NA BASHIR YAKUB -
Unapopekuliwa yapo mambo
ambayo usipoyazingatia wewe
unayepekuliwa basi yatakuingiza
matatani mbeleni au
hata kama umebambikiziwa kosa
itaonekana ni kweli na
waweza kwenda jela
bila kuwa umetenda
kosa lolote.
Kawaida
wanaopekua ni askari. Usitarajie
huyu anayekuja kukupekua
awe ndiye wa
kukwambia haki zako . Badala
yake wewe unayepekuliwa ndiye
uwe wa kumwambia
askari kuwa hiki
ndicho hiki hapana. Askari
anapokuja kukupekua tayari
wewe unashukiwa na hivyo ni
rahisi kwake kuacha kufuata au
kuongeza jambo lisilokubalika
ilimradi atimize lengo
lililomleta. Wewe ndiye wa
kusema hili ndio
na hili hapana.
Hivyo basi ni muhimu sana kwako
kujua kuhusu kupekua
na mambo gani
ya msingi ufanyiwe
au usifanyiwe ili
kuepuka uwezekano wa kwenda jela
bila kosa.
Usiseme mimi sina haja
ya kujua kuhusu
kupekua kwasababu ni
mwema sana na
hivyo si rahisi kutakiwa
kupekuliwa. Laa hasha, kupekuliwa na
kukamatwa na polisi
humkumba yeyote awe mwema
ama vinginevyo. Kujua ni
silaha na hivyo
ni muhimu kukaa
na silaha hii.
Makala yatapitia sura
ya 20, vifungu vya 38 hadi 45 vya Sheria
ya Mwenendo wa Kesi
za Jinai .
1.NANI ANARUHUSIWA
KUKUPEKUA.
Askari ndiye anayeruhusiwa kukupekua. Hata raia
wanaweza kumzuia raia
mwenzao wakampekua ikiwa
wana taarifa kuhusu kuficha au
kumiliki kitu ambacho ni
kosa kwa mujibu
wa sheria. Isipokuwa
ni haramu kabisa
kwa raia kumpekua
raia mwenzake bila
kuwa na kibali
maalum.
2. VITU
GANI VINAWEZA KUPEKULIWA.
Mtu kama mtu
anaweza kupekuliwa, kwa
maana nguoni mwake
kama mifukoni nk. Pia
vifaa kama gari,
,meli, nk navyo vyaweza
kupekuliwa. Halikadhalika nyumba
kama nyumba nayo yaweza
kupekuliwa pamoja navyo
vifaa vingine.
3. JE
WAWEZA KUPEKULIWA MDA
WOWOTE.
Hapana, si kweli
kuwa waweza kupekuliwa
mda wowote anaotaka
askari. Sheria niliyotaja
hapo juu inasema
mda wa kupekua
ni kuanzia jua
linapochomoza na mwisho
ni linapozama. Yametumika
maneno jua kuchomoza
na kuzama badala
ya kutaja mda labda
saa 11 za
asubuhi mpaka saa 12 za
jioni kwasababu ya utofauti wa jiografia
ya sehemu na
sehemu.
Muonekano wa saa
12 za jioni
wa kanda ya
ziwa ni tofauti
na ule wa
pwani nk. Kwahiyo
kutaja saa kwa
lengo la kumaanisha
usiku unapoingia na
unapotoka ingekuwa kama inapotosha.
Hata hivyo inawezekana
tu kupekuliwa nje ya
muda huo kwa
kibali maalum cha mahakama.
4. MPEKUAJI KUAMBATANA
NA SHAHIDI MWENYEJI.
Askari anayepekua aje
na shahidi mwenyeji. Mjumbe au
kiongozi kutoka serikali
za mitaa ni mtu
muhimu kuwa mwenyeji. Jirani pia anaweza kuwapo. Hii
ni kuhakikisha wanakuwa
mashahidi kuwa hakuna
kilichoingizwa ndani wakati
kuingia kupekua na pia kushuhudia
vinavyochukuliwa.
5. ORODHA
YA VITU VINAVYOCHUKULIWA.
Ni lazima kila
kinachochukuliwa kuandikwa kwenye
orodha maalum . Orodha
hiyo utaisaini wewe uliyepekuliwa, askari
aliyekupekua, pamoja na mashahidi
ambao ni mjumbe au
serikali za mitaa au
jirani mwema.
Hii huepusha badae
kuambiwa kuwa hata
kitu fulani ambacho kinajenga
kosa kuwa kilikutwa kwako. Lakini
pia ni muhimu
kwa ajili ya
kurejesha mali zako
baadae zikiwa zimetimia.
6. KIBALI
CHA KUPEKUA.
Askari mwenye cheo
chini ya Sub Inspector
haruhusiwi kupekua nyumba
au eneo la mtu bila
kibali maalum aidha kutoka
mahakamani au kutoka
kwa mkubwa wake mwenye cheo
cha Sub Inspector
kwenda juu. Hii
ni kwa kesi
ya kupekua nyumba.
Kwa kesi ya
kupekua mtu binafsi
pale anaposimamishwa au
upekuzi wa gari
na vifaa vingine
askari yeyote anaweza
kupekua bila kibali.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
tatizo la polisi ukijua sheria ya haki zako,ndivo unavo jitengenezea mazingira magumu kuwa adui yake
Good