Na Bashir Yakub -
1.LESENI YA MAKAZI
NININI.
Leseni ya makazi
ni leseni/kibali maalum kinachotolewa kwa
mmiliki wa makazi
ili kutambua na
kurasimisha makazi hayo.
Leseni ya
makazi ni nyaraka
ya umiliki wa
makazi kama ilivyo
nyaraka nyingine za umiliki
wa ardhi. Leseni
ya makazi ni
kwa ajili ya
ardhi makazi tu
na si ardhi
nyingineyo.
2. JE
LESENI ZA MAKAZI
ZINATAMBULIWA NA SHERIA.
Ndio, leseni za makazi
ni kwa mujibu
wa sheria namba
4/1999 Sheria ya Ardhi.
Leseni za makazi
zinatambuliwa na kifungu
cha 23 cha sheria hiyo.
Kwahiyo wanaodhani kuwa
leseni za makazi
ni mpango tu
wa serikali za
mitaa na watendaji
wa kata wajue
sio kweli. Leseni
za makazi ni
nyaraka iliyo kisheria
kwa mujibu wa
kifungu hicho japo
juu.
3. TOFAUTI
YA LESENI YA
MAKAZI NA HATI .
Hati ni “Right Of Occupancy”
kwa jina la
kitaalam, wakati leseni
ya makazi ni “Derivative Right” .
Tofauti za viwili hivi
ni nyingi ila kubwa
ya kukufanya uelewe ni
kuwa, leseni ya makazi
hutolewa kwa makazi ya mjini
ambayo hayajapimwa na
hayakuwa rasmi lakini
yasiyo hatarishi.
Wakati hati
hutolewa katika makazi
rasmi na ambayo
yamepimwa. Isipokuwa la
kuzingatia ni kuwa
iwe leseni ya makazi
ama hati vyote
vinatambuliwa na serikali kama
nyaraka rasmi za
umiliki na kila
moja ina haki
sawa na nyingine katika
umiliki.
4. NANI
HUTOA LESENI ZA
MAKAZI.
Leseni za makazi
hutolewa na manispaa husika. Iwe
kubadili jina au kupata mpya
ni kazi inayofanywa
na manispaa ya
yalipo makazi husika. Hii
ni kwa mujibu
wa kifungu cha
23( 3) Sheria ya Ardhi.
5. MASHARTI YA KUPATA
LESENI YA MAKAZI.
Kwanza, muombaji awe Mtanzania
aliyefikisha umri wa
miaka 18 au
zaidi. Pili, awe ndiye
mmiliki wa makazi
husika. Tatu, eneo lisiwe katika
maeneo hatarishi au maeneo ya hifadhi. Nne, eneo liwe
maeneo ya mjini. Tano, yawe ni
makazi kwa kipindi
kisichopungua miaka mitatu. Sita, lisiwe eneo
ambalo lina hati ya kawaida au
hati ya kimila. Saba, malipo
ya ada na tozo
nyingine zitalipwa kwa mujibu
wa kifungu cha 23 (3)( c ).
6. FOMU INAYOJAZWA
NA MUOMBAJI.
Muomba leseni ya
makazi anatakiwa kujaza
fomu namba 73 kwa
mujibu wa kifungu cha
170 Sheria namba 4 ya ardhi. Kwenye
fomu hiyo jina la
mwombaji litahitajika, anuani yake na
ya makazi, aina ya
umiliki anaoomba kama
ni binafsi, kundi, familia,
kampuni, taasisi nk, taarifa za mtaa, kata, wilaya, taarifa
za matumizi ya
ardhi kwa sasa, matumizi mapya
yanayoombewa leseni, ukubwa wa
eneo husika, kutakuwa na sehemu ya
maoni na mapendekezo ya mwenyekiti
serikali ya mtaa, sahihi yako,
dole gumba na
picha zako.
Fomu hii inapatikana kwa wanasheria, au manispaa,
au hata ofisi nyingine
za kata wanazo.
7. MUDA WA LESENI YA
MAKAZI.
Kifungu cha 23 (3) ( b ) kinasema kuwa
leseni ya makazi
itatolewa kwa muda ambao sio
chini ya miezi
sita lakini sio
zaidi ya miaka 5. Kwahiyo muda
wowote utakaopewa kati
ya muda huo
utatakiwa uhuishe ( renew)
baada ya
kuisha kwake.
Maana
yake, ukipewa miaka 2 basi ikiisha
huisha(renew). Halikadhalika miaka 3, 4 5, 1,miezi 6 ,8, 10 nk.
Kwa ufupi haya
yatakufaa.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
Saaafi, kuna mtu alikua anasema hakuna shwria inayosimamia leseni ya makazi
Asante kwa taarifa nzuri kuhusu leseni ya makazi. Nina swali. Mdogo wangu amemilikishwa eneo langu kwa makosa. Nifanyeje kubadili jina lake kuja kwangu?