Na Bashir Yakub -
1.NI WAKATI
GANI WANATAKIWA KULINDWA.
Ni ule wakati
ambao marehemu ameacha
mali lakini bado
hajapatikana msimamizi wa
mirathi kwa ajili
ya kusimamia mali hizo huku
kukiwa kuna watoto
wanaohitaji mahitaji muhimu
kutoka katika mali
hizo. Pengine hajapatikana msimamizi
wa mirathi kwakuwa
kuna mgogoro mahakamani,
au ndugu hawaelewani, au msimamizi
wa mirathi aliyeteuliwa
hajulikani alipo, au
kuna utata katika
wosia n.k.
Chochote kile ambacho
kitasababisha msimamizi wa mirathi
achelewe kupatikana basi
ujue ni wakati
huo ambapo mahitaji
na maslahi ya mtoto yanatakiwa
kulindwa.
2. YAPI MAHITAJI
YA WATOTO WADOGO.
Mahitaji ya watoto
wadogo ni kama
ada za shule,
mavazi, matibabu, na kila
ambacho ni muhimu
kwa ustawi wa mtoto.
Na kwa
suala la ada mtoto si lazima awe
mdogo sana bali
hata wale wa
kidato cha tano,
sita, chuo nao
waweza kuwa watoto
ambao maslahi yao
ni muhimu kulindwa .
3. WATOTO
WANAOSTAHILI KULINDWA.
Watoto wanaostahili kulindwa
ni wale ambao
watakuwa ni warithi
halali wa marehemu.
Ni wale ambao
hakuna mgogoro kuwa ni
warithi au si
warithi. Aidha ikiwa kuna
mgogoro kama watoto
au mtoto fulani
ni mrithi halali
au si mrithi basi
pia unaweza kuomba
kulinda maslahi yake ambapo
mahakama itaamua ikiwa
anastahili au hastahili.
4. NINI
UFANYE KULINDA MAHITAJI
YA WATOTO.
( a )
Mtu yeyote mwanafamilia,
ndugu, mzazi aliyebaki,mlezi anatakiwa
kupeleka maombi mahakamani
akiiomba mahakama kusimamia
baadhi ya mali
kwa muda ili
kupata mahitaji ya
watoto wakati wakisubiri
utatuzi wa mgogoro
katika familia.
( b ) Atapeleka maombi
hayo kwa kutumia Fomu
namba 7 ya Kanuni
za Mirathi ( The Probate
Rules).
( c ) Katika maombi
atataja tarehe ya
siku alipokufa marehemu
na wapi alikuwa
akikaa kabla ya
kifo chake.
( d ) Ataeleza ikiwa
marehemu aliacha wosia au
hapana na ikiwa
kuna mtu yeyote
amekwisha fungua mirathi
katika mahakama yoyote.
( e ) Ataeleza mali
zilizopo na zipi
kati ya hizo
anaomba kuzitumia ili
kulinda maslahi ya watoto/mtoto.
( f ) Pia
ataambatanisha kiapo kwa kutumia Fomu
namba 6 ya
kanuni za mirathi ( The
Probate Rules).
( g ) Baada ya
hapo atasikilizwa na maamuzi
yatatolewa.
5. UMUHIMU WA
KUFANYA HIVI.
Mara nyingi mtu anapokufa
kwenye familia hubaki
migogoro. Na wakati
mwingine mgogoro huwa
umefikishwa hadi mahakamani.
Mgogoro unapokwenda mahakamani
haijulikani ni lini
utakwisha. Haijulikani utaisha
baada ya miaka
mitatu, miaka minne ama
mitano.
Katika mazingira yenye
sura kama hii ikiwa
kuna watoto/mtoto yuko
shule ambaye alikuwa
akimtegemea marehemu kusoma
ina maana hatakuwa na
msaada na pengine
itafikia hatua atatakiwa
kuacha masomo.
Lakini si
masomo tu bali
pia wako katika hatari
ya kupoteza hata
mahitaji muhimu kwakuwa
aliyekuwa anatoa mahitaji hayupo
tena. Hii ni
kwasababu haijulikani mgogoro
utaisha lini .
Ni katika mazingira haya
unapotakiwa kuchukua hatua
zilizoelezwa humu ili kuyalinda
maslahi ya watoto/mtoto kwa kuwapatia
mahitaji muhimu kutoka mali
za marehemu kwa
muda ili kusubiri
mgogoro wa ndugu/wanafamilia uishe.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MWANDISHI
WA MAKALA YA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment