusimamisha na kukutoza faini kwa kuendesha mwendo mdogo
bila sababu za msingi.
Unakuta msururu wa magari yanayotembea taratibu, unadhani
mbele kuna tatizo kumbe kuna mtu anatembea mwendo wa kinyonga. Akisumbuliwa kwa honi anadhani wanamwonea yeye
ndiye yuko sahihi zaidi kwakuwa anaendesha mwendo mdogo. Hili ni kosa unaweza kupiga hata simu polisi
ukaomba msaada wa kukamatwa na kuadhibiwa kwa mtu wa aina hii.
Aidha, ifahamike kuwa vibao/alama za barabarani ndizo mwongozo
mkuu wa kiasi cha mwendo wa kuendesha. Kwahiyo hatua ya kwanza ni kuhakikisha
unafuata alama hizi za mwendo zilizoko barabarani. Pale ambapo hazipo basi
haifai kuendesha mwendo mkubwa sana wala mwendo mdogo sana. Ni kutumia mwendo
wa kati kwa kati.
Mwendo kasi pekee ndio umekuwa ukipigiwa sana chapuo kama
kosa, lakini kumbe hata mwendo wa polepole nao unaweza kuwa kosa.
Ni ukweli usio na ubishi kuwa mwendo mdogo pasipostahili
unaweza kukusababishia wewe mwenyewe ajali au ukawasababishia watumiaji wengine
ajali.
Basi, ilikuwa ni muhimu hili nalo kujulikana ili wale wenye
imani zao kuwa kwenda polepole ndio utiifu wajue kuwa sio kweli. Na pengine
siku nyingine wakiadhibiwa wasione wameonewa.
Yatutoshe hayo, fuata sheria acha kuwasababishia watu
usumbufu.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
Casinos Near Casinos in Chicago by Phone - MapYRO
Find the nearest Casinos 강릉 출장샵 in Chicago 여주 출장샵 by Phone. MapYRO provides 의정부 출장안마 a complete listing 안동 출장샵 of all Casinos with at 계룡 출장샵 least 534 slot machines in Chicago.