NA BASHIR YAKUB -
Baadhi ya wasomaji
wameuliza maswali mengi kuhusu
habari ya umiliki
wa mali kwa
wanandoa. Wanataka kujua ipi
mali ya ndoa
na ipi siyo, wanataka kujua mali
unayokuwa nayo kabla
ya ndoa inahesabika
vipi baada ya kuingia nayo
katika ndoa, wanataka kujua uuzaji
wa mali za
ndoa, wanataka kujua kigezo
kinachozingatiwa katika kugawana
mali ndoa inapovunjika, wanataka kujua iwapo
inawezekana kuwa na umiliki wa
pekee wa mali wakati upo
katika ndoa, wanataka
kujua haki ya mali kwa
ndoa ya mke zaidi
ya mmoja, wanataka kujua
nani kati ya
mume na mke
ana haki zaidi
ya mali na mengine mengi.
Haya yameulizwa na
watu tofauti lakini
kwa wingi. Hata hivyo mengi yake
yalikwisha elezwa hapa. Mengi yameelezwa
katika makala tofauti zilizopita.
Tunaamini wapo
walioona na wengine
hawakuona. Kwasababu hiyo hakuna
ubaya kujibu tena
maswali ya aina
hii ili hata ambao
hawakubahatika kusoma waweze
kusoma leo.
1.JE NDOA
INAPOVUNJIKA NI KIGEZO KIPI
HUTUMIKA KATIKA KUGAWA
MALI ZA WANANDOA.
Iliwahi kuelezwa hapa
kuwa wengi wanajua kuwa
katika kugawana mali
za ndoa pale
ndoa inapovunjika kigezo
kinachotumika ni cha
asilimia. Wanajua kwamba sheria
imeeleza wazi kuwa
kuna asilimia fulani
anatakiwa kupata mwanamke
na asilimia fulani
mwanaume.
Hili si
kweli kwani kigezo
kikubwa kinachotumika ni
kigezo cha nguvu au
juhudi za pamoja
katika upatikanaji mali( joint
effort) husika. Juhudi za pamoja
huangaliwa mchango wa kila
mmoja katika upatikanaji
au uendelezaji wa
mali husika.
Na juhudi za pamoja
sio tu pesa au
mali bali pia
hata kazi za
nyumbani nazo ni sehemu
ya juhudi za
pamoja katika kupatikana
kwa mali.
Kwahihyo juhudi ya kila
mmoja itapimwa na
mali zitagawanywa. Mahakama ndio chombo chenye
mamlaka na kazi hiyo.
2. JE MALI
UNAYOINGIA NAYO KATIKA NDOA
INABADILIKA NA KUWA
YA WOTE.
Kifungu cha 58
cha sheria ya
ndoa kinasema kuwa
ndoa haitatumika kubadilisha
umiliki wa mali isipokuwa
kama kuna makubaliano maalum au
vinginevyo.
Hii ina
maana ndoa tu
haibadilishi umiliki na
kuufanya kuwa wa pamoja.
Mali inaweza kuwa
ya mtu mmoja
awe mke au mme
labda iwe vingenevyo kuwa kuna
makubaliano maalum kuwa
mali hii itakuwa
ya wote.
Pia kunaweza
kusiwe na makubaliano
hayo lakini mmoja
akawa amechangia katika kuiendeleza
mali ile. Hapo napo
inaweza kuwa ya
wote. Lakini kinyume
na hayo mali
inaweza kuendelea kuhesabika ni ya mmoja
kati ya mke
au mme hata
kama wako kwenye ndoa.
3. JE HAKI
YA MALI IKOJE
PENYE MKE ZAIDI
YA MMOJA.
Kifungu cha 57
cha sheria ya
ndoa kinasema kuwa ili
kuondoa shaka inapotokea
mme ana mke zaidi ya
mmoja basi wake hawa
watahesabika wana haki
sawa , hadhi sawa na dhima
sawa. Isipokuwa sasa suala
la mali ikiwa ndoa
ya mmoja au wote itavunjika basi
kila mtu atapata kutokana na
mchango wake katika
kupatikana hizo mali.
4. JE MWANANDOA ANAWEZA KUUZA MALI
BILA RIDHAA YA
MWENZAKE.
Kifungu cha 59 cha
sheria ya ndoa
kinasema kuwa mali
ardhi inapokuwa inamilikiwa
na mume au mke
wakati ambapo ndoa
ikiendelea basi mmoja
kati ya wanandoa
hao hataruhusiwa kuuza,
kutoa zawadi, kuweka rehani, au kupangisha .
Na ikitokea akafanya hivyo
basi yule ambaye hakuhusika naye atahesabika kuwa
na maslahi yanayompa
haki ya kuzuia(caveat) hicho
kilichofanyika.
Kwa leo ni
hayo mengine yataelezwa
katika makala nyingine.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI
KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA
JUMATANO. 0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment