NA BASHIR YAKUB -
Kutelekezwa ni pamoja
na kunyimwa huduma
za muhimu ambazo
kama mke alistahili
kupata. Huduma muhimu ni
kama chakula, mavazi ,
makazi, matibabu, hela ya
kujikimu kwa matumizi
ya kawaida ya
mwanamke, pamoja na
kila hitaji ambalo
kama mwanamke alitakiwa
kulipata.
Ifahamike kuwa habari
ya kutelekeza inawahusu wote
mke na mme
kwa maana ya kuwa
mme anaweza kumtelekeza
mke halikadhalika mke
anaweza kumtelekeza mme. Hata
hivyo makala yatazungumzia mme
kumtelekeza mke ambapo sura
ya 29 , Sheria ya
ndoa iliyofanyiwa marekebisho
mwaka 2010 itarejewa.
1.AINA ZA KUTELEKEZA.
( a ) Aina
ya kwanza ni kutelekeza
ambako mume anaondoka
kabisa ndani ya
nyumba ambayo alikuwa
akiishi na mke
wake kama wanandoa na
kwenda kuishi kwingine. Haijalishi huko alikoenda panajulikana
ni wapi au hapajulikani
suala la msingi
ni kwamba hayupo
katika makazi yake
ya kawaida ya familia.
Aidha ikiwa hayupo
nyumbani lakini kwa
sababu za msingi
na za kisheria huko
sio kutelekeza. Sababu
hizo ni kama kuwa
jela, kuwa hospitali, kuwa amehamishiwa
sehemu nyingine kwasababu ya
matibabu kwa mfano
wengine huamishiwa mikoani, na pia kuwa
vitani labda baadae
mkapoteza mawasiliano na
mazingira mengine ya
dharula za kibinadamu na
ambayo siyo ya makusudi hayawezi
kuitwa kutelekeza.
( b ) Aina
nyngine ya kutelekeza ni
hatua ya kuwa mme na mke
wanaishi
wote katika nyumba
moja au chini
ya paa moja lakini mume
huyo hajishughulishi na
kutoa matumizi au
matunzo kwa mke
huyo kwa namna
yoyote ile. Hajui anakula
nini, hajui anavaa
nini, hajui anapata vipi
matibabu, kwa ufupi hajui
lolote zaidi ya
kumuona tu kama
binadamu wengine ambao
anawaona mitaani na
hana uhusiano nao.
Pia kuishi chini ya
paa moja lakini
vyumba tofauti nako
ni kutelekeza hata kama
mke anapewa matumizi
yote yanayostahili. Zaidi, hata
kulala chumba kimoja
lakini vitanda tofauti
kwa muda mrefu
tena kwa makusudi
kwasababu ya mgogoro
wowote nako ni kutelekeza. Lakini
pia kulala kitanda
kimoja bila kushiriki
tendo la ndoa kwa
makusudi kwa muda mrefu bila sababu za msingi za kiafya
au vinginevyo nako ni
kutelekeza.
2. NINI AFANYE
ALIYETELEKEZWA.
Kifungu cha 115( 1 )(
b ) cha sheria ya
ndoa kinasema kuwa mahakama
inayo mamlaka ya kumuagiza
au
kumuamrisha mwanaume kutoa
matunzo au matumizi
kwa mke wake.
Kwahiyo kumbe huna
haja ya kulalama
na kulia na
hali tayari sheria
inaweza kukusaidia katika
hili.
Unachotakiwa
kufanya ni kwenda
mahakamani na kufungua
malalamiko ambapo mme
huyo ataitwa na
atatakiwa kujibu kwanini
hatoi matunzo na
hapo baada ya
taratibu za kimahakama
maamuzi yatatolewa.
Kifungu cha 76
cha
sheria ya ndoa kinazitaja
mahakama ambazo unaweza
kutumia katika kufungua
malalamiko. Ipo mahakama
ya mwanzo, ya wilaya , ya
hakimu mkazi na mahakama
kuu.
Hata hivyo unashauriwa
kuanzia ustawi wa
jamii ambako taratibu zake
ni nyepesi na za
muda mfupi. Ustawi wa jamii
upo kila makao
makuu ya wilaya,
ukifika utauliza na utaoneshwa.
Ikishindikana hapo
sasa unaweza kwenda
mahakamani lakini pia
unashauriwa kutumia mahakama
ya mwanzo iliyo
katika eneo lako
au ya wilaya
iliyo katika wilaya
yako . Kwa kufanya hivi hakuna
shaka habari ya
kutelekezwa na kunyimwa
matumizi itakuwa imepatiwa
dawa sahihi.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment