NA BASHIR YAKUB -
Je nani anawajibu
wa kumtunza mwenzake
kati ya wanandoa. Je
ni mme, je
ni mke au
ni wote . Sheria
inasemaje kuhusu hili. Kwa
kuanza tu ni
kuwa suala matunzo
kwa wanandoa ni
la kisheria. Matunzo sio
hisani,zawadi au upendeleo
maalum bali ni
wajibu uliozaliwa na
sheria.
Sheria ya
Ndoa iliyofanyiwa marekebisho
mwaka 2010 , sura
ya 29 imeweka bayana
habari nzima ya
matunzo baina ya
wanandoa. Niseme mapema tu
kuwa wapo wanaojua kuwa mme
peke yake ndiye mwenye
wajibu wa kutoa
matunzo kwa mke. Tutaona
hili likoje .
Kabla ya hayo
ni vema tukaona
matunzo yanajumuisha nini
na nini kwa
mujibu wa sheria
hii.
1.MATUNZO NI
YAPI.
Kifungu cha 63( a )
cha sheria ya ndoa kinataja
vitu ambavyo kisheria
ndivyo vitakavyoitwa matunzo
kwa mwanandoa. Kifungu kinataja makazi(accommodation), mavazi, na chakula. Haya
ndiyo ya msingi
ambayo mwenye
wajibu wa kuyatoa
atatakiwa kutoa.
2. MKE KUTOA
MATUNZO KWA MME.
Ni vema
kujua kuwa suala la
matunzo linawahusu wanandoa
wote yaani mke
pamoja na mme.
Kila mmoja anao wajibu
kwa mwenzake katika
kutoa matunzo. Isipokuwa
wajibu huu umetofautiana kati
ya hawa wawili .
Mke ana wajibu
wenye mipaka katika
kutoa matunzo halikadhalika mme.
Kifungu cha 63( b ) cha
sheria ya ndoa kinasema kuwa
mwanamke ambaye ana
uwezo anawajibu wa
kutoa matunzo kwa
mme wake ambaye hajiwezi, ambaye ana
ugonjwa wa kimwili
au kiakili ambao
haumuwezeshi kufanya kazi
ya kumuingizia kipato.
Kifungu kiko wazi
kuwa wajibu wa
mwanamke kumhudumia mwanaume
ni pale tu
mwanaume huyo anapokuwa
mlemavu au mgonjwa
wa akili au
mwili. Lakini pia
ugonjwa huo au
ulemavu huo uwe
ni wa kiwango
cha kutomwezesha kufanya
kazi. Ikiwa ugonjwa au
ulemavu ni wa kiwango
cha kumwezesha kufanya
kazi atakuwa nje
ya muktadha wa
kifungu hiki.
Hii maana yake
ni kuwa ikiwa
mwanaume anajiweza si
mgonjwa au si mlemavu
au ni mgonjwa
au mlemavu lakini
ugonjwa au ulemavu
huo haumzuii kufanya
kazi ya kujiingizia
kipato basi mwanamke
au mke wake
hawajibiki kumtolea matunzo.
Mwanamke anawajibika kutoa
matunzo kwa mme
wake pale tu
ambapo mme huyo
hajiwezi kama ilivyoeleza
hapa juu. Kwahiyo hilo
lieleweke hivyo kuwa ikiwa mwanaume
hana tatizo la kumfanya asifanye
kazi ya kujiingizia
kipato hawezi kudai
matunzo kutoka kwa
mke wake. Ni wajibu
wenye mipaka.
3. MME
KUTOA MATUNZO YA
MKE.
Kifungu cha 63( a )
cha sheria ya ndoa
kinasema kuwa ni
wajibu wa mme
kumtunza mke wake
au wake zake
kwa kuwapa makazi, Mavazi na
chakula kutokana na
uwezo wake wa
kipato.
Kwa muktadha
wa kifungu hiki
utaona tofauti kati
ya wajibu wa
mwanamke kutoa matumizi
na ule wa
mwanaume. Kwa mwanaume
kutoa matumizi ni
mda wote. Iwe
mke wake ni mlemavu
au mgonjwa au
hata awe mzima
na unao uwezo
wa kufanya kazi
lakini hafanyi, ni lazima
mwanaume atatoa matumizi.
Isipokuwa jambo la
kuzingatia hapa ni
kuwa atatoa matumizi
kadri ya uwezo
wake wa kipato. Hatalazimishwa kutoa
zaidi kuliko kipato
chake na hatatakiwa kutoa
chini ya kile
kinachohitajika.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment