NA BASHIR YAKUB -
Mara kadhaa imetokea
mtu anahitaji kununua
ardhi sehemu ambayo yeye
haishi. Mara nyingi
hii imetokea kwa
walio nje ya
nchi. Mtu anaona
kiwanja au nyumba
kwenye mtandao au
kwenye chombo chochote
cha habari lakini
anakosa namna ya
kununua.
Saa nyingine
hufanya mawasiliano na
wahusika hadi kufika
bei lakini tatizo likawa
ni vipi atanunua.
Vipi ataweza kununua bila
kuhitaji kurudi nchini hubaki mtihani.
Anapiga mahesabu ya
nauli kwenda na
kurudi, usumbufu, ratiba ya kazi zake na
mambo mengi anaona haiwezekani. Anashindwa
kununua kwasababu tu
ya umbali. Na hii
si
kwa walio nje
ya nchi tu
bali hata walio mikoa
tofauti pia hili
huwatokea japo si
sana.
Pia wako wengine
ambao tatizo sio
kuwa mbali na
maeneo wanayotaka kununua
bali wana shughuli nyingi
mno kiasi cha kutopata mda
mzuri wa kufuatilia
miamala ya manunuzi
mpaka mwisho.
Hawa wote na
wengine wengi kupitia
makala haya watajua namna
ambavyo wanaweza kununua ardhi
bila kuhitajika kuwepo.
1.TARATIBU ZA
KUNUNUA ARDHI.
Imewahi kuelezwa mara
nyingi namna bora
na salama ya kununua ardhi lengo
likiwa hasa kuepuka
utapeli, kuepuka kuuziwa
mara mbili au
zaidi kwa watu tofauti(
double allocation), kuepuka kununua
maeneo yenye migogoro
mahakamani, maeneo yaliyowekewa
mazuio( injuction & caveat), kuepuka
kununua maeneo yasiyo
na hati za
mirathi, yaliyowekwa dhamana n.k.
Tulieleza hatua za
kufuata ili kuyaepuka haya sambamba
na maandalizi ya
mkataba wa mauzo
yanayokidhi vigezo mahususi
vya kisheria. Ni vema
kila mda kusisitiza kuwa
migogoro ya ardhi
inazidi kuongezeka kila
siku na watu
hupata hasara kila
kukicha.
Lakini unaweza kuepuka
kuwa sehemu ya
migogoro hii ikiwa
tu utafuata taratibu
pamoja na kuzingatia
maandalizi mazuri ya
mkataba wa mauzo unaokidhi vigezo
vya kisheria.
2. KUMTUMA MWAKILISHI
KUKUNUNULIA ARDHI.
Namna ya kisheria inayoweza
kutumika kununua ardhi
bila kuhitaji wewe mwenyewe
kuwepo ni kwa kutumia hati
maalum iitwayo hati
ya kiwakili( power of attorney).
Hii
ni hati maalum
inayoweza kutumika kisheria
kwa ajili ya
kazi hii.
3. HATI YA
KIWAKILI NININI.
Hati ya kiwakili (power of
attorney) ni hati
maalum ya kisheria ambapo
mtu mmoja anampa
mtu mwingine mamlaka
ya kisheria ya kutenda jambo fulani
la kisheria kwa niaba
yake. Katika masuala
ya ardhi mtu
anaweza kumpa mtu
mwingine mamlaka ya
kuuza au kununua
nyumba au kiwanja kwa
niaba yake.
Hii ina maana
kama uko nje ya
nchi na unahitaji
kununua kiwanja au
nyumba unachoweza kufanya
ni kuandaliwa hati
ya kiwakili ambayo utakuwa ukimpa
mamlaka mtu fulani ambaye anaweza kuwa kaka, dada,
mama, baba, rafiki
au yeyote yule utakayemchagua ambaye
ataweza kununua kwa ajili
yako.
Haina haja ya
kuhofu kwa kuwa nyaraka itakuwa
imeeleza wazi kuwa mmiliki ni
wewe isipokuwa huyu
amesaidia tu kukununulia.
4. MAMLAKA UTAKAYOMPA.
Hati ya kiwakili
inatoa mamlaka lakini
mamlaka yenye ukomo. Hii
ina maana unaweza
kumpa mamlaka ya
kununua kwa ajili
yako lakini si
ya kuuza, kuweka
rehani, au vnginevyo.
Kwa
hiyo atanunua kwa
ajili yako lakini
hatakuwa na uwezo
wa kuuza au
kufanya kingine chochote
ambacho hakikuandikwa kwenye
hiyo hati ya
kiwakili.
5. HATI YA
KIWAKILI INAPATIKANA WAPI.
Hati ya kiwakili
huandaliwa na wanasheria
ambapo inakuwa na jina
la mtoa mamlaka
na mpewa mamlaka
na wote hutakiwa
kusaini kwa utaratibu
utakaokubaliwa.
Itaeleza wazi
mamlaka aliyopewa mpewa
mamlaka pamoja na
ukomo wa mamlaka
hayo. Baada ya hapo
hati hiyo itasajiliwa
wizara ya ardhi
na manunuzi salama
na ya kisheria
yanaweza kufanyika kuanzia
hapo bila kuhitaji
aliye nje ya
nchi kurudi au
vinginevyo.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI
KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA
JUMATANO. 0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment