NA BASHIR YAKUB -
Kampuni
ya umma ndio
huitwa public company
kwa kiingereza. Kampuni
hii hutofautishwa na
kampuni binafsi (private
company). Zote ni
kampuni kwa ajili
ya biashara na mara zote
hutegemea unahitaji kufanya
nini ili ujue
ni kampuni ipi
uunde.
1.JE KAMPUNI
YA UMMA INAWEZA
KUMILIKIWA NA WATU BINAFSI.
Ndio
inawezekana. Watu wengi
hudhani kwa kuwa jina
la kampuni hii
ni UMMA basi
hudhani ni kampuni ambazo
huundwa na serikali. Neno
umma ni jina
na limetokana na
namna muundo wa
kampuni yenyewe ulivyo , yumkini halina
uhusiano wowote na
kampuni za namna
hii kumilikiwa na serikali.
Hivyo
yafaa ifahamike kuwa hata
wewe mtu binafsi
mjasiriamali wa kawaida waweza kuunda
kampuni ya namna
hii pengine kutokana
na faida zinazotokana
na kampuni ya
aina hii.
2.KWANINI UUNDE
KAMPUNI YA UMMA
BADALA YA KAMPUNI
BINAFSI.
( a ) Uhuru wa
wanahisa. Kampuni ya
umma imetoa uhuru
mkubwa kwa wanahisa.
Wakati kampuni binafsi
inaruhusu kuwa na
wanahisa mwisho 50 kampuni
ya umma haina
ukomo wa idadi
ya wanahisa.
Hii ina maana
waweza kuwa na
wanahisa hata milioni
na zaidi. Hakuna
ukomo wa kiwango
cha mwisho isipokuwa
kuna ukomo wa
kiwango cha chini. Kiwango cha
chini yalazimu wanahisa
kuanzia wawili.
( b ) Uhuru
wa kuuza na kununua
hisa. Katika kampuni binafsi
hakuna uhuru wa
kununua na kuuza
hisa. Katika kampuni binafsi yatakiwa
kabla hujauza hisa
zako kwa mtu
mwingine upate ridhaa ya
wanahisa wenzako. Wakikataa
huwezi kuuza.
Lakini
pia huwezi kumuuzia
hisa mtu ambaye
wanahisa wengine hawampendi. Yule wanayempenda
na kumridhia ndiye huyo
unayeweza kumuuzia tu
na si vinginevyo.
Hii
ni tofauti na
kampuni ya umma
ambapo mmiliki wa
hisa ndiye anayechagua
nani amuuzie hisa.
Hakuna yeyote kati
ya wanahisa wenzake anayeweza
kumzuia kuuza hisa
zake.
Kwa haraka unaweza
kuona kuwa katika
kampuni binafsi uuzaji
na ununuzi wa hisa
ni biashara huru
inayotokana na maamuzi ya mtu.
( c ) Uhuru wa
kutangaza hisa katika
soko la hisa. Katika
kampuni binafsi hakuna
ruhusa ya kutangaza uuzaji
wa hisa katika
soko la hisa.
Soko la hisa
Tanzania ni moja
tu yaani Soko la
hisa Dar es
salaam ( DSE).
Wakati
kampuni ya umma ruhusa
iwazi kuwa unaweza
kutangaza hisa zako na
watu wanaoona kampuni
yako inaweza kufanya
kazi na ina
mwelekeo mzuri wanaweza
kununua hisa na
hivyo kampuni kukua
na kujiimarisha.
3.JINA LA
KAMPUNI YA UMMA.
Sheria
inataka kila jina
la kampuni ya
umma kuishia na neno PUBLIC
LIMITED COMPANY (PLC). Itaanza
na jina lolote
ulilochagua lakini mwisho
lazima iishie hivyo. Mfano
KR PUBLIC LIMITED COMPANY
au KOP PUBLIC LIMITED
COMPANY nk.
Utakuwa
umewahi kuona huko
mitaani neno PLC
katika mabango ya
makampuni mbalimbali. Hili humaanisha
Public Limited Company na sio
hiari kuweka bango hivyo bali
ni lazima.
Baadhi
ya makampuni ya
umma hapa Tanzania
ni kama CRDB, NMB nk,
kwa kutaja ni machache.
Hata
wewe waweza kuunda
kampouni ya namna hii kw faida nilizotaja na nyingine
ambazi sikutaja.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MWANDISHI
WA MAKALA YA
SHERIA KUPITIA GAZETI LA JAMHURI
KILA JUMANNE.
”. 0784482959, 0714047241
bashiryakub@ymail.com
Kwanini CRDB na NMB ni makampuni ya umma ila hayana PLC yaani PUBLIC LIMITED COMPANY