NA BASHIR YAKUB -
Uhaini ni kosa la jinai .
Ni kosa kati
ya makosa makubwa
ya jinai. Katika
jinai yapo makosa
makubwa na yapo
makosa madogo. Yumkini
udogo na ukubwa
wa kosa waweza
kupimwa kwa kutizama
adhabu ya kosa.
Kosa ambalo huadhibiwa
kwa adhabu ndogo
huwa ni kosa
dogo na lile
ambalo huadhibiwa kwa
adhabu kubwa huwa
ni kosa kubwa.
1.NI SHERIA IPI HUELEZA
MAKOSA
YA JINAI.
Sheria zinazofafanua makosa
ya jinai zipo
nyingi. Hakuna sheria moja katika makosa
ya jinai. Hata
hivyo sheria kuu
katika makosa ya
jinai ipo. Ni sheria
inayojulikana kama kanuni
za adhabu( penal code).
Hii ni sheria kuu
katika makosa ya jinai.
Ni sheria inayoeleza
karibia makosa yote ya
jinai. Mbali na
sheria hiyo pia
zipo sheria nyingine kama za
kuzuia na kupambana
na rushwa, sheria ya
uhujumu uchumi, sheria ya
ugaidi na nyinginezo. Hizi
nazo hueleza makosa ya
jinai.
Tofauti kubwa kati ya sheria hizi
na ile ya
kanuni za adhabu
ni kuwa hizi sheria nyinginezo
hueleza makosa rasmi
ya jinai. Kwa mfano sheria
ya
ugaidi itaeleza mambo
ya ugaidi tu
na si vinginevyo, sheria ya
uhujumu uchumi itaeleza
makosa yanayotokana na
uchumi tu na si
vinginevyo, sheria ya
utakatishaji fedha itaeleza
utakatishaji fedha tu
na si vinginevyo.
Wakati sheria ya
kanuni za adhabu
ndani mwake utakuta
makosa tofauti tofauti
ya jinai. Utakuta makosa ambayo
hayafanani na yasiyokuwa na
uhusiano.
Utakuta kuhusu kubaka,
kuiba, kupigana, kuua, kuharibu
mali, rushwa, kughushi , uhaini na
mengine mengi. Kwahiyo kwa
mtu anayehitaji kuyajua makosa
ya jinai basi na
asome sheria ya
kanuni za adhabu.
2. UKIFANYA
HAYA UTAKUWA UMETENDA
UHAINI.
( a ) Kifungu cha 39
( 1 ) cha kanuni
za adhabu kinasema
kuwa mtu yeyote
ambaye yumo
ndani ya Jamhuri
ya muungano au
popote akajaribu kumuua
rais atakuwa ametenda uhaini.
( b ) Pia
mtu yeyote aliye
ndani ya Jamhuri
ya muungano au
popote na akaanzisha
vita dhidi ya
Jamhuri ya muungano
atakuwa naye ametenda
kosa la uhaini.
( c ) Mtu
yeyote ambaye yuko
ndani ya Jamhuri
ya muungano au popote ambaye atajenga,
kusababisha au kuwezesha,
kuchochea, kushawishi, kushauri, kuhusu kifo, kumlemaza, kumzuia, au
kufungwa kwa rais
atakuwa ametenda uhaini.
( d ) Mtu
yeyote ambaye yuko
ndani ya Jamhuri
ya muungano au popote ambaye atajenga,
kusababisha au kuwezesha,
kuchochea, kushawishi, kushauri
kumwondoa rais madarakani
visivyo halali atakuwa
ametenda uhaini.
( e ) Mtu
yeyote ambaye yuko
ndani ya Jamhuri
ya muungano au popote ambaye
atajenga, kusababisha au
kuwezesha, kuchochea, kushawishi,
kushauri kumwondolea rais
heshima na jina
la mkuu wa
nchi, amiri jeshi
mkuu, au kiongozi
wa serikali atakuwa
ametenda kosa la
uhaini.
( f ) Mtu
yeyote ambaye yuko
ndani ya Jamhuri
ya muungano ambaye
atajenga, kusababisha au
kuwezesha, kuchochea, kushawishi,
kushauri kupindua serikiali
iliyo madarakani, kutishia serikali, bunge au
mahakama atakuwa ametenda
kosa la uhaini.
3. NI
IPI ADHABU YA
KOSA LA UHAINI.
Vifungu vya 39
na 40 vya kanuni
za adhabu ambavyo
vimeeleza ni matendo gani
yanaweza kuitwa uhaini vimeeleza
pia adhabu ya
matendo hayo. Vimeeleza kuwa
adhabu ya kukutwa
na hatia ya
uhaini ni kifo. Uhaini
ni kati ya makosa
machache sana ambayo
adhabu yake ni kifo.
Kwahiyo kwa namna
yoyote ukijihusisha na tendo lolote kati ya matendo yaliyotajwa hapo
juu ndipo utahesabika
umetenda uhaini na adhabu
yake ni kifo
ikiwa itathibitika mahakamani. Kila kilichoelezwa
hapo juu katika A – F ni tafsiri
halisi ya uhaini.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI
KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA
JUMATANO. 0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment