NA BASHIR YAKUB -
Kawaida hatimiliki(
granted right of
occupancy) hazitolewi kwa
ardhi za vijijini. Ardhi za
mijini tu ndizo
huwa na hadhi ya kupata
hatimiliki. Lakini wapo watu
ambao wamechukua maeneo ya
vijijni kwa ajili
ya uwekezaji.
Wapo waliochukua
ardhi kama wachimbaji
wadogo, kilimo, madini, n.k. Hawa pengine wangependa wapate
hatimiliki ili kukuza
biashara zao sambamba
na kupata faida zinazotokana na
kuwa na hati miliki. Moja ya
faida ya kuwa
na hatimiliki ni
pamoja na kupata
mkopo.
Swali ni je
inawezekana kuipatia ardhi
yako ya kijijni
hatimiliki yenye hadhi sawa na
ile inayotolewa kwa
ardhi za mijini?.
1.ARDHI YA
KIJIJI NI IPI.
Sheria za ardhi namba 4 na 5 kwa pamoja zimeainisha
aina tatu za ardhi
kwa hapa Tanzania.
Kwanza ardhi ya
jumla, ardhi ya
hifadhi, na ardhi ya
kijiji. Ardhi ya jumla( general land) ni hii
ardhi ya mijini
ambayo huwa na
hati miliki( right of
occupancy). Hii ni
asilimia 2 ya
ardhi yote ya
Tanzania.
Ardhi ya hifadhi( reserved land)
ni kama mbuga,
kingo za mito na bahari, makaburi, viwanja vya
wazi n.k. Hii ni asilimia 28 ya ardhi
yote. Ardhi hii huwa
haimilikishwa labda isemwe
vinginevyo.
Ardhi ya vijiji( village land). Hii ni
ardhi ya vijiji
kama jina lake
lilivyo. Sote tunajua vijijini
ni wapi. Inachukua
jumla ya asilimia 70 ya ardhi
yote.
2. UMILIKI
WA WA AINA
TATU WA ARDHI
YA KIJIJI.
Ardhi ya kijiji
iwe kwa uwekezaji, makazi au vinginevyo
inaweza kumilikiwa kwa
namna tatu tofauti. Kama
ifuatavyo.
( a ) Kumiliki kwa
haki bila nyaraka
yoyote ya umiliki( deemed right of
occupancy). Kwa mtu anayewekeza
kijijini huu si
utaratibu mzuri kwake. Hapa mmiliki
atamiliki ardhi kijijini
bila kuwa na
nyaraka yoyote inayomtambulisha kama
mmiliki lakini hilo
halitamwondolea uhalali wake
katika kumiliki. Wamiliki wengi
vijijni humiliki kwa
mtindo huu. Wengi
wana ardhi lakini
hawana nyaraka yoyote
kudhibitisha kumiliki.
( b ) Kumiliki kwa
hati ya kimila(customary certificate). Sura ya 114
sheria na 5
ya 1999 ya
ardhi ya vijiji
inatambua uwepo wa
hati za kimila. Hati
hizi hutolewa na
halmashauri za vijiji
kwa utaratibu maalum.
( c ) Kumiliki kwa
hatimiliki( granted right of
occupancy). Hatimiliki
hutolewa kwa maeneo ya
mijini tu lakini
hata vijijini zinaweza
kutolewa ikiwa ardhi
inachukuliwa kwa ajili
ya uwekezaji au shughuli
nyingine za serikali.
4. UTARATIBU WA
KUPATA HATI UNAPONUNUA ARDHI
YA KIJIJI KWA UWEKEZAJI.
( a ) Kwanza miliki
ardhi kijijini kwa kufuata
utaratibu wote wa umiliki
ardhi ya vijiji
kama unavyoainishwa na Sheria
ya ardhi ya
vijiji, sura ya 114
pamoja na kanuni
zake za mwaka 2001. Kwa
ufupi uwe unamiliki
ardhi ya kijiji
kihalali.
( b ) Baada ya
hilo utafanya maombi
maalum kwenda kwa kamishna
wa ardhi makao
makuu wizara ya
ardhi ukiomba kupatiwa
hati miliki katika ardhi
ya kijiji.
( c ) Katika maombi
hayo utaambatanisha nyaraka zote za
umiliki. Pia kama ni
kampuni inayoomba au
taasisi na si mtu binafsi
basi pia nyaraka
za kuthibitisha usajili
wake zitaambatanishwa.
( d ) Kamishna ataangalia
ikiwa kila kitu kinachohitajika kimefuatwa na
ikiwezekana atawasiliana na
uongozi wa ardhi
wa kijiji husika
ili kujiridhisha zaidi.
( e ) Ikiwa kila
kitu kitakuwa vizuri
basi ardhi hiyo
itabadilishwa kutoka ardhi
ya kijiji( village land)
na kuwa ardhi
ya jumla( general land).
( f ) Ikishakuwa ardhi
ya jumla basi
msajili wa hati( registrar of
titles) anaweza sasa
kutoa hatimiliki kwa
mwombaji ambayo itakuwa
na hadhi sawa
na zile hati za
mijini.
( g ) Wakati mwingine
ardhi iliyoombwa itamilikishwa kituo cha uwekezaji
Tanzania( TIC) halafu kituo hicho ndicho
kitakachompatia mwombaji.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment