NA BASHIR YAKUB -
Una mahusiano na
mwanaume au mwanamke ambaye
kimsingi mpo katika
uchumba. Unampa zawadi
nyingi naye anakupa
zawadi. Mnayo ahadi ya
kufunga ndoa na
kuishi kama mme
na mke . Na
kwasababu hiyo unajitoa
sana kimatumizi kwa
mtu huyo.
Lakini katika
mazingira usiyoyaelewa unaona
sasa mambo hayaendi
vizuri. Hayaendi vizuri
katika kiwango ambacho
sasa mahusiano yamevunjika
kabisa. Hakuna tena
mahusiano. Au bado yapo
lakini kwa mambo
unayofanyiwa unaona kabisa
hutakiwi tena.
Kumbuka huko nyuma
umegharamia sana. Umegharamia
kwa fedha na
mali. Swali ni je
vitu hivi haviwezi
kurudishwa ?. Vitu hivi haviwezi kufidiwa ?.
Na je sheria imeongelea
kuhusu jambo hili ?.
Majibu ya maswali haya yote ni
ndiyo. Ni ndiyo,
na gharama pamoja nazo
zawadi zinaweza kurejeshwa. Unaweza kushangaa
kuona sheria imeongelea hata
mambo ya uchumba
lakini ndio ukweli.
Wengi tunaijua sheria
katika kuongelea wizi,
dhamana, mikataba, mirathi, ndoa,
na mengine. Lakini
ni vyema tukajua
kuwa sheria ni
pana na imeongelea
mambo mengi mno. Hili
la uchumba nalo
ni sehemu ya yaliyoongelewa.
1.KUVUNJA UCHUMBA.
Kifungu cha 69( 1 ) cha
Sheria ya Ndoa
iliyofanyiwa marekebisho 2010 kinasema kuwa mtu anaweza
kufungua shauri na
kudai fidia baada
ya uchumba kuvunjwa.
Kwa haraka utaona
kuwa tafsiri ya
kifungu hiki sio kufungua
shauri ili kumlazimisha mtu akurudie,
hapana. Mahakama haiwezi
kutoa maamuzi kuwa fulani
lazima
amrudie fulani. Isipokuwa
lengo lake ni
kumtaka yule aliyeumizwa
katika hili kudai
fidia kutokana na
maumivu aliyoyapata. Hapa hatujaongelea kurudisha
zawadi.
Kudai fidia na
kurudisha zawadi ni
vitu viwili tofauti. Fidia inahusu
kulipwa maumivu uliyoyapata
kutokana na tukio hilo la
kuachwa pamoja na
muda uliopoteza na
huyo mtu. Wakati zawadi
ni kurejesha kile
ulichotoa. Kwahiyo la zawadi
tutaliona baadae.
Aidha masharti ya kufungua
shauri la kudai
fidia ni kuwa ,
moja anayefungua shauri
awe ni yule aliyeumizwa,
pili ahadi ya kuoana
lazima iwe ilikuwa
imefanyika Tanzania, tatu wakati mnaingia kwenye
mahusiano iwe mlikuwa
nyote mmetimiza miaka 18 .
2. KURUDISHA ZAWADI.
Kifungu cha 71
cha Sheria ya
ndoa kinasema kuwa
mtu anayo haki
ya kufungua shauri
kudai kurejeshewa zawadi ambazo
alizitoa kwa mtu
ambaye alikuwa ana ahadi
ya kufunga naye
ndoa lakini ndoa
haikufungwa.
Zawadi ni pamoja
na fedha, nyumba,
magari, nguo na kila
kitu chenye thamani(valuable). Haijalishi
mali hiyo
ipo kwenye jina
la nani suala la
msingi ni kuthibitisha
kuwa wewe ndiye
uliyetoa hiyo zawadi.
Shauri la namna
hiyo unaweza kulifungua
mahakama yoyote ya
mwanzo, ya wilaya, ya hakimu
mkazi au hata mahakama
kuu. Itategemea na
thamani ya kiwango cha
mali unazodai.
Kama mali hizo
zitakuwa zimekwishatumika au
hazipo tena pengine
zimeuzwa au kutolewa
zawadi kwa mtu
mwingine basi itatakiwa
kulipwa fedha zinazolingana
na mali hizo
au mali hizo zikanunuliwe tena
kwingine ili kumrudishia
anayedai.
Ukishindwa kabisa
kurudisha basi mali zako binafsi
ambazo hazikuwa sehemu ya
zawadi zitauzwa ili
kupata kiwango kinachodaiwa
na kama huna
mali yoyote ya kuuza
utatakiwa kwenda jela
kama mfungwa wa madai.
Kwa hiyo watu
wanatakiwa waelewe kuwa
uchumba na ahadi za
kuoana si jambo
jepesi kama wanavyolitamka na kuliahidi .
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment