NA BASHIR YAKUB -
Yafuatayo ni maneno/taarifa/maudhui ya
msingi yanayotakiwa kuwa
kwenye wosia . Taarifa
yoyote kati ya
hizi ni ya muhinu na
inacho kitu cha
msingi na cha
kisheria inachosimamia na kulinda. Maana yake
ni kuwa kukosekana
kwake kutaathiri wosia
wako kwa namna
moja au nyingine.
( a ) Anza kwa
kuandika kichwa( heading). Kichwa
utaandika kawaida kama
unavyoandika kichwa cha
barua au taarifa
nyinginezo.
Mfano
“WOSIA” au “ WOSIA WANGU
MIMI PASCHAL STEVEN MUTIGANZI”, vyovyote kitakavyoandikwa muhimu
kiwepo kichwa.
( b ) Kinachofuata baada
ya kichwa ni
sentensi muhimu sana.
Ni sentensi inayolenga kuondoa
utata mbeleni.
Mfano ; “ HUU NI
WOSIA WANGU NA WA MWISHO
MIMI PASCHAL STEVEN MUTIGANZI”.
Ni sentensi inayoazimia
kuwa hakuna wosia mwingine baada
ya huo. Ni sentensi
inayolenga kufuta/kuondoa aina
yoyote ghushi.
( c ) Kinachofuata ni
kipengele ambapo mtoa
wosia/mwandika wosia anajitambulisha kwa majina
kamili, anuani na
tarehe ya kutoa/kuandika wosia. Anuani ijieleze
vizuri. Isiwe tu
P.O. BOX… ikaishia hapo.
Ieleze namba ya
nyumba kama ipo, mtaa,
kata, wilaya na
mkoa. Na anuani
nzuri ya kuweka
ni ile ya pahala yalipo
makazi yako ya
kudumu wewe mtoa
wosia. Ikiwa unayo makazi
mawili ya kudumu
kwa wale wa mitala basi
chagua mojawapo.
Mfano: “WOSIA HUU
UMEANDIKWA LEO TAREHE
13 / 2 / 2017 NA MIMI PASCHAL
STEVEN MUTIGANZI WA NYUMBA
NAMBA 13 , MTAA WA
MWINJUMA, KATA MWANAYAMALA , WILAYA
YA KINONDONI, MKOANI DAR
ES SALAAM, wa S.L.P
100 .
( d ) Andika sentensi ya
kuvunja wosia nyingine
zilizopita. Hii ni pale
ambapo umeandika wosia
mpya na kufuta ule
wa nyuma. Lakini
hata kama haujawahi
kuandika wosia ila
sasa ndio unaanza
basi hakuna ubaya
pia ukiweka sentensi
hiyo.
Mfano ;
“WOSIA HUU UNAFUTA
WOSIA NYINGINE ZOTE
NILIZOWAHI KUTOA/KUANDIKA HUKO
NYUMA”.
( e ) Kinachofuata ni
kipengele kinachotaja orodha
ya mali ulizonazo. Habari si tu
kutaja mali, bali
pia ni kuzichambua
mali hizo na kutaja
pahala zilipo kila
moja. Mali utazitaja kwa
namba. Namba 1….2……3…..n.k.
Mfano ;
“JUMLA YA MALI
NILIZONAZO NI, 1. NYUMBA
NAMBA 13 , ILIYOPO MTAA
WA MWINJUMA, KATA MWANAYAMALA
, WILAYA YA KINONDONI, MKOANI DAR
ES SALAAM. 2. GARI…..”(
taarifa za gari
au mashine yoyote zitajwe
kama ilivyo kwenye kadi
yake ya usajili)……( endelea kutaja
mali )
( f ) Kinachofuata ni kipengele
kinachotaja orodha ya
warithi/wanufaika wa mirathi.
Wataje kwa majina
yao yote.
Mfano; “WARITHI WANGU
KATIKA WOSIA HUU NI 1………………………..2……………………………3…………………..”n.k.
( g ) Kinachofuata ni
kipengele kinachoeleza nani umempa nini.
Mfano; .
1. “NYUMBA NAMBA
13 , ILIYOPO MTAA WA
MWINJUMA, KATA MWANAYAMALA , WILAYA
YA KINONDONI, MKOANI DAR
ES SALAAM NINAMPA
MWANANGU/MAMA YANGU/MKE WANGU……..……”2……….3……..n.k.
( h ) Kinachofuata ni
kipengele kinachohusu maziko
au msiba. Wapi uzikwe,
msiba uwe vipi,
muda gani uzikwe, kwa
staili ipi uzikwe
na kila kitu ambacho ungependa kifanyike katika
msiba na maziko
yako kwa ujumla
wake.
Mfano;
“ NITKAPOKUFA NIZIKWE KIJIJINI
KWETU GININGI NA
ZISIPITE SIKU NNE
BILA KUZIKWA n.k.
( I ) Kinachofuata
ni kipengele kuhusu
kumteua msimamizi/wasimamizi wa
mirathi.
Mfano ; “MSIMAMIZI/WASIMAMIZI WA
MIRATHI YANGU ATAKUWA/WATAKUWA……………………………”(
mtaje/wataje kwa majina
yao yote).
( j ) Kinachofuata ni
sahihi yako wewe mtoa
wosia pamoja na
majina ya mashahidi
na sahihi zao
pia.
Mfano; “MASHAHIDI,
1. JINA……………………
SAHIHI…………………… 2. JINA………….. SAHIHI……………..” n.k.
Unaweza kuamua shahidi
akawa wakili ni
jambo zuri pia, isipokuwa tu
wale mashahidi wa
msingi wanaotakiwa na sheria ni lazima wawepo. Makala kuhusu
mashahidi wanaoruhusiwa na
sheria itaelezwa wakati mwingine.
Kwa ufupi wosia
mzuri utakuwa katika
muonekana na mfumo
huo.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MWANDISHI
WA MAKALA YA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI KILJUMANNE.
0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment