NA BASHIR YAKUB -
Hivi karibuni kumeibuka
miradi mingi binafsi
na ya serikali
hasa kupitia NHC ya
ujenzi wa nyumba
za pamoja. Miradi ipo kwa
majina tofauti ipo
inayoitwa APARTMENT, CITY, VILLAGE,
TOWN, n.k. Baadhi ipo kigamboni,
Arusha na maeneo
mengine .
Pia ipo
katika mitindo tofauti
ipo ile ya
maghorofa ya
kwenda juu, maghorofa ya mshazali,
na ile ya
nyumba moja moja
lakini katika eneo
moja (common ground).
Kutokana na hilo
makala yalenga kukufahamisha usinunue tu kwa
kupenda muonekano,mazingira na
rangi , bali pia uwe na
uhakika wa faraja(comfortability) inayotokana
na mambo mengine nje ya muonekano,
rangi
na mazingira.
1.TOFAUTI KATI
YA NYUMBA ZA
MIRADI NA NYUMBA
ZA KAWAIDA.
Ipo tofauti kati
ya nyumba za
kawaida tulizozoea na
hizi za miradi
zilizotajwa humu. Tofauti
ipo katika ngeli hizi :
( a ) Taratibu
zake za ununuzi.
( b ) Vitu
unavotakiwa kujua kabla ya
ununuzi.
( c )
Sheria zinazozilinda na,
( d ) Maisha yako
baada ya kuwa
umenununua.
Makala yataeleza vitu unavyotakiwa
kujua vinavyotofautisha nyumba
hizi na nyingine za
kawaida.
2. VITU UNAVYOTAKIWA
KUJUA.
( a ) Uwepo wa
malipo na michango
mbalimbali. Pamoja na kuwa ni mali
yako umenunua , kanuni ya 15( 2 )
ya The Unit
Title Regulations, G.N 357/2009 imeeleza
baadhi ya michango. Ipo
michango kwa ajili
ya chama na
uongozi, michango kwa
ajili ya maeneo
ya matumizi ya
pamoja, michango kwa ajili
ya huduma mbalimbali
mnazotumia pamoja.
Michango hapa haihusishi
bili zako za
umeme,maji n.k. Michango hii inaweza
kuwa inalipwa kila
mwezi au vinginevyo
kadri ya utaratibu
wa eneo husika.
Hii ni tofauti
na nyumba za
kawaida ambazo haziko
katika mfumo huu ambapo ukinunua
umenunua hakuna mchango
wa chama au
vinginevyo.
( b )
Uwepo wa
katiba. Tofauti na nyumba
nyingine ukinunua utaongozwa
na sheria za
kawaida zinazoongoza nchi na watu wote
hapa kuna katiba
maalum ya kuongoza
mkusanyiko katika eneo
husika. Kanuni ya
14 ya The
Unit Titles Regulations, G.N 357/2009 imeeleza
hatua hiyo na
kutoa mfumo wa
katiba yenyewe inavyotakiwa kuwa.
Unachotakiwa kufanya
ni kuwa
soma katiba hiyo
na masharti yake
kuona kama utayaweza au laah. Jambo hili hakuna nyumba
za kawaida.
( c ) Uwepo wa
sheria ndogondogo( By Laws). Sheria ndogondogo
ni tofauti na
katiba hapa juu. Sheria ndogondogo
zinaanzishwa na kifungu
cha 19 cha The Unit
Titles Act,No 16/2008. Sheria
ndogondogo zitatungwa na
uongozi wa eneo
la mradi wakati
katiba haitungwi na
uongozi wa mradi
bali inachukuliwa kama
ilivyo kutoka Kanuni
ya 14( 2 ) ya
The Unit Titles
Regulations, G.N 357/2009.
Umuhimu ni kuwa
kabla hujanunua pata
sheria hizo, zipitie
uone kama unakubaliana
nazo au lah. Hii
ni tofauti na
ununuzi nyumba za
kawaida ambapo hamna
kitu kama hicho.
( d ) Uwepo wa
maeneo ya pamoja. Ujue mapema
ni maeneo gani
mtatumia watu wote
mnaoishi hapo na
ikiwa utapenda kushiriki (share) maeneo hayo
au hapana. Korido
za pamoja, maegesho ya
magari ya pamoja, eneo
la kuogelea la
pamoja( swimming pool), viwanja
vya pamoja, na maeneo
mengine kadri chama
na sheria zenu
zitakavyoelekeza.
( e ) Uwepo wa
chama. Ukinunua ni lazima
uwe mwanachama wa
chama hicho. Najua
wapo wasiopenda hizi
habari za vyama vyama
lakini hapa ni
lazima. Kifungu cha 35 cha
The Unit Titles
Act,No 16/2008 kinasema katika
nyumba za namna
hiyo lazima kuwe na
chama.
Na chama kitakuwa
na mikutano ya
wamiliki na mtatakiwa
kuhudhuria. Mikutano inaweza kupangwa
kila baada ya
muda fulani ambao uongozi
utaona unafaa.
( f )
Uwepo wa uongozi. Kifungu cha
47 cha
The Unit Titles
Act,No 16/2008 kinasema
lazima kuwe na
uongozi. Kazi ya uongozi
itakuwa ni kusimamia
katiba yenu na
sheria zenu ndogondogo ikiwa ni
pamoja kuamua migogoro
ya maeneo hayo.
Mmiliki utatakiwa
kutii uongozi huo na
hauruhusiwi kupeleka mgogoro
wowote unaohsu eneo
hilo mahakamani kabla
ya kushitaki kwa uongozi kwa
ajili ya usuluhishi.
Kifungu cha 69 cha
The Unit Titles
Act,No 16/2008 kinataka hivyo.
3. ANGALIZO
Makala hayalengi kwa
namna yoyote kuzuia
watu kununua nyumba za
namna hiyo, laa hasha,
isipokuwa yanalenga kutanua
mawazo ya wanunuzi
kutoka kupenda muonekano, rangi
za majengo na mazingira tu,
kwenda mbali zaidi kwenye
maisha ya jumla
katika nyumba za
namna hiyo.
Pia ifahamike
kuwa haya yote
na mengine ambayo hayakuzungumzwa humu yapo kwa
mujibu wa sheria
na hivyo kila
aina ya nyumba
za namna hiyo ni Lazima
haya
yawepo.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MWANDISHI
WA MAKALA YA SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
”. 0784482959, 0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment