NA BASHIR YAKUB -
Matunzo ya mke
kutoka kwa mme
ni jambo la
lazima. Kwa maana
kuwa ni lazima
mme kutoa mahitaji
kwa mke wake .Hakuna uhiari katika
hili. Ni lazima na neno
lazima
maana yake inajulikana.
Ifahamike kuwa matunzo
anayotoa mme kwa
mke wake si msaada, si
hisani, si upendeleo, si
zawadi bali ni
wajibu.
Matunzo yenyewe ni
kama chakula , sehemu
ya kulala na
kuishi, mavazi, matibabu na
kila kitu ambacho
ni muhimu kwa
mahitaji ya mke
husika. Kifungu cha 63(a)
cha Sheria ya
ndoa kinasema kuwa
ni wajibu na
lazima kwa mume
kumtolea matunzo mke
wake.
1.VIPI MUME AKISHINDWA KUTOA
MATUMIZI.
Yapo mambo ambayo
mke anaweza kuyafanya
ikiwa mme wake
atashindwa kumtolea matumizi .
Mojawapo ni hili
la kuruhusiwa kuuza
mali ya mme
wake bila ridhaa
ya mme huyo.
Tutaona likoje hili
baadae. Mengine ambayo
anaweza kufanya mke
ikiwa amenyimwa matumizi
ni pamoja na
kufungua shauri mahakamani
kudai matumizi, na hata kudai talaka
ikiwa hali hiyo
imekuwa sugu.
2. KUUZWA
KWA MALI YA
MME.
Kwa ujumla kifungu
cha 64( 1 ) cha Sheria ya ndoa
kinasema kuwa mke
ataruhusiwa kuuza mali
ambayo kimsingi inamilikiwa na
mme wake kwa
ajili ya kujipatia
matunzo au mahitaji
muhimu ya kwake
na/au ya watoto/mtoto
wake.
Kuhusu ni kipi
kinaweza kuuzwa, wakati
gani kiuzwe, kwa masharti
yapi tutaona hapa
chini.
3. MASHARTI
KABLA MKE
HAJAUZA.
( a ) Kwanza ambaye
anaruhusiwa kuuza ni
lazima awe mke
halali wa mme huyo.
Kimada( concubine) hawezi
kuuza mali ya
mwenzake. Ni mke
wa ndoa tu
ndiye anayeruhusiwa. Yaweza kuwa
ndoa ya kidini, ya kimila, ya
serikali au ile
inayotokana na kuishi wote
miaka miwili.
( b ) Ni
lazima iwe mke
amenyimwa matumizi muhimu. Ikiwa
hajanyimwa matumizi hawezi
kuwa na mamlaka
ya kuuza mali
ya mme wake.
( c ) Pia
ikiwa ana watoto/mtoto
na hawana matumizi
basi napo anaweza
kuuza mali ya
mme wake.
( d ) Huwezi kuuza
mali ya mme wako kwa
ajili ya kujipatia
matumizi ya anasa.
Matumizi yatakayokupelekea kuuza mali ya
mme ni yale
ya lazima.
4. JE
NI MALI YOYOTE
INAYOWEZA KUUZWA ? .
Hapana si mali
yoyote inayoweza kuuzwa. Kifungu cha 64
( 1 ) kinasema kuwa mali
ambayo inaweza kuuzwa
ni ile mali
inayohamishika. Mali inayohamishika ni
kama gari, pikipiki,
mali duka, samani
na vifaa vya ndani
nk. Kwa maana
hii hutaweza kuuza
ardhi katika mustakabali
huu. Ardhi ni nyumba,
kiwanja na shamba.
Aidha mamlaka hayaishii
katika kuuza tu
bali hata kubadilishana. Unaruhusiwa
kufanya utaratibu wowote
wa kubadilishana ambao utaona kwamba
unaweza kukupatia hela
ya mahitaji yako .
5. NI
WAKATI GANI UNAWEZA
KUUZA MALI YA
MME WAKO.
Kifungu cha 64( 2) cha
sheria ya ndoa
kinasema kuwa ni wakati ambao
unaishi na mme wako
katika nyumba moja au
chini ya paa
moja lakini akawa
hatoi matumizi yako au ya
mtoto.
Pili ni wakati ule ambao mme
amekutelekeza na kwenda kuishi
kwingine kunakojulikana au
kusikojulikana.
Na tatu ni
wakati ambao mmetengana
kwa makubaliano maalum
kuwa mme atakuwa akikupatia
matumizi lakini baadae
akawa hafanyi hivyo.
Kwa ufupi huo
ndio msimamo wa
sheria katika hilo.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment