NA BASHIR YAKUB -
Wenye nyumba hawako
salama ikiwa wapangaji
wao ni wahusika
wa dawa za
kulevya. Ni muhimu
kulijua hili ili
kujihadhari na kile
ambacho kinaweza kukuletea
madhara. Sheria mpya
ya kupambana na kuzuia
dawa za kulevya “The
Drug Control and Enforcement
Act, No 5
of 2015” imeeleza
kwa mapana uhusika
wa watu wa
kada mbalimbali katika
dawa za kulevya.
Tunachotakiwa kujua ni
kuwa uhusika haumlengi
tu yule mwenyewe
mhusika halisi bali
umeelekezwa mbali na hata kufika kwa
wenye nyumba au
wamiliki wa nyumba/eneo.
Pia uhusiano katika
sheria hii haumlengi
tu mwenye nyumba na
mpangaji wake, bali pia mwenye
nyumba na wale
walio katika nyumba yake
wawe watoto, mke, ndugu,
rafiki n.k., madhali ni
watu wako katika
nyumba yako au
eneo unalomiliki basi watakuhusu katika
hili .
Hata hivyo kabla ya
kuona hatia ya
mwenye nyumba/eneo tutizame
kwanza ni vitu
gani vinaitwa dawa za kulevya
ili kama unajihadhari
ujue lipi la
kujihadhari nalo.
1.NI VITU
GANI VINAITWA DAWA
ZA KULEVYA.
Sheria ya Kupambana
na dawa za
kulevya inataja aina
nyingi mno ya
vitu ambavyo imeviita
dawa za kulevya. Vipo
jamii ya kimiminika,
jamii ya unga,
jamii ya miti,
majani, mbegu n.k.
Kifungu cha 2
cha sheria hiyo
kinachosomwa sambamba na Schedule
ya 1 ya sheria
hiyohiyo kimeorodhesha zaidi
ya sampuli 100
ya vitu ambavyo
vinahesabika kuwa ni
dawa za kulevya hapa
Tanzania. Humo imo pia
bangi, mirungi, cocaine, heroine,
mandrax, morphine, cannabis resin
au opium,coca leaf, alphaprodine, etorphine n.k.
Ni vigumu kuzitaja kwa
Kiswahili lakini pia ni
vigumu kuzitaja zote kwa
kuwa ziko zaidi
ya mia. Muhimu
ni kuwa jihadhari
na mienendo ya wapangaji
au wale
uliowaweka katika nyumba/eneo lako.
Pia ujue kuwa
mirungi nayo ni
dawa za kulevya tofauti
na wengi wanavyodhani kuwa ni
kiburudisho cha starehe halali kama
ilivyo sigara au
vingine.
2. HATIA YA MWENYE
NYUMBA IKIWA MPANGAJI
ANAHUSIKA NA DAWA
ZA KULEVYA.
Kifungu cha 19 ( 1 ) cha
sheria hiyo kinakataza mmiliki
wa muda au
wa kudumu kuruhusu
eneo lake kutumika
kwa namna yoyote
katika shughuli yoyote
ya dawa za
kulevya.
Mmiliki wa muda
anaweza kuwa muangalizi
wa nyumba labda
ameachiwa jukumu hilo
na mmiliki halisi au
anaweza kuwa mpangaji
aliyempangisha mpangaji mwingine( sublease). Wote
hawa wanaweza kuwa
na hatia katika
kifungu hiki.
Mmiliki wa kudumu
ndiye mmiliki halisi wa
nyumba/eneo. Huyu naye
anawajibika katika kifungu
hiki.
3. VITU
GANI USIRUHUSU VIFANYIKE
KATIKA NYUMBA/ENEO LAKO.
Kifungu hicho
cha 19 kimeeleza
vitu hivyo. Kinasema maandalizi
yoyote ya
shughuli za madawa
ya kulevya yasifanyike kwenye nyumba/eneo
lako, matumizi yoyote kwa
mfano kuvuta bangi, kujidunga, kunusa, kulamba, au
kula. Kuuza au kununua. Kutumika kama
eneo la kutengenezea dawa, Kutumia
nyumba kama kituo
cha kufukishia dawa na aina
nyingine yoyote ya shughuli
hiyo.
4. ADHABU
KWA WENYE MAENEO/NYUMBA.
Kifungu cha 19( 2 ) kimeainisha adhabu ya
faini ya Shilingi
zisizopungua milioni tano au
kifungo kisichopungua miaka
mitatu jela, au vyote
viwili.
Kwa makala haya
ni vema sana kwa
wenye nyumba kujihadhari na shughuli
zinazofanywa na wapangaji
au yeyote anayekaa
katika nyumba/maeneo
yao. Usiseme simo
na hali unajua
kinachoendelea, kwa mujibu
wa sheria hii
umo.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment