NA BASHIR YAKUB -
1.MGAWANYO WA WOSIA.
Wosia umegawanyika mara
mbili . Upo wosia
wa maandishi na
upo wosia wa mdomo. Wosia hizi zote zinakubalika alimradi
zimekidhi vigezo vya
kisheria vinavyohitajika.
( a ) Wosia wa
maandishi . Ni wosia ambao
unakuwa umeandikwa. Unaandikwa na
mtoa wosia na
unashudiwa na mashahidi. Ni
wosia ambao unahimizwa
sana kwakuwa ni wa
kuaminika zaidi.
( b ) Wosia wa mdomo. Huu
ni wosia ambao
haukuandikwa isipokuwa aliyeutoa
alitamka tu kwa
maneno. Ni wosia unaokubalika
ikiwa utakidhi vigezo vya kisheria.
2. MASHAHIDI WANAOTAKIWA
KUSHUHUDIA WOSIA.
( a ) WOSIA WA KIKIRISTO.
Sheria
inayotumika kwa wosia
unaoandikwa na mtu
aliyeishi maisha haya inajulikana
kama “The Indian
Succession Act 1865”. Kwa
wakristo wanaoandika wosia ni
sharti kufuata misingi
ya sheria hii ili
wosia zao kuwa
halali.
Sheria hii imezigawa
wosia mara mbili.
Kwanza wosia wa
upendeleo( privileged will) ulio katika
kifungu cha 52 cha sheria
hiyo na wosia
usio wa upendeleo( unprivileged will) ulio kifungu cha 50.
Wosia wa upendeleo ni
wosia unaoruhusiwa kutolewa
na watu maalum
kwa mfano wanajeshi wanapokuwa
vitani na mabaharia
wanapokuwa baharini huko
bahari ya mbali .
Wosia usio wa upendeleo
unawahusu watu wa
kawaida wasio hao waliotajwa. Unaitwa wa
upendeleo kwasababu
wamepunguziwa masharti kutokana
na mazingira wanayokuwemo.
Kwa mujibu wa
kifungu cha 52 wosia
wa upendeleo ukiwa wa maandishi
sio lazima kuwa
na mashahidi au
kuwa na sahihi
ya mtoa wosia. Maandishi tu
yasiyo na mashahidi
yanakubalika na ndio
maana unaitwa wa
upendeleo.
Na kama ukiwa wa
mdomo basi mashahidi
wawili wanahitajika ili
ukubalike.
Kwa wosia Usio
wa upendeleo unaotumiwa na
watu wa kawaida mashahidi
wanaohitajika ni watu wawili
au zaidi kwa
mujibu wa kifungu
cha 50. Mtu mmoja
hakubaliki kuwa shahidi. Mashahidi hawa
hutakiwa kumshuhudia mtoa
wosia akisaini wosia.
( b ) WOSIA WA
KIMILA.
Huu ni kwa
wale walioishi maisha
ya kimila. Sheria inayoongoza
wosia huu inajulikana
kama “The Local
Customary Law ( Declaration)
Order 1963, GN No. 279/1963”.
Schedule ya 3 amri
ya
8 ya sheria
hii inasema wosia wa
mdomo unatakiwa kushuhudiwa
na mashahidi wasiopungua
wanne huku watu
wa ukoo wa
mtoa wosia wasipungue
wawili na watu
baki wasipungue wawili.
Amri ya 19 inasema
wosia wa kuandikwa
ushuhudiwe na mashahidi wasiopungua wawili wanaojua
kusoma na kuandika huku
mmoja akitoka ukoo
wa mtoa wosia na mmoja
mtu baki lakini
ikiwa tu mwenye kutoa wosia
anajua kusoma na
kuandika.
Ikiwa hajui kusoma
na kuandika basi
wasipungue wanne wawili wa ukoo
wake na wawili
watu baki.
( c ) WOSIA WA KIISLAMU.
Huu unahusisha wale
walioishi maisha ya
kiislamu. Unaongozwa na Qurani
tukufu, hadithi pamoja na
Sunna za mtume
Muhammad S.A.W. Pia “The
Islamic Law ( restatement) Act,
sura ya 375, G.N.No 222/1967” nayo
hutoa mwongozo.
Hapa wosia unaweza kuwa
wa mdomo au
maandishi pia. Uwezo na
uhuru wa kutoa wosia au kugawa mali upo katika
1/3 ya mali zako zote. Mashahidi wanaotakiwa
ni wawili na
kati ya hao
lazima awepo mwanaume
mtu mzima mmoja kutoka ukoo
wa mtoa wosia.
Angalizo ni kuwa
unapotoa wosia siku
zote hakikisha unafuata taratibu
za sheria inayokuhusu. Wosia wako
utakuwa batili ikiwa
utakuwa umekiuka misingi ya sheria
inayokuhusu. Mara zote kama
hujui hakikisha unapata
ushauri kwa wanaojua
ili kuepusha mgogoro kwenye
familia yako baadae. .
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment