NA BASHIR YAKUB -
Suala la wapi ukufungue kesi ni suala
kitaalam. Unapokosea mahali pa kufungua
kesi unakaribisha kushindwa
kesi hata kama
una haki katika kile
unachodai. Si kila mahakama
unaweza kufungua kesi. Zipo
mahakama unaweza kufungua
kesi na zipo Mahakama
huwezi
kufungua kesi.
1.MADHARA YA KUFUNGUA KESI
MAHAKAMA ISIYO.
Sheria iko wazi
kuwa yeyote anayefungua
kesi katika mahakama
ambayo hakutakiwa kufungua
basi kesi hiyo
ni sharti itupwe(strike out). Haijalishi una
haki za msingi
katika madai yako
au lah, kitendo cha
kufungua pale pasipo
stahili chatosha kabisa
kufuta kesi yako mara
moja.
Kwa madhara kama
hayo upo umuhimu mkubwa
wa kujua ni
wapi pa kufungua
kesi na ni
mahakama ipi ni
sahihi katika lalamiko
ulilonalo. Kila lalamiko au shauri
linayo mahakama yake
sahihi unapoweza kulifungua .
Kuna lalamiko unaweza
kufungua mahakama A lakini huwezi
kufungua mahakama B. Yapo
mambo ya
kujua na kuzingatia
unapotaka kufungua kesi katika mahakama
sahihi.
2.MAMBO YA
KUZINGATIA UNAPOTAKA KUFUNGUA
KESI KATIKA MAHAKAMA
SAHIHI.
Kwanza ujue eneo
ulipotokea mgogoro kuna
mahakama zipi. Karibia
kila eneo linazo
mahakama zake za
mwanzo, za wilaya, na za ardhi. Kwa mfano
sinza kuna mahakama
ya mwanzo Sinza
na kuna mahakama ya
wilaya ya kinondoni na mabaraza
mengine ya ardhi.
Pili ujue kiasi
cha thamani ya mgogoro
wako. Kwa mfano kama
unamdai mtu hela, au
fidia, ujue kwa pamoja
ukijumlisha zinakuja kiasi
gani. Au kama
ni mgogoro unaohusu
mali basi lazima
ujue mali hiyo
ina thamani kiasi
gani kifedha.
Tatu lazima ujue aina ya
mgogoro wako. Kwa mfano je ni
mgogoro wa kazi,
ni mgogoro wa
ardhi, ni mgogoro wa
watoto, ni mgogoro /kosa la
jinai, ni mgogoro wa biashara au
madai mengineyo kama
ya fidia, ni mgogoro
unaohusu mila na sheria
za
kiislamu n.k.
Haya yote matatu
yatakupa majibu sahihi
wapi ukafungue shauri ili kuepuka
kufutiwa kesi na
kupoteza madai yako
ya msingi. Hapa chini
tutaona mambo hayo
matatu yanavyohusika katika
kupata mahali sahihi
pa kufungua kesi.
3. MAHAKAMA SAHIHI
KWA SHAURI LAKO.
( a ) MAHAKAMA YA
MWANZO.
Mahakama ya
mwanzo iliyo katika
eneo lako unaweza
kufungua mashauri ya
mirathi. Utafungua pia mashauri
yote ambayo yanahusisha sheria za
kimila na za kiislamu mfano masuala
ya talaka na ndoa.
Kwa mashauri mengine
ya madai utapeleka mgogoro
ambao thamani yake
haizidi milioni 3 kwa mgogoro unaohusu
mali inayohamishika na kwa mgogoro
unaohusu mali isiyohamishika isizidi milioni 5.
Lakini pia lazima
iwe Mahakama ya mwanzo
ya eneo lilipotokea tukio.
( b ) MAHAKAMA YA
WILAYA NA MAHAKAMA YA
HAKIMU MKAZI.
Iwe ni mahakama ya
wilaya iliyo katika
eneo lilimotokea tukio
linalokupeleka mahakamani.
Lakini pia thamani ya
mgogoro kwa mali
inayohamishika usizidi mlioni 100 na
kwa mali isiyohamishika usizidi
milioni 150.
Mahakama za
hakimu mkazi ni
zile ambazo wengine
huita mahakama za
mkoa. Pia mahakama hizi hupokea rufaa
kutoka mahakama za mwanzo.
( c ) MAHAKAMA
KUU.
Hii hupokea migogoro kutoka
katika wilaya na
mikoa yote katika nchi. Thamani
ya mgogoro ni
kuanzia milioni 100 kwenda
mbele bila ukomo
kwa mali inayohamishika na
kuanzia milioni 150 kwenda
mbele bila ukomo
kwa mali isiyohamishika. Pia
hupokea rufaa kutoka
mahakama za wilaya
na hakimu mkazi.
( d ) MAHAKAMA MAALUM.
Hizi hushughulikia
masuala maalum katika
nchi. Kwa mfano ukiwa na
mgogoro wa ardhi
utapeleka baraza la
ardhi la kijiji, la
kata, la wilaya
na baadae mahakama
kuu kitengo cha
ardhi.
Ukiwa na mgogoro
wa kazi na ajira utapeleka
tume ya usuluhishi, baadae tume
ya uamuzi na baadae
mahakama kuu kitengo
cha kazi. Mgogoro mkubwa
wa kibiashara ni
mahakama kuu ya
biashara.
Kwa ujumla huu ni mwongozo
mfupi tu wa wapi
ukafungue kesi.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI
KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA
JUMATANO.
0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.com
Baada ya kuona chapisho kwenye mtandao la Jenna kutoka USA akisema jinsi alivyosaidiwa na Dk. DAWN, niliamua pia kuwasiliana naye kwa msaada kwa sababu sikuwa na chaguo nilichotaka ni kumrudisha mpenzi wangu na furaha. Kwa mshangao mkubwa mpenzi wangu alifika nyumbani akiwa amepiga magoti kwamba nitafute nafasi moyoni mwangu kumsamehe, hakika nilistaajabu na kushtuka mpenzi wangu alipopiga magoti akiomba msamaha na mimi nimkubalie tena. Kweli nimepungukiwa na maneno, na sijui ni kiasi gani cha kukushukuru wewe Dr. DAWN. Wewe ni Mungu aliyetumwa kurejesha uhusiano uliovunjika, Na sasa mimi ni mwanamke mwenye furaha. mawasiliano yake ni Whatsapp +2349046229159
dawnacuna314@gmail.com