NA BASHIR YAKUB -
Wapo wazazi wanaowakatalia wazazi
wenzao kuwaona watoto/mtoto
baada ya kuwa
wameachana. Wengine hawakuachana
bali hawakuwahi hata kuishi pamoja isipokuwa
walizaa tu lakini
yule mzazi anayeishi
na mtoto anamzuia
mzazi mwenzake kumuona
mtoto husika.
Basi makala
haya yatatizama jambo
hili kwa sura
ya sheria zetu.
Uhalali wake na
uharamu wake, hatua unazoweza
kuchukua na mtazamo
wa jumla ikiwa jambo
hili ni haki
kisheria ama laah.
Sheria namba 21
ya mwaka 2009
Sheria ya Mtoto
ndiyo itakayotupatia majibu
ya suala hili
kwa ujumla wake.
1.KUMUONA MTOTO
HUMAANISHA NINI.
Unapotizama kwa
ujumla sheria ya
mtoto hasa vile
vifungu vinavyozungumzia habari
ya kumuona mtoto
utaona kuwa vinazungumzia kumuona
mtoto kwa maana
ya hatua ya baba
mzazi, mama mzazi,
au mlezi mwenye
mamlaka kutembelea eneo
alilohifadhiwa mtoto kwa
ajili ya kuonana
na mtoto huyo.
Haijalishi
anaumwa au yu
mzima, yuko kituo
cha kulelea watoto au
nyumbani kwa mtu, na
hali nyingine au
mazingira yoyote atayokuwemo. Pia kumuona mtoto
si tu kumuonesha
mtu kuwa mtoto
ni yule halafu
basi. Bali kumuona mtoto
kunajumuisha kumuona na
kumgusa kimwili.
2. JE
NI MTOTO WA
UMRI GANI ANAYEONGELEWA
HAPA.
Kifungu cha 4 cha Sheria ya mtoto kinajibu
swali hili. Kifungu
kinasema kuwa mtu
mwenye umri wa chini ya
miaka 18 ataitwa
mtoto . Kwa hiyo tunapoongelea kumuona
mtoto tunamaanisha mtu
ambaye umri wake
uko chini ya
miaka 18 yaani
kuanzia miaka 17
kushuka chini. Mwenye
miaka 18 kamili
si mtoto kwa
maana ya kifungu
hiki.
3. HAKI
YA KUMUONA MTOTO
HII HAPA.
Kifungu cha 38 cha
sheria ya mtoto
kinatoa haki kwa
mzazi au mlezi
ambaye hakai na
mtoto kuwa na
uwezo wa kumuona
mtoto. Haki hii ipo
kisheria na mzazi
au mlezi anayekaa
na mtoto hapaswi
kumnyima mzazi mwenzake
au mlezi mwingine haki
ya kumuona mtoto
huyo.
Suala la msingi
ni kuwa kumuona
kwako mtoto kusiwe
na lengo lolote
la kumdhuru au
kumfanyia jambo lolote lililo
kinyume na haki
za mtoto pamoja
na haki za
binadamu kwa ujumla
wake. Nje ya
haya haki yako
ya kumuona mtoto
iko palepale.
Usinyimwe haki hii
kama wewe ni
baba na mama ndiye anayekaa
na mtoto na usinyimwe
haki hii kama
wewe ni mama
na baba ndiye
anayekaa na mtoto
halikadhalika mlezi.
4. NINI UFANYE
UKINYIMWA HAKI
YA KUMUONA MTOTO.
Kifungu cha 38
cha Sheria ya
mtoto kinasema kwamba
unatakiwa kwenda mahakamani
kufungua malalamiko kwa
ajili ya kupewa
haki hiyo. Wewe
utakua mlalamikaji na
na mzazi au mlezi aliyekunyima
haki hiyo atakuwa
mlalamikiwa.
Sehemu nzuri
ya kufungua malalamiko
ya aina hii ni
mahakama ya mwanzo
iliyo ndani ya
eneo alilomo mtoto.
Sio eneo unaloishi
wewe bali eneo ambako
mtoto analelewa na kuishi. Pia waweza kufungua
lakamiko hili hata mahakama
ya wilaya iliyo katika
wilaya anakolelewa na
kuishi mtoto.
Mwisho sababu zinazotolewa
na wale wanaonyima
haki hii kwa mfano
ati hujawahi kuleta
matumizi, ati ulimtelekeza mtoto
miaka mingi, nk hazina mashiko
kumnyima mzazi haki
hii.
Ikiwa kuna
mtu analalamikia sababu hizo
basi naye anayo
haki ya kuyalalamikia
hayo mahakamani lakini
sio kumnyima mzazi
mwenzake au mlezi
haki ya kumuona
mtoto.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
Je ni kila baada ya MDA gani mzazi asiekaa na mtoto ataruhusiwa kumuona mtoto???
Naomba hiki swali lijibiwe