NA BASHIR YAKUB -
1.WOSIA NININI.
Wosia ni matakwa
ya mtu ambayo
angependa yatekelezwe baada
ya kifo chake. Yanaweza
kuwa matakwa kuhusu
mali, maziko, madeni, watoto,mke/wake
n.k.
2. AINA
ZA WOSIA.
Tunao wosia wa
maandishi na wosia
wa maneno, lakini
pia tunaweza kupata
aina za wosia kutokana
na sheria mbalimbali zinazotumika
kugawa mali za
mirathi kama ifuatavyo :
( i )
Wosia wa
Kiislamu. Ni wosia ambao
misingi yake itakuwa
ni kutokana na Quran
Tukufu, Sunna na Hadith
za mtume Muhammad S.AW. Aina hii
ya wosia ni
maalum kwa mtu aliyeishi maisha ya
kiislam(muislam).
( ii )
Wosia wa
kikristo. Ni aina ya
wosia ambao misingi
yake imejengwa katika misingi ya Sheria
ya Urithi ya India ( The Indian
Succession Act , 1865) . Sheria
hii kwa jina
hilo hilo la Sheria
ya Urithi ya
India ndiyo hutumika hapa
Tanzania kwa mtu aliyeishi
maisha ya kikiristo(mkristo).
( iii )
Wosia wa kimila . Misingi ya
wosia huu imejengwa
katika Azimio la
Sheria za Kimila ( The
Local Customary Law
Declaration Order G.N. No. 279 of
1963) . Wosia huu
hutumika kwa watu
walioshi kimila.
3. NI
WOSIA UPI UANDIKE
KATI YA HIZI.
Niseme mapema tu kuwa unapoandika
wosia hakikisha unaandika kwa kufuata misingi
ya mfumo wa
maisha yako ( dini yako). Hili
si hiari ni
lazima.
Unapofanya kosa la
kuandika wosia bila
kufuata misingi ya
sheria husika kwa kujua
au kutokujua basi
wosia huo utakuwa ni
batili.
Unaweza kudhani umeandika wosia na kuamini
kuwa mambo yote sasa
yako vizuri lakini
kumbe hujaandika wosia.
4. JE
WOSIA NI UTASHI
WA MTU ?.
Ndio, wosia ni
utashi wa mtu
lakini utashi wenye mipaka.
Wengi
hudhani kwakuwa wosia
ni utashi na
mali ni zako basi
unaweza kufanya/kugawa unavyotaka
. Kwa wanaojua
hivi mawazo yao
sio sahihi.
Pamoja na wosia
kuwa utashi ni
lazima mgao pamoja na
kanuni za uandaaji
wake zirandane na
sheria husika. Kama we ni
muislamu lazima ugawe
kama sheria na
kanuni za kiislamu
zinavyosema, kama ni mkristo au
mtu wa mila
ni lazima ufuate
sheria inayokuhusu inavyosema.
Sheria zenyewe ni
hizi hapo juu
zilizoelezwa katika 2.
Nirudie tena kuwa hautagawa wala
kuandika unavyotaka
isipokuwa utagawa na
kuandika kama sheria inayokuhusu inavyotaka.
5. MADHARA
YA WOSIA ULIOKIUKA
MISINGI.
Wosia unapokiuka misingi
ya sheria husika
unakuwa batili. Bahati tu
iwe kwamba hapajatokea
mgogoro wowote. Iwe tu ndugu,
warithi wanaelewana na hivyo wosia
upelekwe tu hivyohivyo, au kusiwe
na mtu anayejua
taratibu za wosia.
Lakini wosia uwe
haujafuata misingi na atokee mtu
wa kulalamika mahakamani basi
wosia huo utabatilishwa
na mahakama itatoa
amri ya kugawa kwa
mujibu wa sheria
husika. Kile ulichousia
hakitafuatwa kabisa.
Lakini kama hilo
halitoshi utakuwa hujaacha
wosia bali bomu
kwa familia yako.
6. NASAHA.
Usikurupuke tu kuandika
wosia kwakuwa tu
mali ni zako,
watoto ni wako,
na mke/wake ni
wako. Pata ushauri kuhusu
misingi ya wosia
kutokana na aina/mfumo
wa maisha unayoishi( dini).
Wosia
una sehemu kuu
mbili kwanza mfumo
wa uandishi, na pili
maudhui ya nani
anapata nini.
Haya yote mawili
yanaongozwa na sheria na sio
matakwa binafsi.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MWANDISHI
WA MAKALA YA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
”. 0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment