NA BASHIR YAKUB -
1.KUTELEKEZA WATOTO/MTOTO. Ni kosa la jinai. Ni
kinyume na kifungu cha
166 cha Kanuni za adhabu.
Adhabu yake ni
kifungo cha miaka
miwili. Kosa linamhusu mzazi, mlezi, au mwingine
yeyote aliye na jukumu la kuangalia
watoto/mtoto.
2.KUKATAA KUMPA
CHAKULA NA NGUO MTOTO. Ni
kosa la jinai. Ni kutokana na kifungu
cha 167 cha
kanuni za adhabu. Adhabu yake
ni kifungo cha miaka miwili.
3.KUMNYIMA CHAKULA NA NGUO
MTUMISHI. Ni kosa la jinai. Ni kutokana na kifungu cha
168 cha kanuni za adhabu. Adhabu yake ni kifungo cha miaka miwili. Watumishi wa hapa ni
wale wanaotegemea matajiri
wao kama wale
wa wafanyakai wa ndani n.k.
4.UKATILI KWA WATOTO. Ni kosa la jinai. Ni kutokana na kifungu cha 169A cha
kanuni za adhabu. Adhabu yake ni kifungo
kisichopungua miaka mitano na kisichozidi miaka kumi na tano.
5.KUHARIBU MTOTO. Ni kosa la jinai. Ni kutokana na kifungu cha 219( 1 ). Adhabu yake ni kifungo cha maisha.
6.KUFICHA KUZALIWA KWA MTOTO. Ni
kosa la jinai. Ni kutokana na kifungu
cha 218 cha kanuni za adhabu.
Adhabu yake ni kifungo cha miaka miwili.
7.KUJARIBU KUJIUA. Ni kosa la jinai. Ni kutokana
na kifungu cha 217 cha kanuni za adhabu. Adhabu yake ni kifungo cha miaka miwili.
8.KUMSAIDIA ANAYETAKA KUJIUA. Ni kosa la jinai. Ni kutokana na
kifungu cha 216 cha kanuni za
adhabu. Adhabu yake ni
kifungo cha maisha.
9.KUFANYA FUJO HADHARANI. Ni kosa la jinai. Ni kutokana na kifungu cha 87 cha kanuni za adhabu. Adhabu yake ni kifungo cha miezi sita.
10.LUGHA YA MATUSI NA UGOMVI. Ni kosa la jinai. Ni kutokana na kifungu cha 89( 1 ) cha
kanuni za adhabu. Adhabu yake ni kifungo cha miezi sita.
11.KUCHOCHEA MAPIGANO YA WAWILI. Ni kosa la jinai. Ni kutokana na kifungu cha 88 cha kanuni
za adhabu. Adhabu yake ni kifungo cha miaka miwili.
12.VITISHO. Ni
kosa la jinai. Ni kutokana na kifungu cha 89B cha kanuni za adhabu. Adhabu yake
ni kifungo cha mwaka mmoja.
13.KUPUUZIA WAJIBU WA KIOFISI. Ni kosa la jinai. Ni kutokana na kifungu cha 121 cha kanuni za adhabu. Adhabu yake ni kifungo
cha miaka saba.
14.KUZUIA KUZIKWA/MAZIKO. Ni kosa la jinai. Ni kotokana
na kifungu cha 128
cha kanuni za adhabu. Adhabu yake
ni kifungo cha miaka miwili.
15.KUBAKA. Ni
kosa la jinai. Ni kutokana na kifungu cha 131 cha kanuni za adhabu. Adhabu yake ni
kifungo cha maisha
na viboko au bila viboko.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI
KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA
JUMATANO. 0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment