NA BASHIR YAKUB -
Jirani yako au
mtu mwingine yeyote
amejenga na kuziba
njia. Njia yoyote iwe kubwa
kama barabara ama ndogo ambayo
hata gari haiwezi
kupita. Iwe tu kama ya pikipiki
au baiskeli au hata ya
miguu tu. Yote
haya hayajalishi na hizi
zote ni njia kwa
mujibu wa sheria.
1.HAKI YA
NJIA KISHERIA .
Kifungu cha 151
cha sheria namba
4 sheria ya
ardhi ya mwaka
1999 kinaeleza haki hii. Kinaitambua haki
hii kwa kusema
kuwa haki ya
njia ipo kwa njia zile
ambazo ni kwa ajili
ya matumizi ya
umma. Umma hapa
humaanisha watu wote
lakini pia wakazi
wa eneo fulani
wanaotumia njia hiyo
kwa ajili ya
shughuli zao mbalimbali.
Kifungu kimepanua matumizi ya
njia ya umma
kwa kumaanisha hata
njia zilizotengwa kwa ajili
ya makampuni binafsi. Kwa
mfano kuna sehemu
ukipita utaona njia au
sehemu ya lami
ya barabara imekatwa maalum
kwa ajli ya
kuruhusu watu au magari ya
kampuni fulani kupata
sehemu ya kuingilia.
Lakini pia zipo
njia zimetengwa kwa ajili ya
shughuli za serikali. Haraka utaona
kuwa haki ya njia haijagusa tu
kule mitaani wanakoishi
watu tu bali
hata sehemu za
makampuni binafsi nk.
2. KUZIBA
NJIA YA UMMA.
Kuziba njia ya
umma ni kosa
kwa mujibu wa
kifungu cha 177( 4 ) cha
sheria ya ardhi. Wako
watu wakorofi huko
mitaani huziba njia
kwa makusudi. Yawezekana kabisa mtu
akiwa anajua kabisa eneo fulani
ni njia na
watu hupita hapo
lakini kwa makusudi au bila
kujali akajenga ukuta au akaweka uzio wa
sinyenge au akapanda
mti pale au akaweka kifusi au
kwa namna nyingine
yoyote.
Na wengine huambiwa
na watu lakini
wasisikie kwasababu ya
pesa, au urafiki
na viongozi wa
serikali au cheo
au rushwa au vinginevyo.
Basi
yatupasa kujua kuwa watu
hawa huwa wakitenda
makosa na si wakunyamazia.
Njia kuzibwa si lazima
iwe imezibwa yote. Hata kuibana na kuitoa katika
uhalisia wake katika
kiwango chochote nako
ni kuziba njia.
Njia yafaa iachwe
vilevile ilivyo.
3. NINI
UFANYE IKIWA NJIA
IMEZIBWA.
Yako mambo mawili
unaweza kufanya ikiwa mtu
amewazibia njia. Moja ni
jepesi na la
pili sio jepesi. La
kwanza ni kwenda
mahakamani kwa kufungua
malalamiko na pili
ni kupeleka malalamiko
kwa kamishna wa
ardhi.
Kwenda mahakamani ni njia
ambayo sio nyepesi sana.
Ina gharama , na
inapoteza muda zaidi. Na
ikiwa utaamua kwenda mahakamani
basi mahakama inayotumika
katika mambo kama haya ni
mahakama ya ardhi.
Baraza la ardhi
la kata na
la kijji ni sehemu
ya mahakama za
ardhi. Hata hivyo kama
utaamua kwenda mahakamani
ni vema zaidi
ukaanza na mabaraza
haya ya kata na kijiji.
Na uzuri mabaraza haya
hayana gharama, na kesi
haichukui mda mrefu.
Ni tofauti na
ukiamua kutumia baraza
la ardhi la
wilaya au mahakama
kuu ya ardhi.
La pili ambalo
sasa ni ndilo jepesi ni kupeleka
malalamiko kwa kamishna
wa ardhi . Kifungu cha 176 (
1) kinasema kuwa kamishna wa
ardhi ana mamlaka ya
kutoa amri kuhusu
njia iliyozibwa ikiwa
ataridhika kuwa ni kweli
njia imezibwa tena kimakosa.
Kwa hiyo badala
ya kuhangaikia mambo mengine
ni bora basi
ukapeleka malalamiko yako
kwa kamishna wa ardhi
naye atatoa amri
ambayo ni lazima
kwa aliyeziba njia
kuitekeleza.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment