NA BASHIR YAKUB -
Yapo mambo unayotakiwa
kufanya mara tu
baada ya kusajili
kampuni. Tunazungumzia yale
utakayoyafanya ule mda baada
ya kuwa umepewa
cheti cha kuzaliwa
kwa kampuni( certificate of
incorporation) kutoka BRELA. Mambo
haya ni ya
kisheria na kutoyafanya
kwake kunahesabika ni
kuvunja sheria.
Kwahiyo mambo haya
ni lazima na
sio hiari.
Hata hivyo kabla
ya kueleza hayo ni
muhimu tukajikumbusha kuhusu taratibu
za kusajili kampuni. Tunasema
kujikumbusha kwakuwa makala kuhusu
taratibu nanamna
ya kusajili/kuunda kampuni
hatua kwa
hatua yalishaandikwa
hapo awali.
Haya
yote yatakuwa yakitoka
Sheria ya Makampuni ,Namba 12 ya
mwaka 2002.
1.HATUA ZA
KUSAJILI/KUUNDA KAMPUNI.
( a ) Kwanza hakikisha
unajua unahitaji kufanya
biashara gani. Hii
ni kwasababu katika
vitabu vya kampuni
lazima uandike biashara
unayotaka kufanya au
unayofanya tayari.
( b ) Hakikisha mko
wawili au zaidi.
Hakuna kampuni ya mtu
mmoja. Kampuni binafsi
huanzia watu wawili
na mwisho ni watu
50. Unaweza kuwa wewe na mke
wako, rafiki, ndugu,
mzazi, mtoto nk.
( c ) Fahamu kampuni
yenu inatakiwa kuwa na
hisa ngapi na kila hisa
itakuwa inauzwa bei
gani. Pia unatakiwa kujua
kampuni itakuwa na
mtaji wa shilingi
ngapi. Kwa mfano kampuni
itakuwa na hisa
10000, bei ya kila
hisa ni Tshs 1000 ambapo, hisa x bei
ya hisa = mtaji wa
kampuni, kwa maana ya
10000 x 1000 = 10000000
ambao ndio mtaji
wa kampuni.
( d )
Andaa jina ambalo
ungependa kampuni yako iitwe.
Jina lolote linakubalika
isipokuwa lisiwe tayari
linatumiwa na kampuni
nyingine au lisiwe
kwa namna moja
au nyingine lina
viashiria vya matusi au
lugha isiyostahiki.
( e ) Peleka maombi
BRELA kuhusu jina
ulilochagua kwa uhakiki.
Uhakiki wanaangalia kama
linatumiwa na kampuni
nyingine tayari au
linavyo viashiria vya lugha
isiyostahiki. Siku hizi
uhakiki hufanyika kupitia
mtandao( online search/name clearance).
( f ) Baada ya
kuwa jina limepitishwa
basi utatakiwa kuandaa waraka
na katiba ya kampuni(
memorundum & article of association)
ikiwa ni pamoja
na kujaza fomu ambavyo
kwa
pamoja vitapelekwa BRELA kwa
usajili.
2. BAADA YA KUSAJILI FANYA
HAYA.
( a ) Hakikisha unapata namba
ya mlipa kodi
pamoja na leseni
ya biashara kabla
hujaanza kufanya biashara.
( b ) Kama
kampuni yako ni
binafsi ( private limited)
hakikisha nyaraka zote
za kampuni kama barua,
mikataba , bango la nje nk. unaweka
neno LIMITED baada ya
jina la kampuni,
mfano KIKWE COMPANY LIMITED. Na
kama ni ya
umma( public limited) andika
neno PLC ( Public Limited
Company) baada ya jina. Kutoweka neno limited au PLC ni
kosa kwa mujibu
kifungu cha 34 cha sheria
ya Makampuni.
( c ) Hakikisha unaweka
bango lenye jina
la kampuni nje
ya ofisi. Kifungu cha
112 cha Sheria
ya Makampuni kimeweka
ulazima katika hilo.
( d ) Hakikisha kila
mwaka kampuni inafanya
mkutano mmoja wa
jumla( annual general meeting).
Hii ni kwa
mujibu wa kifungu
cha 133 cha Sheria
ya Makampuni. Mkutano
huu ni wa
lazima.
( e ) Kujaza fomu
ya hisa kwa
kila aliyechukua hisa
za kampuni ndani
ya siku 60. Hili
linakwenda sambamba na
kutoa cheti cha umiliki wa
hisa ( share certificate) kwa
kila aliyechukua hisa
na kuzilipia.
( f ) Mwisho hakikisha
unafanya mrejesho wa
kila mwaka ( annual return)
kwa mujibu wa kifungu
cha 128 cha
Sheria ya Makampuni. Hii ni
fomu maalum ambayo
hujazwa na kupelekwa
BRELA kila mwaka. Hueleza hali ya kampuni
ikoje kwa mwaka
mzima hasa kuhusu
ofisi ilipo , wanahisa,
hisa, wakurugenzi, nk. Lengo ni kutaka kujua
ikiwa kuna mabadiliko
yoyote katika hayo au lah.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment