NA BASHIR YAKUB -
1.WARRANTY NININI
KATIKA BIASHARA.
Warranty ni mkataba
kati ya mtengeneza
bidhaa na mnunua
bidhaa ambaye naye
anakwenda kumuuzia mtu wa
tatu( mteja). Kunakuwa na watu
watatu. Kwanza ni mtengeneza bidhaa,
pili ni
mnunua bidhaa ambaye naye
anakwenda kuuza(mfanyabiashara) na tatu ni
mnunua bidhaa (mteja) anayenunua
kwa ajili ya
matumizi.
Kwa mfano una
duka la simu
kariakoo, we ni mfanyabiashara. Yule
aliyekuuzia simu kwa mfano
tecno company huyo ni mtengenezaji. Na anayekuja
kariakoo kununua simu kwa
ajili ya matumizi
huyo ni mteja. Kwahiyo kisheria
Warranty ni mkataba
kwa ajili ya
hawa watatu katika kuhakikisha ubora na
ufanisi wa bidhaa.
2. JE MIMI
KAMA MFANYABIASHARA
NINALAZIMIKA KUANDIKIWA MKATABA
WA WARRANTY .
Ndio unaponunua bidhaa
popote kwa ajili ya
kuuza tena ni
lazima uwepo mkataba
wa warranty . Ni mkataba
wa warranty pekee
utakaokuweka salama na
bidhaa uliyonunua.
Mfanyabiashara sio
mtengeneza bidhaa na hivyo
kwake sio rahisi
kujua ubora, muda wa
kuishi wa bidhaa,pamoja na
mambo mengine yanayohusu
uimara na ufanisi
wa bidhaa katika
matumizi.
Ni kutokana na
hilo analazimika kupata
mkataba wa warranty
ambao ndio uhakiki na ithibati ya ufanisi
na ubora wa
bidhaa.
3. JE KUNA TOFAUTI
KATI MKATABA WA
KUNUNUA BIDHAA NA
MKATABA WA WARRANTY.
Ndio kuna tofauti. Mkataba wa
kununua bidhaa ni mkataba wa kununua kama neno lilivyo na
hueleza kuhusu manunuzi.
Wakati mkataba wa
warranty ni mkataba
ambao hauelezi jambo jingine
lolote isipokuwa ubora
katika matumizi ya
bidhaa, ufanisi wake, muda
wa matumizi, na
kila jambo linalohusu uimara na umathubuti
wa bidhaa.
Pia lazima ueleze nini
kitatokea iwapo bidhaa
haitafanana na maelezo hayo. Ikiwa
bidhaa itarejeshwa, au pesa
ya manunuzi itarejeshwa
au vinginevyo, ni lazima ielezwe. Hii
ndio huitwa “warranty
contract.”.
4. JE WARRANTY
KWA MDOMO INAKUBALIKA
KISHERIA.
Ndio inakubalika ila
sio nzuri kisheria.
Warranty nzuri inayoweza
kukusaidia kubadilishiwa bidhaa kwa kupewa nyingine
au kurudishiwa fedha
ikiwa kuna tatizo ni
warranty iliyo katika
maandishi. Hii ni rahisi
kuithibitisha kuliko ile
ya mdomo.
Warranty ya
mdomo inahitaji uwe
na mashahidi waliosikia
mtengeneza bidhaa akiitoa. Jambo hili
laweza kuwa gumu. Hivyo ni muhimu kuwa na
mkataba wa
warranty wa maandishi.
5. KUNA TOFAUTI
GANI KATI YA
WARRANTY NA GUANRANTEE.
Warranty hutolewa na
mtengeneza bidhaa wakati
guarantee hutolewa na muuza bidhaa(mwenye duka). Ukienda kariakoo
kununua simu mwenye
duka atakupa guarantee. Yeye anapata
warranty wewe anakupa
guarantee.
Na guarantee sio
lazima iandikwe ila sheria inaamini
unapomuuzia mteja bidhaa kwa matumizi ni lazima
iwe bora na
imara na kinyume
chake unatakiwa kumpa
bidhaa nyingine au kumrudishia mteja fedha
yake.
Ni jambo hili
linalomlazimu mfanyabiashara kupata
warranty ili mteja akirudisha
bidhaa basi naye
airudishe kwa mtengenezaji
kupitia mkataba wa warranty. Lakini
kama hana mkataba
wa warranty ina maana atalazimika
kutoa hela yake mfukoni
kumrudishia mteja.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MWANDISHI
WA MAKALA YA SHERIA
KUPITIA GAZETI LA
JAMHURI KILA JUMANNE.
”. 0784482959, 0714047241
bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment