NA BASHIR YAKUB -
Wanaokopa hela kwenye
taasisi za fedha
wanatakiwa kujua haki
walizonazo. Haki kabla ya
kuchukua mkopo, haki wakati
wa kuchukua mkopo, haki
wakati wa kurejesha,
na haki baada
ya kurejesha au kushindwa
kurejesha. Hautakiwi kusubiri taasisi
iliyokukopa iwe ndiyo ya kukueleze
haki ulizonazo bali watakiwa
ujue haki hizo
kwa jitihada zako.
Taasisi ya fedha
inaweza kukueleza baadhi
ya haki lakini
ni muhali kukueleza
haki ambazo wao zinawabana.
Watakueleza haki ambazo hazina
madhara kwao.
Basi
yakupasa ulijue hili.
Masuala ya kuweka
rehani ili upate
mkopo yanaongozwa na
sheria mbili. Sheria
namba 4 ya
mwaka 1999 Sheria
ya ardhi, pamoja
nayo Sheria namba
17 Sheria ya
rehani ya mwaka
2008. Humo zimo haki nyingi
za mtoa mkopo
wakadhalika mchukua mkopo.
Hata hivyo tutatizama
haki moja tu ya
notisi kabla ya
kuuzwa kwa nyumba/kiwanja
cha mkopaji.
1.KUSHINDWA KUREJESHA
MKOPO.
Kifungu cha 127 ( 1 ) cha
sheria ya ardhi
kinaeleza habari ya
kushindwa kurejesha mkopo. Kifungu kimeieleza
habari hii ikiwa
miongoni mwa mambo
ambayo yanachukuliwa kama ukiukwaji wa masharti
ya mkataba wa
mkopo.
Mengine ambayo
yanachukuliwa kama ukiukwaji wa
masharti ya
mkopo ni kuweka rehani
mara zaidi ya
mmoja kwa taasisi
tofauti, kuuza, kupangisha
wakati kuna rehani
bila taarifa au
ridhaa kutoka kwa mtoa
mkopo n.k. Hata hivyo
haya na mengine
yatachukuliwa kama kukiuka masharti
ya mkopo ikiwa yamekatazwa katika
mkataba wako na
taasisi ya fedha.
Pia kwa mujibu
wa kifungu hicho
kushindwa kurejesha mkopo
kunajumuisha pesa kamili
uliyoikopa, riba, pamoja na
makato mengine ambayo
yanajenga sehemu ya
mkopo.
2. NOTISI
YA SIKU 60.
Hii ni notisi
ya lazima kabla
nyumba/kiwanja chako hakijauzwa. Si
tu lazima upewe bali pia
ni lazima iwe
ya siku 60. Kamtindo
ka kuwapa watu
siku 14 au
chini yake au
zaidi kidogo kanakiuka
sheria. Na hapo baadae tutaona
ufanye nini ikiwa
hilo limekiukwa.
Kifungu cha 127( 1 ) ( a ) kimeeleza kuwa pale mkopaji
anapokuwa ameshindwa kurejesha
kwa mujibu wa makubaliano
ya mkopo basi taasisi
ya fedha itampa
mkopaji taarifa( notice) ya
siku 60 ambapo
siku hizo zikiisha
kabla mkopaji hajalipa
basi taasisi hiyo inaweza
kuendelea na hatua za kuuza
ikiwa itaamua kufanya
hivyo.
Kwahiyo ni lazima
kuwepo na taarifa
ya siku 60. Na
siku hizo zinaanza
kuhesabiwa tokea siku
ulipopokea notisi ya kwamba umeshindwa
kulipa. Hivyo basi ukipokea
notisi leo anza kuhesabu mpaka
siku 60. Humo
katikati hawataruhusiwa kuuza
mali yako. Na wakiuza
ndani ya muda huo basi
itakuwa ni makosa.
Juu ya hilo
ni vema pia
ukajua kuwa notisi hiyo
ya siku 60
haihusishi tu uwezo
wa kushindwa kulipwa.
Bali pia lolote
lile ambalo ni
sharti katika mkataba
wa mkopo na
ambalo taasisi ya
fedha inadai umelikiuka. Hapo pia
haitachukua hatua ya
kuuza mali yako
hadi upate notisi
hiyo ya siku
60.
3. NINI
UFANYE IKIWA
NOTISI HIYO ITAKIUKWA.
Kwanza kama nyumba/kiwanja hakijauzwa
kimbilia mahakamani na
weka zuio, na
pili kama tayari
mali imeuzwa tena kwa
kukiuka notisi na muda
wake basi unaweza
kufungua shauri la
kubatilisha mauzo hayo
kwa msingi wa
kukiukwa kwa taratibu
za mauzo na
waweza kurejeshewa mali
yako.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment