NA BASHIR YAKUB -
Mtu anapokufa huacha
warithi wa namna mbalimbali.
Yumkini ndani mwake waweza kuwamo
watoto wenye umri
mdogo na hata vichaa.
Umri mdogo twaweza
kuuhesabu kuanzia mwaka
0 mpaka 18. Aidha wakubwa ambao wamezidi
miaka 18 hao nafasi yao
inajulikana ikiwa marehemu
ameacha mali.
Mali zao watakabidhiwa
kwa utaratibu maalum
ulioratibiwa na sheria.
Swali litakuwa kwa watoto wadogo ambao
hawawezi kukabidhiwa,
tutahitaji kujua sheria
inasemaje.
Hapa kuna mazingira
ya aina mbili kwanza, ni pale marehemu
anapoacha warithi watoto
tu na hakuna
mkubwa hata mmoja na pili ni
pale anapoacha warithi wakubwa na
watoto.
Pia kwa ufupi
tutaangalia sheria inavyosema
kuhusu mali za mrithi ambaye
hana akili timamu. Hii
nayo tutaangalia mazingira
yote, mazingira anapokuwa
na warithi wenzake
na mazingira anapokuwa
mrithi pekee.
1.MTOTO MDOGO.
Sura ya 352 kifungu
cha 23 Sheria ya
mirathi kinasema kuwa
urithi au hati
ya kusimamia mirathi
haiwezi kutolewa kwa mtoto
mdogo.
Tukiachana na hilo
tujue kuwa ikiwa mtoto mdogo
si mrithi pekee
isipokuwa wapo ndugu zake wengine
ambao ni warithi
basi mmoja wao
muadilifu atateuliwa kusimamia
mirathi yote ikiwemo ya mtoto
mdogo. Msimamizi huyo
atakuwa na wajibu
wa kuhakikisha anatunza
mali ya mtoto/watoto
hao mpaka wanakua
na kuwa na uwezo
wa kutunza mali
zao binafsi.
Pili ni pale ambapo
mtoto/watoto wadogo ndio
warithi pekee wa
mali yaani hakuna mkubwa
kati yao. Ikiwa
hilo litatokea basi
mlezi wa watoto anaweza kuomba
mahakamani kusimamia mirathi hadi
watakapokua.
Taasisi ya udhamini
( trust cooperation) pia
yaweza kuomba au kupewa bila
kuomba jukumu la kusimamia
mali za watoto hadi
watakapokua. Hii ni kutoka
kifungu cha 22 cha sheria
ya mirathi. Yeyote
atakayeteuliwa kati yao
atakuwa na wajibu mkubwa wa
kuhakikisha anatunza mali
za watoto kwa
kadri mahakama itakavyoelekeza.
Wakati mwingine wanaweza
kujitokeza walezi wengi
kila mmoja akitaka kusimamia
mali za watoto.
Ikiwa itakuwa hivyo
basi suala hilo
litapelekwa mahakamani na
mahakama itaamua nani
anafaa kusimamia mali
hizo kwa kuzingatia
zaidi mustakabali wa baadae ya
hao watoto.
2. ASIYE
NA AKILI TIMAMU.
Kifungu cha 23 cha sheria ya
mirathi kinakataza kabisa
mtu asiye na
akili timamu kusimamia
mali au kupewa
hati ya kusimamia
mirathi. Hii haijalishi hata katika
mazingira ambayo yeye ndiye mrithi
pekee.
Kifungu cha 37
cha sheria ya
mirathi kinasema kuwa
ikiwa mtu anayestahili
kurithi au kusimamia mirathi hana
akili timamu basi
mali zake zitatunzwa
na mtu ambaye
anamtunza mtu huyo . Atasimamia mali
hizo kwa maslahi
ya mtu huyo. Isipokuwa kama kuna
anayepinga kuhusu fulani
kusimamia mali za
asiye na akili
timamu basi atapeleka maombi yake mahakamani
na sababu kwanini anadhani fulani hafai katika hiyo
nafasi.
Zaidi, msimamizi
ataruhusiwa kutumia hela
inayotoka katika mali
zile kwa matumizi
ya mtu huyo tu
ikiwa kuna mali
zinazozalisha. Matumizi ni kama mavazi, malazi, makazi, matibabu na mahitaji mengine
muhimu kwa ustawi wa binadamu.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MWANDISHI
WA MAKALA YA SHERIA KUPITIA GAZETI
LA JAMHURI KILA JUMANNE. ”. 0784482959,
0714047241bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment