NA BASHIR YAKUB -
Iliwahi kuelezwa katika
safu hii kuhusu
aina mbalimbali za
makampuni. Kubwa
lililoelezwa ni kuwa unatakiwa
kujua aina gani ya kazi/biashara unataka kufanya
ili ujue ni aina gani
ya kampuni itakufaa. Si
kila kampuni inaweza kufaa katika unalotaka
kufanya.
Na hii ndio
sababu zikawepo aina
mbalimbali za kampuni. Pia
yafaa ujue kuwa kila
aina yua kampuni utakayochagua inazo
hasara zake na
faida zake. Hata
hivyo ili pawe
na hasara itategemea uchaguzi
wako wa kampuni
kulingana na aina
ya kazi unayotaka
kufanya.
Makala ya leo
yataeleza kampuni isiyo
na hisa na kwa
kazi gani kampuni
hii inafaa .
1.NINI MAANA
YA KAMPUNI KUTOKUWA
NA HISA.
Kampuni kutokuwa na hisa
maana yake ni kuwa kampuni
itakuwa kama kampuni
nyingine zilivyo lakini
haitakuwa na mtaji
mkuu( share capital). Kawaida kampuni
tulizozoea huwa zina hisa
kwa mfano utasikia
kampuni hii ina
hisa 10000, au
hisa 30000 au 100
nk. Katika kampuni ya aina hii hukutakwa
na kitu
cha namna hii.
2. JE INAWEZA
KUWA NA WANAHISA.
Hapana kama haina
hisa basi haiwezi
kuwa na wanahisa. Hakuna mtu anaweza kujiita
mwanhisa kama kampuni
haina hisa. Itakuwa
na wakurugenzi, katibu, na
wanachama lakini sio wanahisa.
3. JE KUNA
MGAO WA FAIDA
KWA WANACHAMA.
Hapana kampuni ya namna hii
haina mgawanyo wa faida (profit dividend) kwa wanachama
wake. Hili halimaanishi kwamba
kampuni hii haitakuwa
ikilipa mishahara kwa
wafanyakazi wake hapana.
Katika uendeshaji wa
kampuni kuna tofauti kubwa
kati ya mgawanyo
wa mapato na
malipo ya mishahara.
Mgawanyo wa mapato huwa
ni kwa wamiliki
wa kampuni au
wanahisa. Wakati mishahara huwa
ni kwa wafanyakazi
ambao pengine sio
wanahisa au wamiliki
wa kampuni. Mishahara
huwa ni kwa
waajiriwa.
4. JE KAMPUNI
HII INAFAA KWA
BIASHARA/KAZI IPI.
Kampuni ya namna
hii inafaa kwa
watu ambao wanataka
kufanya kazi ya
kutoa misaada katika
jami, kazi za
hisani, klabu za michezo, vyama vya
kijamii nk. Kampuni ya
namna hii ni
nzuri na inafaa
kwa makundi haya.
Uzuri wake ni
kwamba itafanya biashara
yoyote halali kama kawaida sawa
na kampuni nyingine huku
ikitumia faida kuhudumia
jamii. Hii ni tofauti na utakapoamua kuunda
NGO ili kuhudumia jamii
ambapo hautaruhusiwa kufanya
biashara.
Lakini pia sawa
na kampuni zenye
hisa wanachama katika
kampuni hii hawatakuwa
na hatia iwapo kampuni itakuwa
na madeni .
Mali zao binafsi hazitaweza kuuzwa
ili kulipia madeni
ya kampuni.
Kwahiyo taasisi ,
kikundi au watu
binafsi ambao wangependa
kufanya biashara lakini
huku wakitoa huduma
za hisani katika
jamii, au vilabu
vya michezo hii
ni aina ya
kampuni inayofaa na
yenye faida nyingi kwao hata
ambazo hazikuelezwa humu.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MWANDISHI
WA MAKALA YA SHERIA
KUPITIA GAZETI LA
JAMHURI KILA JUMANNE.
”. 0784482959, 0714047241
bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment