NA BASHIR YAKUB -
Kwa mujibu wa
sheria ya usajili wa
ardhi sura ya 334
ipo aina ya
mikataba ya pango
ambayo baada ya
kuwa imeingiwa kati
ya mpangaji na mwenye nyumba/eneo
ni lazima isajiliwe.
Mikataba ya aina
hiyo isiposajiliwa inakuwa
haijakidhi vigezo vya
kisheria na hivyo
kubatilika.
Aidha pango huhusisha
shughuli mbalimbali. Yapo
mapango kwa ajili
ya biashara maduka,
bar, mahoteli n.k. na pia
yapo mapango kwa
ajili ya makazi. Iwe
umepanga kwa ajili ya biashara
au makazi madhali
aina yako ya
upangaji inahitaji kusajiliwa
kisheria basi huna budi
kufanya hivyo ili
uhalali wa pango lako
upatikane.
Kabla ya kuona aina ya mikataba ya
pango ambayo ni lazima
kusajiliwa ni vyema
kujikumbusha kidogo kuhusu
haki za mpangaji.
1.HAKI ZA
MPANGAJI.
( a ) Haki
ya kutoingiliwa na
mwenye nyumba ili kumpa uhuru mpangaji kufurahia pango
lake.
( b ) Haki
ya kumpa taarifa(notice) mapema
mpangaji ikiwa mwenye nyumba anataka
kukagua nyumba/eneo lake.
( c ) Haki
ya kutoondolewa au
kusitishiwa mkataba mpaka
baada ya kupewa taarifa
maalum( notice) .
( d ) Haki
ya kuambiwa ukweli
kuhusu hali ya
nyumba kabla ya kusaini
mkataba wa pango. Mfano
kuambiwa ikiwa eneo
linajaa maji kipindi
cha mvua, kuambiwa ikiwa
nyumba inavuja n.k.
( e ) Haki
ya kukataa sharti
lolote ambalo linalenga kuminya uhuru
wa mpangaji au
linalovunja sheria yoyote
ya Tanzania.
( f ) Haki
ya kupewa taarifa
mapema(notice) kabla ya
kupandisha kodi ya
pango.
( g )
Haki ya kupewa
taarifa mapema(notice) kabla
ya kubadilisha sharti
lolote katika mkataba
wa pango.
Haki ni nyingi
hizi ni baadhi
tu.
2. MKATABA
WA PANGO AMBAO
NI LAZIMA KUSAJILIWA.
Kifungu cha 54 ( 1 )
cha Sheria ya
Usajili wa Ardhi ,
Sura ya 334 kinasema
kuwa pango ambalo
mkataba wake unazidi
miaka mitano linatakiwa
kusajiliwa.
Wapo watu wanapanga
mahoteli, bar, maduka nk. ambao miaka ya
pango katika makubaliano yao ni zaidi
ya mitano. Hawa
mikataba yao ni
lazima isajiliwe.
Mara
nyingi mkataba wa
pango huweza kuwa
wa miaka mingi
kutokana na aina
ya biashara anayotaka
kufanya mpangaji
halikadhalika uwekezaji anaotarajia
kufanya eneo analotegemea
kupanga. Wakati mwingine
mpangaji hukubaliana na
mwenye eneo kufanya
marekebisho makubwa ( renovation)
ili enepo lifanane
na aina ya biashara
anayotaka kufanya.
Mbali na hayo ni
vema kufahamu pia
kuwa mkataba ambao
ni chini ya
miaka mitano lakini mkataba huo
una sharti la
kuhuisha( renew) kwa miaka
mingine, ambapo ukijumlisha
miaka ya awali
na hiyo ya
kurenew jumla inazidi
mitano basi nayo
ni lazima kusajiliwa.
Tumeongelea
mikataba inayozidi mikaka
mitano lakini hatupaswi
kusahau kuwa hata
mikataba ya pango
iliyo chini ya miaka mitano inaweza
kusajiliwa japo sio lazima.
Mikataba hii una
chaguo kusajili au
kutosajili. Kisheria
kutosajiliwa kwake kwa namna
yoyote hakuathiri uhalali
wake.
4. WAPI
UKASAJILI.
Msajili wa nyaraka
anayepatikana ofisi za
ardhi ndiye anayehusika
na usajili wa
mikataba hii. Unapofika ofisi
yoyote ya ardhi
utapewa maelekezo lipi
la kufanya ili
mkataba wako uweze
kusajiliwa.
Aidha ipo ada ya
kulipa kabla ya
usajili ikiwemo kodi
ya faida.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
Haya ni maelekezo elekevu!