NA BASHIR YAKUB -
Yafaa kujua utaratibu unaotakiwa kufuatwa
kabla ya kufutiwa hati miliki
ya ardhi (nyumba/kiwanja). Unapojua utaratibu huu
ndipo unapojua kama ulionewa
au hapana. Na kuonewa ni pamoja na
kukiuka utaratibu. Na kukiuka taratibu yoyote ya
kisheria kunabatilisha mchakato
wa kufutwa kwa
hati yako na kutakiwa kurudishiwa
eneo lako au
fidia.
Makala yaliyopita tulieleza mambo ambayo
ukifanya unahesabika kukiuka
masharti ya umiliki wa
ardhi na ni hapo unapoweza
kufutiwa umiliki. Leo tuangalie
utaratibu wa kufuta umiliki ikiwa imethibitika kuwa
tayari umekiuka masharti
hayo. Sheria namba 4 ya 1999 ,
Sheria Ya ardhi
imeeleza utaratibu wa
kufuta umiliki wa ardhi.
UTARATIBU.
1.Ni
lazima uwe umekiuka masharti
au moja ya
masharti uliyopewa wakati unakabidhiwa
ardhi/hati kwa mujibu
wa kifungu cha 48 ( 1) cha Sheria
ya ardhi. Usikubali kufutiwa
umiliki ikiwa hujakiuka
sharti/masharti ya umiliki uliyopewa, labda iwe
vinginevyo.
2. Baada
ya kuwa umekiuka
masharti yafaa upewe
taarifa maalum( notice) kwa mujibu
wa kifungu 48(2). Ni taarifa inayoeleza masharti
ya umiliki uliyokiuka
na onyo la
kufutiwa umiliki. Taarifa
hiyo ni ya
siku 90(miezi mitatu). Taarifa
hiyo utapewa wewe mmiliki na
kila mwenye maslahi
katika ardhi hiyo
mf, mpangaji, mrehani nk.
3. Baada
ya siku 90 kuisha na
pengine hujajirekebisha au
kufanya kile ulichoambiwa
kufanya basi kamishna
wa ardhi atatakiwa
kupeleka pendekezo kwa
rais ili kufutiwa umiliki. Ni rais
tu mwenye mamlaka
ya kufuta umiliki
wa ardhi.
Zingatia, barua au
nyaraka nyingine yoyote ambayo inasema umefutiwa
umiliki lakini aliyefuta
sio rais wa
nchi, sio halali.
4. Ikiwa rais
atakubali kukufutia umiliki
wa ardhi basi inatakiwa kufutwa huko
kutangazwe katika gazeti
maalum la serikali/taarifa ya serikali(GN)
na katika gazeti
la kawaida(newspaper) ambalo
linafika eneo ardhi
yako ilipo. Hii
ni kwa mujibu
wa kifungu cha 49(1).
Ili utaratibu uhesabike
umefuatwa ni lazima
matangazo haya yatolewe
la sivyo kufutiwa
huko kunabatilika.
5. Rais
atakapofuta umiliki wa
ardhi basi ardhi hiyo
itahama kutoka kwa mmiliki wa
awali kwenda serikalini au
vinginevyo itakavyoamriwa kwa
mujibu wa kifungu cha 49(2).
6. Ikiwa kuna
maendelezo yoyote ya
kudumu ambayo ulifanya
kwenye hiyo ardhi
basi ni lazima
ulipwe fidia ya
maendelezo hayo kwa
mujibu wa kifungu
cha 49(3).
Isipokuwa maendelezo hayo
yawe yalikuwa ni sehemu
ya masharti ya
umiliki wa ardhi
hiyo. Yasiwe nje
ya yale uliyokuwa
umepewa kwenye umiliki.
7. Ikiwa ardhi
hiyo ilikuwa inadaiwa
kodi au tozo za ardhi basi kodi
na tozo hizo
zinaondolewa na deni
hilo linakufa, mpaka isemwe
vinginevyo. Hii ni
kwa mujibu wa
kifungu cha 49(2)(e)..
NAMNA YA
KUDAI HAKI YAKO
IKIWA TARATIBU ZIMEKIUKWA.
Kwanza, waweza
kupeleka malalamiko yako
kwa kamishna wa
ardhi na baadae
kwa rais. Utaandika barua
ikieleza kile ambacho unahisi
kuonewa au taratibu kukiukwa.
Pili, ni kupeleka malalamiko
yako mahakamani. Hapo sio barua
bali utapeleka nyaraka maalum
za kufungulia shauri(Plaint/Application). Humo pia
utaeleza pahala unapohisi
kuonewa au taratibu kukiukwa pia.
Pia unaqweza kuchukua
hatua hizi kwa
pmoja na kwas wakati moja.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA
NA MSHAURI WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment