NA BASHIR YAKUB -
Tumesikia mara kadhaa
wazazi wakigombania kukaa na mtoto/watoto. Haya hujitokeza
baada ya kuvunjika
kwa ndoa kwa
talaka, baada ya
kutengana bila talaka
au pasi na
ndoa wazazi tu
wamezaa na sasa
hawaelewani na mgogoro wa
nani akae na mtoto
umeibuka.
Tunahitaji kujua ikiwa
kuna haja ya
kugombania mtoto kwa matusi na
ugomvi wakati
zipo taratibu za
kisheria. Tujue kama yafaa kutumiana
jumbe chafu za
kudhalilishana pale unapotaka ukae
na mtoto. Jibu ni
hapana ila ni
watu tu wajue
taratibu.
Ifahamike kuwa iwe
kwa ndoa au
bila ndoa haki
ya mtoto kukaa
na wazazi au
mzazi iko
kwa yeyote. Ni aidha
atakaa na wote wawili au
mmoja wao. Sheria namba
21 ya 2009, Sheria ya
Mtoto ndiyo sheria
ambayo kwasasa inasimamia
ustawi na haki za mtoto.
Hivyo makala yataeleza
yaliyo katika sheria
hii.
1.MTOTO NI
NANI.
Kifungu cha 4( a )
cha sheria ya mtoto
kinatafsiri neno mtoto
kumaanisha mtu
ambaye yuko chini
ya umri wa miaka
18. Kwa maana hii miaka 18
kamili sio mtoto isipokuwa sasa
chini yake ndiye mtoto kwa
tafsiri ya kifungu
hiki.
Sambamba na hilo kifungu
cha 7( 1 ) kinaeleza haki
ya mtoto kukaa
na wazazi wake wote
wawili. Basi yaje
hayo ya kutengana
na mtoto kuishi
maisha ya mzazi mmoja , bado
uhalisia ni haki
ya msingi ya mtoto kukaa
na wazazi wake
wawili kama ilivyoainishwa hapa.
2. NAMNA
YA KUOMBA KUKAA
NA MTOTO.
( a ) UTAOMBA WAPI.
Utaomba
mahakamani. Swali la ni mahakama
ipi ina mamlaka
hayo au ni mahakama ipi
utakwenda kuomba linajibiwa na Kifungu cha 3
( a ) cha sheria
hiyo kinachozitaja mahakama
za mwanzo, za
wilaya, za hakimu
mkazi na mahakama
kuu kushughulika na
masuala hayo.
Lakini
ni vema zaidi ikiwa
utaitumia mahakama ya
mwanzo au ya wilaya
kwa hatua za
awali.
Hivyo basi hapo
ndipo utakapopeleka maombi
yako.
( b ) NANI ANARUHUSIWA
KUOMBA.
Kifungu cha 37 ( 1 ) cha
sheria hiyo kinasema yeyote
kati ya wazazi
wawili ambao wanagombania
mtoto anaweza kuomba.
Kila mmoja ana
haki na haki
ya mmoja haiondoi
haki ya mwingine.
Wapo wanaodhani haki ya mwanaume
ipo chini na
ya mwanamke ipo
juu katika hili,
si kweli. Haki ni
haki na kila
mmoja ana haki. Kwahiyo huna
haja ya kujihofia
kuwa pengine itakuwa hivi
au vile.
( c ) NI
KITU GANI UTAPELEKA
MAHAKAMANI.
Utapeleka maombi rasmi
ambayo yatakuwa yameandaliwa
kwa hoja za
kisheria huku yakiwa
yamesainiwa na muombaji .
Kawaida maombi hulipiwa
ada mahakamani japo
haiwezi kuzidi elfu
50.
Baada ya maombi kuwa
yamesajiliwa utatolewa wito
kwa ajili ya yule
unayegombea naye mtoto na
kesi itahesabika kuanza
rasmi.
( d ) ILI MAHAKAMA
IKUPE MTOTO UNATAKIWA
KUTHIBITISHA NINI NA NINI
?.
Kifungu cha 37( 4) na
kifungu cha 4 ( 2 ) kwa pamoja vimeongelea suala
la maslahi mapana
ya mtoto( best interest
of the child). Kwahiyo
ili mahakama iweze
kukupatia mtoto unatakiwa
kuonesha kuwa yule aliye
na mtoto hawezi
kumpatia mtoto huyo maslahi mapana
kama sheria inavyotaka na
badala yake wewe
unaweza.
Kutompatia maslahi
mapana ni pamoja na
mazingira mabovu anayoishi
mtoto huko aliko, uwezo
mdogo wa huduma
muhimu, tabia chafu za
aliye na mtoto, uchizi, ugonjwa wa
kuambukiza au ugonjwa
uliompotezea fahamu aliye
na mtoto, mazingira hatarishi
kama baa, dangulo, kumbi za
starehe, na mengine yote
ambayo kwa sura
yake hayajengi ustawi
bora wa mtoto.
Hivyo kuthibitisha
baadhi, yote au hata
moja kati ya
haya litaipelekea mahakama kuamua
ukae na mtoto.
Yako mengi kuhusu mada
hii lakini angalau
kwa ufahamu wa
jumla ni hayo.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment