NA BASHIR YAKUB -
Ni kipindi muhimu
kujua kuhusu hisa. Hivi
karibuni utakuwa umesikia
makampuni mbalimbali hasa
yale ya simu
yakiwatangazia watu kununua
hisa. Ni muhimu kwako
kujua kuhusu biashara
hii. Huenda ikawa
ya faida kwako
au eneo zuri kwako kwa kuwekeza.
Mapema niseme kuwa
usiogope wala usiwe mwenye hofu. Biashara ya
hisa ni ya
watu wote tajiri au
maskini. Laki moja,
laki mbili nk. unaweza
kununua hisa. Ili umiliki
hisa kwenye kampuni ya simu
si lazima umiliki
mamilioni kama unavyodhani.
Na hapa ndipo
tunapokosea na kuwaacha matajiri
watambe nasi tubaki
kulalamika.
1.HISA NININI.
Hisa ni mali
kama zilivyo mali
nyingine unazomiliki.
Tofauti ya hisa
na mali nyingine ulizonazo kama shamba, gari,
nyumba nk.ni kuwa
mali nyingine huweza
kushikika au kuonekana
kwa macho wakati
hisa ni mali
isiyoonekana kwa macho.
Yumkini zote ni
mali tu.
Hisa ni maslahi
au haki fulani
unayokuwa nayo katika taasisi au
kampuni fulani. Ndiyo
maana ni mali
isiyoonekana kwasababu huwezi
kuona maslahi au
haki kwa macho.
2. KUMILIKI
HISA KATIKA KAMPUNI.
Kampuni yoyote unayoiona huwa inao
wanahisa. Wanahisa ndio
wamiliki wa kampuni.
Kwahiyo hata wewe
ukinunua hisa kwenye
kampuni yoyote na
wewe unakuwa mmoja
wa wamiliki.
Haijalishi ukubwa wa kampuni
na kiwango chako cha
hisa ulichonunua bali ni
kuwa ukishanunua tu
hapohapo na wewe
unakuwa mmoja wa wamiliki. Hata hisa za laki
moja nazo zinakufanya kuwa mmoja
wa wamiliki.
Kiwango cha hisa zako
ndicho kiwango cha umiliki wako.
Kampuni ikiwa na
hisa 100,000 na wewe
ukamiliki hisa 50,000 basi
wewe unaimiliki nusu
ya kampuni. Ukimiliki
hisa 25,000 basi
wewe unamiliki robo
ya kampuni. Halikadhalika
ukimiliki hisa 500,
100, 50, 10, 5
au hata hisa
3 basi hichohicho
kiwango chako cha hisa
ulichonunua ndicho kiwango
chako cha umiliki wa kampuni husika.
Kwahiyo ukinunua hisa
100 Vodacom basi
wewe utaimiliki Vodacom
kwa kiwango cha hisa hizo
ulizonunua. Isipokuwa ni muhimu
kujua kuwa anayemiliki
hisa nyingi kuliko wote ndiye hujulikana
kama mmiliki mkuu
wa kampuni.
3. JE
UTAFAIDIKAJE NA HISA.
Kila mwanahisa hupata
gawio la faida
pale kampuni inapotangaza
faida. Kampuni hutangaza
faida kila baada
ya mwaka au
nusu mwaka au vinginevyo.
Utapata mgao
kwa asilimia kutokana
na kiwango chako
cha hisa ulizonazo. Ukiwa na
hisa nyingi utapata mgao
mkubwa, ukiwa na hisa kidogo
utapata mgao mdogo
na vivyo hivyo.
4. HISA
HUPATIKANA VIPI.
Kampuni husika hutangaza
kuuza hisa zake pamoja
na bei
ya kila hisa. Bei
ya hisa moja
inaweza kuwa Tshs 1,000/=, 10,000/= nk. Lakini
pia kampuni nyingi
huweka kima cha
chini cha hisa
unazotakiwa kununua, mfano kampuni
itasema tunauza hisa kuanzia hisa
100 au 50 na
si chini ya
hapo nk.
Kwahiyo wewe utafuata sharti
hilo na mengine
yatakayokuwa yamewekwa na
utanunua hisa unazotaka.
5. JE
UKINUNUA HISA UNAPEWA
NINI.
Ukinunua hisa unapewa
cheti cha umiliki wa
hisa. Cheti cha
umiliki wa hisa
ndicho ushahidi kuwa
wewe unamiliki hisa
katika kampuni fulani. Cheti hicho
kama hisa zote
ulizochukua umezilipia vizuri
na hudaiwi unaweza
kukitumia kukopea hela
katika mabenki, kama
dhamana mahakamani nk.
Cheti cha umiliki
wa hisa ni
sawa ni sawa
na hati ya
nyumba/kiwanja, au kadi
ya gari na vyombo vingine.
Hati hizi zinavyoweza
kutumika ndivyo na
cheti cha umilki
wa hisa kinavyoweza kutumika.
6. JE
UNAWEZA KUUZA HISA
BAADA YA KUNUNUA.
Ndio, hisa ni bidhaa kama
bidhaa nyingine. Unaweza
kununua hisa leo na kesho
ukiwa na shida
ya hela ukauza.
Katika makampuni ya
umma ( PLC) kama haya ya
simu unaruhusiwa kumuuzia yeyote
utakayemuona amefika bei.
Ni kiasi gani
uuze hakuna anayekupangia. Ni
biashara kama biashara
nyingine yoyote. Unaweza
kuwa umenunua hisa
kwa tshs 1,000,000/= lakini
ukauza hata 5,000,000/=.
Ni wewe tu na
mteja wako. Na
unaruhusiwa hata kumtumia dalali
kukutafutia mteja.
Lakini pia unaweza
kuamua kuuza baadhi ukamaliza
shida yako na
ukabakiza baadhi. Si
lazima kuuza zote.
Hayo ni kwa
uchache tu kuhusu
hisa.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment