NA BASHIR YAKUB -
Zipo namna nyingi
za kuachana kisheria
kwa wanandoa ambao
wanadhani sasa hawawezi kuendelea. Wengi wetu
tunajua zile za kupitia
mahakamani. Zile ni sahihi lakini
upo uwezekano pia wa
kuachana kwa mkataba
maalum bila kuhitaji
kwenda mahakamani.
Aidha yafaa ifahamike
kuwa Kuachana katika
ndoa na kuamua
kuishi nje ya
ndoa ni jambo
la kawaida. Kisheria si
dhambi mwanandoa yeyote
kuona kuwa sasa
hawezi kuendelea kuwa katika ndoa. Ni
kwasababu hii hata
sheria ikatambua uwezekano
wa watu kuachana
na halikadhalika ikaweka
utaratibu maalum kwa walio
tayari kwa hilo.
Tofauti na kuachana kwa
mkataba namna nyingine
ni kwa njia
ya talaka mahakamani
na kwa njia ya kutengana
mahakamani ambazo nazo tutaziona hapa
chini kabla ya kutizama
ile ya mkataba.
1.KUACHANA KWA TALAKA.
Kifungu cha 99
cha Sheria ya
ndoa kinaongelea talaka.
Maombi ya talaka
hupelekwa na yule anayedhani hawezi
kuendelea na ndoa kutokana
na sababu anazoamini
kuwa ndoa hiyo haiwezi kuendelea.
Mahakama huzisikiliza pande
zote mbili na
kuja na maamuzi.
Kifungu cha 107( 2 )
cha sheria ya
ndoa kinazitaja sababu
ambazo zote au
mojawapo ikithibitishwa ni
ushahidi kuwa ndoa
hiyo haiwezi kuendelea.
Baadhi ni ukatili, zinaa, kutelekeza, kifungo cha maisha au
kifungo kisichopungua miaka mitano, na
nyingine nyingi.
Talaka huombwa mahakamani
na hivyo maombi yake hupelekwa mahakamani.
2. KUTENGANA MAHAKAMANI BILA TALAKA.
Hatua hii ni
kwa mujibu wa kifungu
cha 99 cha
sheria ya ndoa.
Mnatengana kwa muda fulani
lakini
bila talaka. Talaka ni
kutengana milele wakati
hii ni kutengana
kwa muda. Njia
hii nayo muombaji
hutakiwa kwenda mahakamani
na kufungua maombi.
Wahusika wote wataitwa
na kila mmoja
atajieleza na baadae mahakama
itatoa maamuzi. Njia
hizi zote mbili mwombaji hutakiwa
kupitia mahakamani isipokuwa
hii ya mkataba
ambayo itaelezwa hapa
chini.
3. KUACHANA KWA
MKATABA MAALUM.
Kifungu cha
67 cha sheria
ya ndoa kinasema
kuwa wanandoa wanaweza
kwa njia ya
maandishi ambayo yatakuwa
yamesainiwa na wote
wawili kuamua kuishi tofauti/nje
ya ndoa. Kwahiyo
utaona hapa kuwa
unachotakiwa kufanya ni
kukubaliana na mwanandoa
mwenzako kwamba sasa
naona mambo hayaendi
na hivyo ni bora
kila mtu aishi
maisha yake.
Akikubali basi mtakaa
chini mtaandikishana kisheria
kabisa na kila
mtu ataendelea na
maisha yake. Isipokuwa
ni lazima mnapoamua kutumia njia
hii hakikisha katika maandiko
yenu viwemo vipengele vinavyohusu
matunzo ya watoto/mtoto
kwa maslahi mapana
kabisa, muafaka na
hatima kuhusu mali
mlizonazo, pia matunzo
au vinginevyo kwa
mmoja kati ya
wanandoa kama hilo litakuwa
ni la lazima.
Kwahiyo haya ni
maandiko na ni
mkataba sawa na
mikataba mingine ya
kisheria. Faida ya
njia hii ni kuwa
ni nyepesi, haitumii mda
mwingi, haina gharama kubwa na inatekelezeka
kwa urahisi.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment