NA BASHIR YAKUB -
Katika saa za
kazi zipo saa
za kazi katika
siku za kawaida, saa
za kazi za ziada
na saa za
kazi katika siku ambazo ni
za sikukuu. Kuna umuhimu
mkubwa sana kwa mfanyakazi kujua
masaa ya kazi .
Kama hujui masaa ya kazi ya
kisheria basi ni vigumu
kujua usahihi wa
ujira unaolipwa .
Malipo ya
kazi hayatokani na mshahara pekee. Yapo
malipo mengine ya
ziada yatokanayo na
muda wa ziada zikiwemo siku
za sikukuu. Ili ujue
usahihi wa kile unacholipwa
yakupasa kujua pia mchanganuo wa masaa
ya kazi. Masaa
ya kazi yapo
aina mbili.
Yapo masaa
ya kazi ya kawaida na
yapo masaa ya kazi ya
ziada. Sikukuu nazo hujumuishwa
katika masaa ya
kazi ya ziada.
1.JE SAA
ZA KAZI NI NGAPI KATIKA SIKU ZA
KAWAIDA ?.
Katika siku za
kawaida saa za kazi
ni 9. Kwahiyo kwa siku
mfanyakazi anatakiwa kufanya
kazi masaa 9. Hii
ina maana atafanya
kazi masaa 45 kwa wiki ikiwa atafanya kazi kuanzia jumatatu mpaka ijumaa.
Muhimu sana katika
suala la saa za
kazi ni kuwa
mfanyakazi asifanye kazi zaidi
ya saa 45 kwa
wiki kwa masaa ya kawaida.Hata
siku zikizidi lakini
masaa 45 kwa
wiki yasipite. Hayo ni
masaa ya kawaida.
2. JE
SIKU ZA KAZI NI
NGAPI ?.
Siku za kazi
zinazoruhusiwa ni sita
kwa wiki. Lakini itategemea na
taratibu za ofisi
yako. Zipo ofisi watakwambia tunafanya kazi jumatatu
mpaka ijumaaa na
wapo wengine watakwambia
kazi ni jumatatu
mpaka jumamosi. Hawa wote
watakuwa hawajakosea kwasababu bado wako ndani
ya ukomo wa siku za
kisheria.
Linalopaswa kuzingatiwa hapa
ni kuwa vyovyote
itakavyokuwa masaa ya
kazi kwa wiki
yasizidi 45. Iwe siku
tano kwa wiki au sita muhimu
masaa yasizidi 45 kwa
wiki. Haya ni
masaa ya kawaida. Masaa
ya kawaida ni yale
masaa ambayo sio
ya ziada.
3. TOFAUTI
KATI YA SIKU
5 ZA KAZI
NA SIKU 6 ZA KAZI.
Tumesema masaa ya
kazi kwa wiki
yasizidi masaa 45
iwe kwa kufanya
kazi siku tano
kwa wiki au
sita kwa wiki. Hii
ina maana yule anayefanya siku
tano kwa wiki
atatakiwa kufanya kazi
masaa 9 kwa siku ili iwe 9 x siku 5 = 45 masaa ya ukomo kwa wiki.
Lakini yule anayefanya
kazi siku sita
kwa wiki itatakiwa iwe
masaa manane kwa
siku tano yaani 8 x 5 = yaje
masaa 40 labda hiyo ni jumatatu
mpaka ijumaa, halafu masaa
5 jumamosi ili
hesabu ya masaa
45 kwa wiki isivuke. Hivyo
itakuwa 8 x 5= 40
halafu + masaa 5 ya jumamosi = 45
masaa kwa wiki.
4. MASAA YA
ZIADA.
Mfanyakazi
anayefanya kazi masaa
9 kwa siku, kwa siku
sita katika wiki anatakiwa
kulipwa malipo ya
masaa ya ziada.
Atakuwa amefanya kazi
masaa 9 x siku 7 =63 masaa
kwa wiki kutoka masaa
45 yanayotakiwa. Hivyo 63 – 45 = masaa 18 ya
ziada yanayostahili malipo nje
ya mshahara.
5. MALIPO YA
ZIADA NI
KIASI GANI ?.
Mfanyakazi
atakayefanya kazi saa
za ziada basi
atatakiwa kulipwa 1.5 ya
mshahara wake wa saa
kwa kila
saa lililozidi. Mshahara unaopokea
unaweza kuugawa ukaona
kwa saa unalipwa
kiasi gani. Ukishapata jibu chukua 1.5
ya kiasi hicho.
Hiyo 1.5 ndiyo
unayotakiwa kulipwa katika
kila saa lililozidi.
6. KAZI SIKU
ZA SIKUKUU.
Masaa ya kazi ya
siku za
sikukuu yote ni
masaa ya ziada
kuanzia asubuh hadi
mfanyakazi anapoondoka. Lakini
malipo ya ziada
ya siku za
sikukuu ni zaidi
ya malipo ya ziada ya siku
za kawaida.
Hapo juu tumesema
1.5 ya mshahara wa
saa ndiyo hulipwa
kwa kila saa
lililozidi. Hata hivyo
kwa sikukuu itakuwa
mara mbili yake . Itakuwa 1.5 x 2 kwa
kila saa.
Yapo mengi ila
haya yatoshe kwa
leo.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI
LA SERIKALI LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI KILA
JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA JUMATANO.
0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.com
asante kwa maelezo mazuri ya kisheria: Naomba kuuliza iwapo nimefanya kazi kwa muda wa ziada kwa masaa 50 mwezi ni fomula gani itatumika kukokotoa malipo?
Je,kuna FIXED OVERTIME listeria na inahusu wafanyakazi wote au baadhi wenye hadhi flani?
Naomba kuuliza siku ya jumapili inachukuliwa kama saa za ziada?
Mimi Amos Masamaki nimesitishiwa mkataba wangu wa kazi je nini ninastahili kulipwa?