NA BASHIR YAKUB -
1.WAKFU NININI.
Sheria ya Mirathi na Usimamizi
Mali Sura ya 352
ndiyo sheria inayoeleza
masuala yote ya
msingi kuhusu habari
nzima ya Wakfu. Kwa
mujibu wa sheria hiyo kifungu
cha 140 Wakfu
ni kutoa mali
kulingana na sheria za
kiislam kwa ajili
ya dini, hisani au
kwa ajili ya watu/mtu
wa familia fulani.
Suala la Wakfu
huenda sambamba na
suala la wadhamini. Kwa
mujibu wa kifungu
hicho wadhamini ni
watu/mtu ambaye ndiye
hupewa jukumu la
kusimamia mali ya
wakfu.
Kama ni nyumba
yenye wapangaji basi mtu
au watu hao ambao ni wadhamini
ndio watahusika na
kukusanya kodi pamoja
na mambo mengine
yote yanayohusu nyumba. Na
kama kuna maendelezo
yoyote ya ukarabati au vinginevyo
hawa ndio watahusika.
2. MAELEKEZO YA
MTOA WAKFU LAZIMA YAFUATWE.
Siku zote mtoa
wakfu hutoa mali
kwa malengo maalum. Yaweza kuwa
malengo ya kiimani
au vinginevyo. Mtoa wakfu
anapotoa nyumba/kiwanja kama
wakfu hutoa kwa
maelekezo ya namna
na jinsi kitakavyotumika. Kwa namna
mtoa wakfu atakavyotoa
maelekezo ndivyo hivyo
inavyotakiwa kuwa.
Ni kosa mali
ya wakfu kutumika
kinyume na maagizo
ya mtoa wakfu. Ikiwa
itatumika kinyume basi
kuwe na sababu
za msingi ambazo
zinalazimisha hivyo. Ziwe ni sababu
ambazo hakuna namna isipokuwa
ni lazima kufanyika hivyo.
Kifungu
cha 150( 1 ) cha sheria ya
mirathi na usimamizi
wa mali kinasema
kuwa matumizi ya
mali za wakfu
ni lazima yazingatie
nia na malengo
ya mtoa wakfu.
Isipokuwa kifungu hicho
kinasisitiza kuwa nia
na malengo ya
mtoa wakfu yatafuatwa
tu pale ambapo
nia na malengo
hayo yatakuwa halali
kisheria. Ikiwa mtoa wakfu
ameelekeza matumizi ambayo
hayakubaliki kisheria basi
maelekezo hayo hayatafuatwa. Lakini ikiwa
hayapingani na sheria
yoyote
basi ni sharti
kuyafuata.
3. IFAHAMU TUME
YA WAKFU.
Kuna chombo cha
kisheria kinaitwa tume/bodi
ya Wakfu Tanzania ( Wakfu Commission of Tanzania). Kazi kubwa
ya chombo hiki ni
kusimamia na kuratibu
mali zote za
wakfu. Wakfu ili
uweze kulindwa na sheria
hii hutakiwa
kusajiliwa.
Chombo hiki
ndicho kinachohusika na
usajili.
Kifungu cha 145( 6 ) kinasema kuwa mali
ya wakfu inatakiwa
kusajiliwa ndani ya
miezi mitatu tangu
iwe mali rasmi
ya wakfu. Pia
kamati ya wadhamini
ambayo ndiyo inasimamia mali
za wakfu nayo
hutakiwa kusajiliwa ndani
ya miezi mitatu
tangu kuundwa kwake.
Pia mgogoro
wowote unaotokana na
mali ya wakfu
husuluhishwa na chombo
hiki.
4. NINI
UFANYE MALI YA
WAKFU INAPOTUMIKA VIBAYA.
Wakati mali ya
wakfu inapotumika vibaya
au kufujwa basi
yeyote mwenye maslahi anaweza kuibua
malalamiko. Kifungu cha 146 cha
sheria ya mirathi na
usimamizi mali kinasema
kuwa malalamiko yatapelekwa
kwenye tume/bodi ya
Wakfu.
Lakini pia kifungu
hichohicho kinatoa mamlaka
kwa tume yenyewe
kuchukua hatua hata
kama hakuna mtu
aliyelalamika. Tume itachukua
hatua mara moja
itakapoona mali ya
wakfu inatumika kinyume
na malengo ya
mtoa wakfu au kuna
ufujaji wowote unaofanywa.
Kifungu hicho kinasema
kuwa tume/bodi itafanya uchunguzi na
ikigundua kuwa kuna
mambo hayako sawa
katika usimamizi wa wakfu
basi inaweza kuichukua
ile mali ya wakfu na
kuiweka chini ya
usimamizi wake au
kuteua wadhamini wengine
ili kusimamia vyema
mali hiyo.
Yapo mengi kuhusu
wakfu lakini kwa
leo ni hayo.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI
KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA
JUMATANO. 0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment