NA BASHIR YAKUB -
1.ZUIO LA
MAHAKAMA NININI.
Ni amri inayotolewa
na mahakama kumzuia
mtu kutofanya jambo fulani
kwa
muda. Kampuni nayo ni
mtu ambapo yaweza
kuomba zuio au
kuzuiwa. Aidha yeyote ana haki ya
kuomba amri hii
ikiwa anaona kuna
jambo fulani linafanyika
na ikiwa litaendelea
kufanyika basi litaharibu
au kupoteza kabisa
kitu fulani.
Kwahiyo zuio ni
amri inayobeba maagizo maalum
kwa mtu au
watu maalum kuwaamrisha
kutoendelea na kitu
fulani kama tulivyoona
hapo juu.Sheria ya Mwenendo
wa Madai, Sura ya 33 na Sheria
nyingine mtambuka zimeongelea
kuhusu zuio.
2. KATIKA MATUKIO GANI
UNAWEZA KUOMBA ZUIO.
( a ) Kwa
mfano, umeshindwa kulipa mkopo
na tayari una
taarifa kuwa benki au
taasisi yoyote ya
fedha inataka kwenda kuuza
na unahisi kuna
pahala hapaendi sawa katika
mikataba yenu.
Basi unaomba
zuio ili hiyo
mali yako uliyoweka
rehani isiuzwe mpaka
hapo hilo eneo ambalo
mmeshindwa kuelewana litakapopatiwa
majibu.
( b ) Kwa mfano, umemuuzia mtu gari,
pikipiki, au mashine
yoyote. Mtu huyo
hajalipa kiasi cha
pesa iliyobaki kama mlivyokubaliana. Lakini anaendelea
kutumia kifaa hicho. Unaweza kuomba
kumzuia kuendelea kutumia
mpaka atakapolipa kiasi
kilichobaki ili asiendelee
kuharibu au kuzeesha
kifaa hicho.
( c ) Kwa
mfano, we ni mpangaji
katika nyumba ya kuishi au biashara.
Mwenye nyumba,eneo anataka kukutoa
kwenye pango hilo
bila kufuata utaratibu
au kwa kukiuka baadhi ya
makubaliano kwenye mkataba
wenu. Unaweza kuomba zuio asiendelee kukutoa.
Pia
mazingira mengine yoyote
ambayo unahisi kuna kitu, jambo
linataka kuharibiwa au kuingiliwa,
kuuzwa, kupotezwa,kufichwa kinyume na
utaratibu unaweza kuomba
zuio hilo.
3. SHARTI KUU .
Ili
uweze kuomba zuio
ni lazima pia kuwepo na
shauri la msingi.
Kwa maana utafungua
shauri la msingi kulalamikia
jambo fulani halafu utaomba zuio
ndani ya shauri hilo. Kwa
mfano unafungua shauri
kulalamikia mwenye nyumba kusitisha
mkataba wa pango
bila kufuata utaratibu.
Hilo
ni shauri kuu.
Halafu ndani mwake
unafungua shauri dogo
la kuomba zuio ili
asikuondoe katika nyumba
mpaka kwanza shauri kuu
la kukiuka utaratibu
litatuliwe.
Kwahiyo ni sharti kuwapo
shauri kuu ukilalamikia jambo fulani halafu ndani
mwake ndio uombe
zuio.
4. UMUHIMU WA
ZUIO.
( a ) Linasaidia mali yako
kutouzwa au kutoondolewa
kwenye nyumba kama
mgogoro unahusu nyumba.
( b )
Linalinda mali yako
isiharibiwe ,isifichwe, isihamishwe,isiingiliwe kwa
namna yoyote ile
kama ipo katika
mazingira hayo.
( c )
Linakupa nafasi ya kutafakari na kujipanga ikiwa
upo katika presha
ya kukimbizana na
jambo ama mgogoro.
( d ) Linatoa mwanya
wa mazungumzo kati
ya mlalamkaji na
mlalamikiwa.
5. WAPI UKAOMBE ZUIO.
Zuio
linaombwa mahakamani. Na linaweza kuombwa
mahakama yoyote katika shauri
lolote. Linaweza kuombwa kwenye
mashauri ya ndoa, mirathi, ardhi,
biashara, mikataba, madai ya
kawaida ya pesa au mali, makampuni n.k.
Na
linaombwa katika mahakama
zote yaani ya
mwanzo, ya wilaya,
ya hakimu mkazi mahakama kuu na ya
rufaa pia. Lakini
pia linaombwa kwenye
mabaraza ya ardhi
ya kata na
wilaya.
6. KUKIUKA AMRI
YA ZUIO.
Ikiwa
utaomba zuio na
kupata halafu aliyezuiwa
akakiuka na kuendelea
na kile alichozuiwa
basi kosa linabadilika na
kuwa la jinai. Inakuwa jinai ya kuingilia
amri na shughuli
za mahakama. Ni
kosa ambalo aliyekiuka
amri hiyo akithibitika
ni kweli
kakiuka basi atatakiwa
kwenda jela miezi
sita ama vinginevyo.
Kinachotakiwa kwako ni
kuripoti tu kuwa
amri iliyotolewa sasa
haitekelezwi na yule aliyeamrishwa
kutekeleza. Utaripoti mahakama
hiyo hiyo iliyotoa
zuio hilo.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA
NA MSHAURI WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment