NA BASHIR YAKUB -
Unao watoto wa
namna mbalimbali. Unao uliowazaa
ndani ya ndoa
na wale uliowazaa nje
ya ndoa. Unawapenda sana
wote kwa usawa kwasababu wote ni
watoto wako. Kuna suala
la kifo na
ungependa baada ya
kifo chako watoto
wako wote wafaidi
kidogo ulichochuma. Lakini je
hilo umelijengea mazingira.
Ni muhimu sana
ujue kuwa suala la
watoto wako kufaidi
ulichonacho halitokani na matakwa
yako, laa hasha bali
linatokana na matakwa ya sheria.
Wewe waweza kuamua
watoto wako wote wa
nje ya ndoa
na wale wa
ndani ya ndoa
wapate mali lakini baadhi
wakakosa kutokana na msimamo
wa sheria.
Ni hapo
unapotakiwa kuandaa mazingira
yanayoendana na matakwa
ya sheria ili
watoto wako wote
waweze kufaidi machumo yako.
1.FANYA HAYA ILI KUWAWEZESHA WATOTO
WA NJE YA NDOA KURITHI.
a. KWA WAISLAMU.
Kama wewe ni
muislam na una mtoto/watoto nje
ya ndoa hakikisha
unaandika wosia ambao
utampatia mali hata
huyo mtoto wa
nje ya ndoa. Lakini
lazima ujue kuwa
mali yako yote uliyonayo ni 3/3 = (100%). Hivyo
2/3 ya mali yote
ni lazima iende
kwa warithi halali
ambamo mtoto wa
nje ya ndoa
hataingia kabisa.
Katika
mali hiyo ya 2/3
wala haihitaji wosia
kwakuwa tayari sheria ya
kiislam imeeleza vipi
hiyo mali igawanywe.
Uhuru wako wa
kugawa mali kwa wosia upo katika 1/3 basi na
si vinginevyo. Na ni kusema kuwa mtoto/watoto wa
nje ya ndoa
haki yao ipo katika
1/3 tu. Ikiwa utampatia mali zaidi ya 1/3
basi anaweza kunyanganywa . Kwahiyo
uelewe kuwa wosia
utakaoandika unahusu 1/3 ya
mali tu.
Zingatia kuwa usipoandika
wosia kugawa 1/3 yote au
sehemu yake kwa mtoto/watoto uliowazaa
nje ya ndoa
basi hawatapata mali
kabisa baada ya kifo
chako. Na hii
ni kwasababu watoto
hao hawaruhusiwi kurithi
kisheria.
Kwahiyo utaona kuwa
unachotakiwa kufanya ili
hao watoto wasikose
ni kupiga hesabu
ili kupata 1/3
ya mali yako
na kuwapa yote
au sehemu yake.
b. KWA WANAOISHI
MAISHA YA KIMILA.
Karibia taratibu za
kimila zote haziruhusu
watoto wa nje
ya ndoa kurithi. Hii
ina maana ikiwa
unaishi maisha hayo
na unakufa hawa
watoto hawatarithi. Unachotakiwa kufanya
ili waweze kurithi
hata baada ya
kifo chako ni kuwahalalisha
watoto hao kabla hujafa.
Utaratibu wa kuwahalalisha
watoto wa nje
ya ndoa hutofautiana katika mila
na mila. Utakachofanya ni
kufuata utaratibu wa
mila yako kama
ulivyo na kuwahalalisha
watoto hao. Usiseme nitaandika
wosia niwape mali
hapana. Hii ni kwasababu
wosia wataupinga kuwa ni
wosia uliokiuka taratibu kwa kuwarithisha wasiostahili. Kinachotakiwa ni
kuwahalalisha kwa mujibu
wa mila yako.
c. KWA WASIO
WAISLAM NA AMBAO HAWAISHI
MAISHA YA KIMILA.
Hawa mara nyingi
ni wakristo . Sheria inayotumika
kwao ni sheria ya
Urithi ya Mwaka 1865. Sheria hii
nayo inakataza mtoto
wa nje ya
ndoa kurithi. Hivyo basi ili
kumwezesha kurithi unatakiwa
kuwa umeandika wosia
ambapo utawapatia mali.
Ikiwa utakufa bila
kuacha wosia hata
kama ulikuwa unaishi
nao hawataruhusiwa kurithi.
Kinachotakiwa ni uandike
wosia na wao
uwajumuishe humo.
Pia lakini hii ni
ziada ni
vema kuwa umewatambulisha kwa
ndugu zako, wana
ukoo na hata
mke kama unaye.
Yote kwa yote
ifahamike kuwa ni muhimu kuweka
maandalizi ya kisheria katika suala
la mirathi. Usipofanya hivyo
usitegemee watoto/mtoto wa nje ya
ndoa kurithi mali zako lakini pia
ujue utakuwa umekufa
huku umeanzisha mgogoro
mkubwa katika familia.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MWANDISHI
WA MAKALA YA
SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
”. 0784482959, 0714047241
bashiryakub@ymail.com
.
0 comments:
Post a Comment