NA BASHIR YAKUB -
Ni kweli ardhi umenunua
kwa hela yako, ni kweli kiwanja umetafuta
mwenyewe, ni kweli wewe ni Mtanzania
wala sio mgeni, lakini
pia ni kweli
ukubali kuwa ardhi
hiyo unaimiliki katika
kipindi maalum na
sio moja kwa
moja/milele.
Hapo ulipo
unapoita nyumbani kwako
unapamiliki kwa muda maalum
na sio
moja kwa moja
kama unavyodhani. Tanzania hakuna
anayemiliki ardhi moja
kwa moja bali
wote tunamiliki kwa
muda maalum.
Hati ya kumiliki
ardhi uliyonayo au unayotafuta
kupata hutolewa kwa
muda maalum. Hakuna hati ya milele
isipokuwa kila hati
inacho kipindi chake.
Kipindi
kinapoisha maana yake
na umiliki wako umeisha.
Tutaona ufanye
nini kipindi kinapoisha na athari za kuacha
kufanya ulichotakiwa kufanya baada
ya kipindi kuisha.
1.MUDA WA
HATI.
Kifungu cha 32( 1 )( a ) cha Sheria
ya ardhi sura
ya 113 kinasema
kuwa hati ya
kumiliki ardhi ardhi
inatolewa mpaka kipindi
kisichozidi miaka 99.
Miaka 99 ndicho
kipindi cha mwisho
kabisa cha kumilikishwa
ardhi wakati kipindi
cha kuanzia kinaweza
kuwa hata mwaka
mmoja.
Hii maana yake
ni kuwa unaweza
kupewa umiliki wa miaka 10,
20, Miaka 33, Miaka
66,
miaka mitano ilimradi
tu kipindi chako
kisizidi miaka 99.
Kama hujawahi kulijua
hili hebu itizame
vizuri hiyo hati
uliyonayo utaona imeandikwa
mda ambao itaisha.
2. NANI HUTOA
MUDA WA HATI.
Kamishna wa ardhi
ndiye mwenye mamlaka
ya kupanga muda wako
wa hati. Ndiye ataamua
hati ya umiliki
upewe kwa miaka
33, 66, 99 au
vinginevyo.
Kamishna hutoa mda
kulingana na matumizi
ya eneo husika yaani
makazi, biashara n.k., kulingana na mtu
anayeomba mgeni au raia, sera
ya ardhi ya
muda husika.
3. ATHARI BAADA
YA MUDA WA HATI
KUISHA.
Hapa ni pa muhimu sana
kwa wamiliki wa majumba
na viwanja. Muda
wa hati unapoisha
maana yake wewe
sio mmiliki tena. Haijalishi ni
nyumba yako umejenga
na umekaa miaka na
miaka na familia.
Basi unachotakiwa kufanya ni
kuhakikisha unaujua muda
ambao hati yako
inaisha na haraka kufanya
utaratibu wa kuihuisha(renew).Ili kuhuisha hati
utafanya maombi maalum
ili upewe muda
mwingine. Usipofanya hivi
basi hati yako
yaweza kufutwa (revocation) na hapo hautakuwa
mmiliki tena.
4. KWANINI UMILIKI UWE WA MUDA
MAALUM ?.
Sababu imeelezwa kifungu
cha 4(1 ) cha
Sheria ya ardhi namba
4/1999. Kifungu kinasema kuwa
ardhi yote ni
mali ya umma
na rais ndiye
msimamizi wake mkuu.
Maana yake ni
kuwa ardhi si mali ya yoyote bali
mmiliki wake ni
umma ambao ni
Tanzania. Tanzania ndiye
mmiliki wa ardhi sio mimi
na wewe.
Mimi na wewe ni kama
tumepangishwa. Ndio maana unapewa
kwa muda maalum na
muda huo ukiisha
unatakiwa ukahuishe( renew). Ndio
maana unailipia kodi
ardhi. Ndio maana
Tanzania ikitaka kukuhamisha
ili kujenga barabara
au mradi wowote
wa maendeleo huwezi kukataa
hata ufanyeje.
Ndio maana ardhi
uliyonayo ina masharti
kwa mujibu wa
kifungu cha 34 cha
sheria ya ardhi
ambayo ukiyakiuka ardhi
hiyo yaweza kuchukulia kuingia
mikononi mwa Tanzania
au Tanzania kumgawia
mtu mwingine.
Kwa ufupi unachomiliki
sio ardhi bali
ni haki au
maslahi ya muda fulani
katika
ardhi. Mwenye ardhi
ni Tanzania mimi
na wewe tunamiliki
haki au maslahi
fulani yenye ukomo maalum
katika
ardhi tulizonazo.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment