Na
Bashir Yakub.
Sheria inayoshughulikia habari nzima
ya madawa ya
kulevya inaitwa “The Drug Control And
Enforcement Act”. Ni
sheria namba 5 ya mwaka
2015. Ni sheria
mpya kabisa. Msanii Wema
Sepetu ni kati
ya Watu walioko
mahakamani tayari kuamuliwa
kwa mujibu wa
sheria hii.
1.AINA YA
DAWA ZA KULEVYA.
Sheria hii inataja
aina nyingi mno
ya vitu ambavyo
imeviita dawa za
kulevya. Vipo jamii ya
kimiminika, jamii ya unga, jamii
ya miti, majani, mbegu
n.k.
Kifungu cha 2
cha sheria hiyo
kinachosomwa sambamba na Schedule
ya 1 ya sheria
hiyohiyo kimeorodhesha zaidi
ya sampuli 100
ya vitu ambavyo
vinahesabika kuwa ni
dawa za kulevya hapa
Tanzania.
Humo imo pia
bangi, mirungi, cocaine, heroine
na aina
nyingine nyingi. Katika
hizi Msanii Wema
anatuhumiwa kukutwa na
misokoto ya bangi.
2. JE
ILIKUWA SAWA WEMA
KUPEWA DHAMANA ?.
Ndio ilikuwa sawa. Wako watu
wanasema kuna mtu
amemkingia kifua akapata
dhamana. Hili si kweli . Dhamana
katika kesi za
madawa ya kulevya
hunyimwa kutokana na
kiwango ulichokutwa au unachotuhumiwa nacho. Kifungu
cha 29 cha
Sheria hiyo ya
kupambana na dawa
za kulevya kimeeleza
hilo kama ifuatavyo;.
( a ) Kama
ni cocaine, heroine, mandrax,
morphine, cannabis resin au opium
kuanzia gramu 200 au
zaidi hakuna dhamana.
Ni pote polisi
na mahakamani.
( b ) Kama
ni dawa aina
ya majani au
mimea kama bangi n.k kuanzia
kilo 100 au
zaidi hakuna dhamana. Ni
pote polisi na mahakamani.
( c ) Kama
ni dawa zenye
mfumo wa kemikali kuanzia
lita 30 au zaidi au
kilo 100 ikiwa
zimewekwa katika mfumo
wa unga au vinginevyo
hakuna dhamana. Ni
pote polisi na mahakamani.
Wema Sepetu alikutwa
na kiwango kidogo kwa taarifa
zilizotolewa, ni kama
msokoto mmoja hivi.
Ukiangalia hapa juu
hakuna popote ambapo kiwango hicho
kimetajwa kuwa hakidhaminiki.
Kwa
hiyo kosa lake
lilikuwa la kudhaminika
kabisa kwa mujibu
wa kifungu hiki.
3. JE WEMA ANAKABILIWA
NA ADHABU ZIPI ?.
Kifungu cha 17 ( 1 )
cha Sheria ya
Kuzuia na Kupambana
na dawa za
kulevya kinaeleza adhabu
ya miaka mitatu
jela, au faini isiyopungua
laki tano au
vyote viwili.
Kwahiyo panapo kupatikana
na hatia atatakiwa
kwenda jela miaka
mitatu, au asiende
jela iamuliwe alipe
faini inayoanzia laki
tano za Tanzania,
au aende jela
miaka mitatu na hapohapo alipe na faini
inayoanzia shilingi laki
tano kwenda mbele.
4. JE KIPI KINAWEZEKANA ZAIDI KWA
WEMA, KWENDA JELA AU
KULIPA FAINI.
Hapa kuna mambo
mawili ;
( a ) Kawaida sheria
inaposema kuwa, kwa kosa
hili mtu atalipa faini au
kwenda jela ( fine or
imprisonment) mahakama hutakiwa
kutoa adhabu iliyo
ndogo kati ya
hizi mbili( lesser punishment) .
Ikiwa
faini ndiyo adhabu
ndogo basi yafaa
mshitakiwa aamriwe kulipa
faini. Lakini ikiwa kifungo
ndiyo adhabu ndogo
basi yafaa mshitakiwa
aamriwe kufungwa.
Kwahiyo kama kifungu
kilichomshitaki Wema
kingekuwa kinatoa chaguo(option) mbili
tu yaani faini
au kwenda jela
basi bila shaka
kama angepatikana na hatia
ilitakiwa aamriwe kulipa
faini.
( b ) Sheria inaposema
kuwa kwa kosa
hili mtu alipe
faini au aende
jela au vyote
viwili mahakama huwa
na uhuru wa
kuchagua lolote katika
haya. Kwa maana
inaweza kuamua ulipe
faini na ukaachiwa, inaweza
kuamua uende jela
na pia inaweza
kuamua uende jela
na ulipe faini.
Tofauti ya hapa
na ( a ) ni
kuwa katika ( a ) kuna
chaguo ni mbili tu
ambazo ni faini
na jela ambapo
mahakama hutakiwa kutoa adhabu iliyo
ndogo katika hizo
mbili. Wakati katika ( b ) kuna chaguo
tatu yaani faini, Jela au
vyote viwili ambapo
hapa sasa mahakama
inao uhuru wa
kuchagua lolote katika
haya bila kujali
adhabu kubwa au
ndogo. Hapa inaweza kuamuliwa
jela, faini au
vyote viwili jela
na faini.
5. JE KOSA LA WEMA
LIPO KATIKA (a )
AU ( b ) .
Kosa la Wema
lipo ( b ) ambapo
mahakama itaamua lolote
katika matatu, kulipa
faini, kwenda jela miaka
mitatu au vyote yaani
kulipa faini pamoja na
kwenda jela. Mahakama itaamua
lolote katika haya
ikiwa tu atapatikana
na hatia. Hatia
mpaka ipatikane kwanza.
6. JE NI SABABU
ZIPI ZITAIFANYA MAHAKAMA
IAMUE WEMA AENDE
JELA AU ALIPE
FAINI AU VYOTE.
Kawaida zipo sababu
ambazo huzingatiwa na
mahakama kabla ya
kuamua mtu alipe
faini, aende jela
au vyote viwili.Baadhi
yake ni hizi;
( a )
Uzito wa kesi au kosa
lenyewe (gravity of an offence).
( b ) Tabia njema za
mshitakiwa kabla na wakati wa
kesi. Hapa tabia inaangaliwa
kumbukumbu za kijinai( criminal records, if any).
( c )Ushirikiano wa mshitakiwa
na mahakama wakati
wa kesi, kwa mfano kukiri
kosa mapema,kufika mahakamani
kwa wakati, nidhamu mahakamani
n.k.
( d ) Ikiwa mshitakiwa
aliwahi kutiwa hatiani
kwa kosa kama
hili hapo awali au
lah (habitual offender).
( e ) Umri
mkubwa sana au mdogo
zaidi wa mshitakiwa, ugonjwa
, ujauzito, wategemezi
wa mshitakiwa hasa
watoto wadogo kama wapo,
hasa wakati wa
kujitetea( mitigation).
( f ) Ni mara
ya ngapi kwa
mshitakiwa kutenda kosa.
( g ) Idadi ya
watu walioathirika na kosa
lake au athari
za kosa lake katika
jamii kwa ujumla.n.k.
Kwa hiyo ili Wema
aadhibiwe na kifungo, faini au
vyote kwa pamoja
itategemea mahakama itajibu
vipi maswali haya .
ikiwa majibu
ya maswali haya
yatakuwa mazuri kwa
Wema basi anaweza
kupewa adhabu ya
faini tu na akaachiwa.
Ikiwa majibu ya
maswali haya yatakuwa
mabaya anaweza
kupewa adhabu ya
kwenda jela bila
faini.
Na ikiwa majibu
ya maswali haya
yatakuwa mabaya zaidi
basi anaweza kwenda
jela na faini
juu yake.
Lakini yote haya
ni mpaka awe
amepatikana na hatia.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA SERIKALI
LA
DAILY NEWS NA
GAZETI JAMHURI KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment