NA BASHIR YAKUB -
Ndio ni kweli
mwanamke aliyeolewa anaweza
kukopa hela kwa
jina la mme
wake. Tena kukopa
kwenyewe si lazima
awe amepata ridhaa
au ruhusa kutoka
kwa mme wake.
Pia si ruhusa tu
bali si lazima
amtaarifu mme huyo. Sheria
ya ndoa , sura
ya 20 iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2010
ndiyo iliyoeleza jambo hili . Lipo kifungu cha
64 cha sheria
hiyo.
Kwa ujumla makala
haya yatatizama jambo
hili likoje, linahusisha nini na
nini, vigezo na sifa
za kufanya hivyo na
mambo mengine ambayo
yanalizunguka jambo hili
lakini kwa ufupi.
1.MWANAMKE GANI
ANAWEZA KUKOPA.
Kifungu hicho kimesema mwanamke anayeweza
kukopa ni yule aliye
kwenye ndoa inayotambulika kisheria.
Ikiwa mwanamke hayupo katika
ndoa ambayo sheria inaitambua basi
haki hii ya
kukopa kwa jina
la mme wake
anaikosa.
Ikiwa mmetengana lakini
ndoa haijavunjika kisheria
basi haki hii inaendelea kubaki.
Isipokuwa tu itaondoka ikiwa
mmetengana kwa makubaliano maalum
ambapo matunzo na
matumizi yote mwanamke
anapata bila wasiwasi.
Pia ikiwa kuna
talaka basi mwanamke
hawezi kukopa kwa
jina la mme
wake kwa kuwa
talaka kisheria inavunja
ndoa na hivyo
tafsiri yake ni kuwa
hakuna ndoa. Lakini
kukiwa na shauri
la talaka mahakamani
na ndoa haijavunjwa
rasmi na mahakama
basi haki hii
inaendelea kubaki kwa
mwanamke huyo.
2. KWANINI SHERIA
IMEMRUHUSU MWANAMKE KUKOPA
KWA JINA LA MME .
Sheria imemruhusu mwanamke
kukopa kwa jina
la mme wake tena
bila hata ridhaa
ya mme wake
kwakuwa imempa wajibu
mume kumtunza mke
wake na mtoto/watoto
kama yupo. Kwa
mujibu wa sheria
ya ndoa ni
lazima mume kumtunza
mke wake pamoja
na watoto kama wapo.
Kwa upande mwingine
mwanamke naye anaruhusiwa
kumtunza mme wake
lakini kwake sio
lazima. Sheria haijampa ulazima
mwanamke bali mwanaume . Kwahiyo
ni katika mazingira
haya ambapo suala la
mke kukopa bila
ridhaa ya mme
wake tena kwa
jina la mme
huyo linapokuja.
Hata hivyo sio
wakati wote mwanamke
anaruhusiwa kukopa kwa
njia hiyo bali
ni pale tu mume
wake anapokaidi wajibu
wake wa lazima
wa kumpa matunzo/matumizi. Hapa
ndipo mwanamke anaweza
kukopa kwa jina
la mme wake tena
bila hata ridhaa ya
mme huyo.
Mke hataruhusiwa
tu kufanya hivyo kwa
kutopewa
mahitaji yake pekee
bali pia hata kama ana
watoto/mtoto nao hawajapewa
mahitaji basi hata
hapo anaruhusiwa kukopa.
3. JE ANAWEZA
KUWEKA REHANI MALI
YA MME WAKE
ILI KUJIPATIA MKOPO.
Ndio kama kuna
mali ya mme
basi mke anaruhusiwa
kuiweka rehani bila
ridhaa ya mme ili kujipatia
mkopo. Hapa anaweza kuiweka
rehani kwa jina
la mme au
lake mwenyewe ilihali
suala la msingi
ni kujipatia mkopo kwa
ajili ya kupata
mahitaji yake au
ya watoto.
Pamoja na hayo
yote ni muhimu
kujua kuwa mke
hataruhusiwa kuweka rehani au kukopa
kwa jina la mme
wake kwa mambo
mengine ambayo yapo nje
ya kujipatia mahitaji
ya matunzo yake au ya mtoto.
Pili hataruhusiwa kuweka
ardhi rehani. Ni
mali zinazohamishika tu
ndizo zinazoruhusiwa.
Tatu anaruhusiwa
kukopa tu pale anapokuwa
amenyimwa mahitaji/matumizi.
4. JE
MWANAUME ANAWEZA KUKOPA
KWA JINA LA MWANAUME.
Sheria hii ya
ndoa iko kimya
kuhusu hilo. Haijaeleza
ikiwa anaweza au
hawezi. Hata hivyo
tafsiri ya jambo
lolote ambalo halikuelezwa
na sheria maana
yake ni kuwa
halipo.
Pamoja na
hayo ikiwa jambo hili
litawezekana basi itakuwa ni kwa
makubaliano maalum kati
yak e mme huyo na mke
wake na halitaingia
katika masuala ya
sheria za ndoa
bali makubaliano ya kimkataba kama
ilivyo katika mikataba mingine
ya kawaida.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment